Aliegundua huu ugonjwa alituweza hata upone,usijiamini sana,,rejea yule mama wa kilimanjaroApumzike kwa amani. Nakumbuka mwaka jana alipost picha akiwa hospitali akasema amepata changamoto ya upumuaji lakini anaendelea vzr, akapona kabisa. Mwaka huu ameugua tena na kuondoka. Mwenyezi Mungu amrehemu.
Malukanga inasumbua ikipata colabo na covidNiliambiwa kuwa Captain John Nyerere alikuwa na "mdudu" lakini siku hizi mdudu hawasumbui kabisa vijana wa generation hii: una uhakika?
Mnyonge mwenyewe
Aliegundua huu ugonjwa alituweza hata upone,usijiamini sana,,rejea yule mama wa kilimanjaro
Sofia alikuwa kwenye oksijeni, RIP.
Tatizo nini sasa hapaambayo inapatikana Mzena wanakotibiwa VIP wa nchi hii
lakini ni kawaida ya hii familia, babu alikimbilia kutibiwa London, mtoto Rose alipelekwa Mzena na mjukuu nae Mzena
sisi tutafia Sinza Palestina na vituo vingine vya afya tunavyojengewa kwa tozo zetu
Tatizo nini sasa hapa
Khaaatatizo ni wao na watoto wao na wajukuu zao kujiwekea ventilators kwenye ma hospitali yao ya ma VIP kwa kutumia tozo za miamala yetu sisi
huku Nanyumbu dispensary hatuna oxygen ventilator
Nyerere alikaa madarakani miaka 29 yuko busy kujijengea sifa kwenye medani za kimataifa badala ya kujenga hospitali na kujenga uwezo wa wataalam…..
….siku yamemkuta yeye madhila ya afya eti katuacha kakimbilia London, Mungu akamwambia weee! usintanie!
anafanana na Makongoro Nyerere na pia sura ya mama Maria ipo RIP dada yetu wa taifaSophia Nyerere, ambaye ni Mjukuu wa Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere, amefariki dunia leo Jumanne katika Hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam, alipokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu. Marehemu Sophia ni Mtoto wa John Nyerere.
====
SOPHIA Nyerere, ambaye ni mjukuu wa Baba wa Taifa la Tanzania, Hayati Julius Nyerere, amefariki dunia leo Jumanne, tarehe 27 Julai 2021, mkoani Dar es Salaam.
Taarifa ya kifo hicho imetolewa leo na familia ya Nyerere, ambayo imesema Sophia amefariki dunia kwenye Hospitali ya Mzena, mkoani Dar es Salaam, alikokuwa anapatiwa matibabu.
Marehemu Sophia alikuwa Mtoto wa Hayati John Nyerere, aliyefariki dunia Mei 2015. John alikuwa mtoto wa nne wa Mwalimu Nyerere.
Taarifa ya familia hiyo imesema, kwa sasa msiba uko nyumbani kwa Mwalimu Nyerere, maeneo ya Mikocheni mkoani Dar es Salaam.