Soon nakuwa mama wa kambo. Nahitaji maombi yenu na ushauri wa maisha haya mapya

Mleta mada, kwanza nikupongeze kwa kuaminiwa na mumeo kulea mtoto ambae sio wa kumzaa. Naweza kushauri mawili matatu kutokana na uzoefu - nami pia ninaishi na mtoto wa kambo na alimleta nyumbani mwaka mmoja baada ya kuwa tumefunga ndoa, akiwa na miaka 6.

1. Mchukulie sawa na watoto wako wengine, pasiwe na tofauti namna unavyoishi nao. Mfano, asome shule moja na wenzake au kama ni tofauti basi ziwe na hadhi inayofanana. Hata unapomtambulisha kwa ndugu/jamaa/marafiki/majirani mtambulishe kama ni mwanao. Epuka kabisa kumtambulisha kama "mtoto wa mume". Hii itasaidia kujenga bond kati yako na mtoto na pia kati yake na ndugu zake.

2. Anapokosea jambo usiwe mwepesi wa kumwadhibu, mshirikishe kwanza baba yake, usije ukaonekana kama unamwonea.

3. Mfundishe/mwelekeze utaratibu wa maisha yenu hapo nyumbani (do's and donts), kila inapobidi bila kuwa mkali. Mfano, wa kwangu alipokuja alikuwa na tabia za kupiga wenzake nikawa namwelekeza mara kwa mara kuwa humu ndani hairuhusiwi kupigana, akikuchokoza mwenzako shitaki kwa mama au baba. Au kabla ya kulala ni lazima kusali kwa pamoja n.k n.k

4. Uwe na mawasiliano na mama yake mzazi. Sababu as long as mtoto hayupo kwa mama, ni lazima atakuwa na uhitaji wa kujua maendeleo ya mtoto wake-kiafya, kimasomo n.k. Usimpe sababu baba mtu kuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na mama wa mtoto. Wewe ndio uwe kiunganishi.

5. Muhimu zaidi, omba sana Mungu mtoto huyo awe ni chambo ya maelewano mazuri kati yako na mumeo.

All the best!
 
Asante sana. Nimekuelewa na ushauri wako nimepokea na nitaufanyia kazi. Nahitaji nondo kama hizi. Barikiwa sana
 
Wengine tulifanyiwa vitimbi na mama zetu wa kambo vya kila aina lakn Leo hii ndio tunawalea na wanatutegemea kwa kila kitu

Hakuna anaye ijua kesho yake
Wengine hadi leo vinaendelea ila wakikwama hao wamekuja....
 
Mpende kama mwanao lakini usiwe na expectations zozote kwamba kuna kiasi cha upendo na wewe unahitaji kutoka kwake. Kama na yeye ataamua kukupenda kama mama yake au la hilo ni juu yake.
 
Sitarajii penye utu na upendo na kutamalaki kwa Mungu iwe katika nafsi, familia, ndoa na etc pawepo na uthubutu wa fikra kama hizi. Mfanye Mungu aishi ndani yako. Upupu haumjui mjomba wala etc...
 
Mpende kama mwanao lakini usiwe na expectations zozote kwamba kuna kiasi cha upendo na wewe unahitaji kutoka kwake. Kama na yeye ataamua kukupenda kama mama yake au la hilo ni juu yake.
Asante kwa ushauri
 
Kikubwa uishi na mtoto wa mwenzio kama wako
Yaani mtu ulipewa taarifa kabla hata hujaolewa afu et leo unakuwa na wasiwasi miaka yote hiyo kama siyo roho mbaya ni nini,kwani mtoto anapunguza nini kwenye familia?
 
Huo Ni mtego amekuletea

Na ni kipimo sahii kabisa cha Ubora wa uanamke Wako (wife material) ktk familia na Ndoa yako kiujumla.

Ukijichanganya hapo,
Iyo Ndoa inaota mbawa
Na uzuri alipewa taatifa kabla ya ndoa sa nashangaa anachoogopa ni nini?
 
Hongera kwa kukubali si jambo rahisi kulea mtoto mkubwa.

Nimeishi na watoto wa kuletwa ( si wa baba)
- wanahisi wewe si mhusika wa maisha yao. Wanachopewa mara nyingi huhisi wangestahili zaidi.

- Wewe si wa muhimu sana kwao. Kwenye kuwaadabisha wanachagua kukusikiliza au kutokusikiliza.

- Fadhila kwako hata baada ya kujitolea ni option, si wajibu.

-Do not force to be loved or respected.
- Mjalie huduma stahiki, usijikombe ukajuta baadaye.

- Jifunze tabia zake ujue namna ya kumuadabisha. Ukimuacha tu atakugharimu.

- Usiondoe family standard zako kumfanya yeye tu awe comfortable.

Mengine with time, mambo yanaenda.
 
Wale mnaosema ana roho mbaya kutwa kusema hamuwaoi single mother.
Nyie roho mbaya zenu hamzioni?
 
Of course ni changamoto na uzuri umefafanua vyema ila cha msingi ni kumlea kama wengine very simple
 
Wengine tulifanyiwa vitimbi na mama zetu wa kambo vya kila aina lakn Leo hii ndio tunawalea na wanatutegemea kwa kila kitu

Hakuna anaye ijua kesho yake
@wangshu jifunze kitu hapa.
Una watoto wako sawa lkn hujui kesho yao.
Kuna wakati watoto wa kambo nyota zao hung'aa sana ukimlea huenda akawa tegemeo lako baadae
 
Mwisho wa siku kulea mtoto asie wako ni shughuli, ni kazi huo ndio ukweli tena ukweli usiotakiwa make ukiusema lazima uambiwe una roho mbaya....

Unaambiwa mlee kama mwanao sawa, mwanao akikosea utamkanya, kama ni kuchapa utamchapa, huyo wa mme mguse uone!!! Unamchapa kwa sababu sio wako....okay ukiamua uache tu napo utaambiwa haumrekebishi kwakua sio wako.

Mke wa bro hampendi kabisa mtoto wa bro, nami namuelewa na nasisitiza bro asilazimishe mke amlee huyo mwanae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…