Soon nakuwa mama wa kambo. Nahitaji maombi yenu na ushauri wa maisha haya mapya

Unataka kujiandaa kisaikolojia kwani unaletewa fisi ufuge? We jilazimishe hakikisha anapata chakula, mavazi, malazi na elimu kama wanao. JILAZIMISHE maana kumpenda mtu si uamuzi. Hatuchagui kupenda. Si lazima umpende, ila mahitaji yake ni lazima.
 
Ndugu yangu kuna wanawake walihisi waume zao wakichukua watoto wao wa nje itawafanya watulie na ndoa zao, walikuja kushangaza baby momma ana watoto wengine na mume wake. Kuna watu waliamua kuachana seriously na wanawasiliana kwa ajili ya mtoto tu, mengine kila mtu anapambana na maisha yake. Mimi mume wangu hawezi piga simu kwa baby momma kila saa in the name of kumjulia hali mtoto; siruhusu huo upumbavu. Mawasiliano yawepo ila kuwe na mipaka, sio mtoto kakohoa simu, kapiga chafya simu. Hata mkimchukua mtoto, itakuwa zamu ya mama yake na yeye kupiga simu kwako kila wakati kumjulia hali kwa sababu umeshamzoesha hivyo. Huna justification my brother.

Na ukute mkeo kagundua kuwa mnapashana viporo ndiyo maana kagoma kumchukua na mtoto. Apambane yeye kulea afu nyie mkutane kufanyana kwa amani? Na kama unahisi anafahamu mnavyochepuka, unahisi ni mjinga sana karuhusu hilo au ndiyo kamuachia Mungu? Na kwa style hiyo jiandae kwa vita kati ya watoto wako, utafurahi kwa kweli. Wewe kuzaa njw humkomeshi mkeo bali watoto wako.

Huyo baby momma anaku-entertain kwa sababu bado anakutaka na yupo single; unafikiri angekuwa na mahusiano yake serious au ameolewa angekuruhusu upigepige simu kila wakati mbele ya mume wake? Baby momma kakuzidi akili na wewe unacheza tu beat lake, unavunja ndoa yako taratibu. Mwanaume mpumbavu hujisababishia kifo chake mwenyewe. Jikute sasa unamkomesha mkeo, mwisho wa siku utaona nani atakomesheka

C.c @espy
 
Nampenda sana mama yangu japo si wa kunizaa.
Baba angu aliniiba kwa mama yangu mzazi nikiwa na miezi mi 3 tu duniani akanileta kulelewa kwa huyu mama ambae ndio mkewe wa ndoa.nikawa mtoto wake wa 5.Namkubali sana lich ya mapungufu yake ambayo wengine huwa wanalazimisha niyaone ila hata siyaonagi
 
Bado sijaona shida iko wapi,ila inaonekana unakauchoyo fulani na roho mbaya tofauti na hapo sijaona kutu cha kudoubt
 
Mi pia namfeel sana shangazi yangu kuliko hata mama yangu yaani alinichukua nikiwa mdogo lakini alinilea kama binti yake yaani mpaka kuna vitu nkikumbuka nabaki kujiuliza ntamlipa nini shangazi yangu alafu pia nilijifunza kwamba anaroho nzuri ya kuzaliwa nayo maana kuna watoto wa marehemu shemeji yake tulikuwa tukiishi nao lakini nao walikuwa kama watoto wake
 
Ndoa gani hio ndugu yangu unaweza kuingia nakutoka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulibahatika Sana mkuu,
Bila shaka Atakua Ni Mnene.

Kuna mdau mmoja aliwai sema,
"Wanawake wanene wanaupendo Sana na watoto hata ambao hawajawazaa"
 
Najaribu kufikiria wewe ni mwanamke wa namna gani vile ulivyojaa hekima naamini kabisa familia yako ni moja ya familia Bora na zenye furaha.

Mleta mada pamoja na ushauri mzuri wenzetu wanaoutoa hapa lakini ushauri wako huu naomba auchukue Kama jibu rasmi la mada yake hii.
 
Olewa na single father ikiwa umeshuhudia kaburi la baby moma. Lasivyo jiandae tu kwa yajayo yasiyofurahisha.
 
Kwakweli ata mi nina mtoto wa nje na mke niliye nae sasa hajui siku nimwambie itakuwa kasheshe? Yani basi ujana maji ya mtoto,
 
Walaa huyo mke hakosei, kulea mtoto yeyote asie wako ni kipaji. Kama amejigundua hana hicho kipaji its better alivyokataa kuliko akubali kumpokea kishingo upqnde halafu aje asimangwe kwa kumnyanyasa mtoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…