Salam ndugu zangu, poleni makada wa CCM mliokwisha timuliwa, mliotimuliwa na ambao mnaendelea kutimulia ndani ya CCM.
Naomba ninukuu haka ka-msemo ka Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Jakaya Mrisho Kikwete :-
"Siasa haina rafiki wala adui wa kudumu. Akili za kuambiwa changanya na za kwako".
Msukuma ambaye alimkana Lowasa live na baadae kuwa karibu na Magufuli, leo anaonekana mbaya. Sophia Simba kama mwenyeki wa UWT Taifa, ni cheo kikubwa sana, ana watu wengi potential nyuma wanaomkubali.Tusibeze!
Kuna maswali haya mawili ya kujiuliza kuhusu kumtimua/kumtumbua mtu:-
1. Je,yeye mwenyewe, familia yake, ndugu zake, marafiki zake wanajisikiaje? Wataendelea kukupenda?
2. Je, yeye na timu yake wataendelea kubaki na kuipenda CCM?
Jibu la hayo maswali ni HAPANA. Kama hapana nini kinafuata?
Hizo network automatically zinaendelea kujikusanya, kuwasiliana, kushaurina na kupanga mikakàti mingi mizito inakuwa against na wewe.Siyo malofa, kuna kulipizana visasi miaka nenda rudi.
Awamu ya 5 imetumbua watu wengi sana,ndani ya serikali na ndani ya CCM.Hao watu wote wanaungana,wanakuwa kitu kimoja,cha kimikakati.