Songwe: Raia wampiga anayedaiwa kuwa mlinzi wa JKT aliyejificha kukamata magendo

Songwe: Mtu anayedaiwa kuwa ni mlinzi wa Kampuni ya Suma JKT, Emmanuel Myela (35) mkazi wa Wilaya ya Mbozi, amelazwa katika hospitali teule ya rufaa mkoani hapa, baada ya kushambuliwa na wananchi wenye hasira, alipokuwa akivizia watu wanaosafirisha bidhaa za magendo toka nchi jirani ya Malawi jana Oktoba 17.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Janeth Magomi alipoulizwa kwa simu kuhusu tukio hilo amesema kwa sasa hawezi kulizungumzia kwa kuwa hakuwa na taarifa iliyo kamili.

Mmoja wa shuhuda aliyekuwepo eneo la tukio, Mussa Mgode amedai kwamba askari hao ambao walikuwa watatu hawakuvalia sare za jeshi wakiwa na pikipiki mbili walifika eneo hilo majira ya saa 9 alasiri kisha walimkamata mtu mmoja waliyedai kuwa amebeba magendo hao.

Alisema baada ya kumkamata mtu huyo palitokea mabishano kati yao na ndipo walipojitokeza wenzao kadhaa ambao waliamua kupambana na ‘askari hao’.

Kama hiyo haitoshi, shuhuda huyo alisema lilijitokeza kundi la wananchi waliokuwa wakitokea kwenye msiba na kuanza kuwasaidia vijana hao na ndipo askari wawili walifanikiwa kukimbia kusikojulikana wakizitelekeza pikipiki zao mbili ambazo baadaye zilichomwa moto na wakazi hao.
Hata hivyo, mmoja wao aliyebaki alikimbilia iliyo jirani na kujifungia, lakini wananchi kwa hasira walivunja dirisha la nyumba hiyo na kumtoa nje na kuanza kumshushia kipigo kikali kabla ya Polisi kufika na kumuokoa.

Kaimu Mganga Mfawidhi, Dk Lighton Alex amethibitisha kumpokea majeruhi huyo akiwa hajitambui kutokana na kipigo.

Amesema askari huyo alifikishwa katika Hospitali hiyo kwa gari ya polisi baada ya kuokolewa kwenye kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali.

Amesema baada kumfanyia vipimo vya mionzi ilibainika kuwa majeruhi huyo alipata mpasuko kwenye fuvu lake la kichwa.

Ameongeza kuwa, mtu huyo ana majeraha mbalimbali kwenye mikono yake yote miwili, pamoja na mguu wa kulia, hivyo kutokana na hali hiyo atapatiwa rufaa ili akapatiwe matibabu ya juu zaidi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mpanda, George Mwambubha lilipotokea tukio hilo, amesema mara kadhaa watu hawa (askari) wamekuwa wakifika kijijini hapo na kukamata vijana wanaosafirisha magendo ya mafuta ya kula na pombe za viroba kutoka Malawi, lakini jana ilikuwa tofauti.

Source:Mwananchi
Safi sana
 
Sasa mkibana kila mahali watu watapumulia wapiiii...

Acheni watu wapumue.
Unaona Mfano JW,POLICE, Na Sehemu Nyingi Wale Viongozi Wa Juu Hutupwa Sehemu Nyingine Huko Ili Taasisi, Idara, Vitengo
Vipumue Vizuri
 
Mwenyekiti wa Kijiji anahitaji kuelimishwa namna ya kuimarisha kamati yake ya ulinzi na usalama wa Kijiji ili kupunguza magendo kukatiza eneo lake....
 
Kwa Comment hizi ndo maana Police hana Damiss kwa Raia wakikamata ni kipigo nyokoleee kwa raia.

Na Raia wakinasa nikipigo...[emoji23]

Ila poa hakuna kumaindiana atakae jaa kwa mwenzie basi avumilie kupigwa bomba na mijebu[emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom