Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Hizo zimebaki kuwa ndoto maana tulitegemea hayo 2015 baada ya kina kingunge kuhama kumbe hola..ccm itabaki milele
Ile ilikua the starting point tu. Yaani kama ni movie, ile ilikua Trela. Subiri kiini cha movie yenyewe October 2020
 
Ile ilikua the starting point tu. Yaani kama ni movie, ile ilikua Trela. Subiri kiini cha movie yenyewe October 2020
Maneno ya mfa Maji hayo..hao ndio watoa siri kwa lowasa wamepigwa chini..unadhani kuna mtu ataleta u spy tena huko?..wanajua upinzani hakuna future na ndio maana waliendelea kubaki ccm
 
Unashangaza kweli ivi katika hao wote umeona yupi ni mwanasiasa Bora?? Wote ni mizigo tu hakuna msaada pale yote ni mizigo tena ya Miba ukidhani kuijenga upinzan ulio Bora kwa waliofukuzwa mtaishia kuwa kujitekenya na kucheka wenyewe
 
Maneno ya mfa Maji hayo..hao ndio watoa siri kwa lowasa wamepigwa chini..unadhani kuna mtu ataleta u spy tena huko?..wanajua upinzani hakuna future na ndio maana waliendelea kubaki ccm
Aondoe wote walioimba ile siku kuwa wanaimani na Lowassa pamoja na PM
 
 
CCM wanatakiwa kwenda mbele zaidi. Bashe na Josef Msukuma hawa ni adui wa CCMt. Lazima wafukuzwe mara moja. Hata michango yao bungeni inathibitisha hilo. Let them be kicked out. Hawa ni virusi ndani ya CCM.We must be serious against such intra enemies of our parpty. Muda wa kuwafukuza ni huu. Tumewachoka.
 
Chama chochote chenye timua-timua kinachodhani kila mwenye mawazo mbadala ni msaliti KAMWE hakiwezi kudumu. Hapa ndio mwanzo wa mwisho wa ccm.
 
Salam ndugu zangu, poleni makada wa CCM mliokwisha timuliwa, mliotimuliwa na ambao mnaendelea kutimulia ndani ya CCM.

Naomba ninukuu haka ka-msemo ka Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Jakaya Mrisho Kikwete :-

"Siasa haina rafiki wala adui wa kudumu. Akili za kuambiwa changanya na za kwako".

Msukuma ambaye alimkana Lowasa live na baadae kuwa karibu na Magufuli, leo anaonekana mbaya. Sophia Simba kama mwenyeki wa UWT Taifa, ni cheo kikubwa sana, ana watu wengi potential nyuma wanaomkubali.Tusibeze!

Kuna maswali haya mawili ya kujiuliza kuhusu kumtimua/kumtumbua mtu:-

1. Je,yeye mwenyewe, familia yake, ndugu zake, marafiki zake wanajisikiaje? Wataendelea kukupenda?

2. Je, yeye na timu yake wataendelea kubaki na kuipenda CCM?

Jibu la hayo maswali ni HAPANA. Kama hapana nini kinafuata?

Hizo network automatically zinaendelea kujikusanya, kuwasiliana, kushaurina na kupanga mikakàti mingi mizito inakuwa against na wewe.Siyo malofa, kuna kulipizana visasi miaka nenda rudi.

Awamu ya 5 imetumbua watu wengi sana,ndani ya serikali na ndani ya CCM.Hao watu wote wanaungana,wanakuwa kitu kimoja,cha kimikakati.
 
Aondoe wote walioimba ile siku kuwa wanaimani na Lowassa pamoja na PM
Ishu sio wimbo..hata jk mbona aliimba nao..ishu ni actions zao baadhi baada ya kutoka pale na baada ya uchaguzi..ccm sio Saccos babu kama vyama vingine..
 
Acha kuleta porojo. Unamtisha nani? Wako huru kuichukia ccm. Ni haki yao. Lakini kuna faida kubwa kuwatimua kuliko wangebaki ccm. Adui uliye naye ndani ni adui mbaya sana kuliko aliyeko nje. Dawa ya msaliti ni kumuondoa. Let them go. Kutoka kwao ni faida kubwa sana kwa chama kuliko kubaki kwao ndani ya chama.
 
Ni uafrika tu, kudhihirisha msimamo wako sio dhambi hata kidogo. Mimi nimekukumbusha ya Trump ili ufute kauli yako kwamba walichofanya hao waliofukuzwa hakijawahi kufanyika popote duniani! Huo ni uuongo. Marekani kuna republicans walimpinga trump toka uchaguzi wa ndani na hata uchaguzi mkuu walimpinga waziwazi mpaka kwenye media. Je aliposhinda ulisikia kamfukuza mtu chama? Waafrika tunafundishwa siasa za kijinga sana yaani kama wanyama.
 
MKUU MENGI YATATOKEA Yaani wewe unikoseshe chakula mezani watoto wangu walale na njaa ila wa kwako wale bado utegemee nikuchekee!!!!!

LAZIMA NIKUFUMUE NGUMI YA TAYA TUONE KM UTAENDELEA NA HICHO KITABASAMU CHA NGURUWE DUME
 
Sisi tunaangalia tu game inavyoenda ila kama ishu ilikua ni kwenye uchaguzi uliopita sidhani kama kulikua na haja ya haya maana itakinyima chama afya.

Kama hawa Jamaa wanaondolewa kwa sababu ya kumuunga mkono Mh.Lowassa ambaye amewahi mpaka kuwa Waziri Mkuu ndani ya CCM sijui kuna nn .

Yeyote anaweza kuibuka mshindi ni jinsi gani amejipanga na kuwashawishi wanachama wenzake . Lengo Kubwa la vyama vya siasa na wanasiasa ni kushika dola na si vinginevyo .

Kingefanyika kitu kwa ajili ya kuweka fair play tu hapo ila kama ni kushikana mashati kuna sehemu tutapoteana kwa zama hizi za vyama vingi ni hatari.
 
Yani mtu awasaliti, wamteme baadhi ya vikao, wampe nafasi ya ubunge viti maalum

Kuna msemo niliona kwenye movie moja,

May be this world (especially Tz) is another planet's hell
 
Kwani si amewafukuza baada ya miaka karibu miwili toka wafanye makosa? Unajuaje ya mbele huko Marekani?
 
Yani nimwonavyo bwana yule jamani pekupeku msije (jpm) yeyote atakae fungua mdomo kuongea vibaya juu yake au chama chake bas police centr patakuw nyumban kwao na kusutu ndo kazin kwao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…