Kufukuza ni kitendo cha lazima katika maisha ili kuponya na kustawisha jumuiya.
Ukiukuza ndipo wengi wanajiunga kwa sababu kila mtu anatamani haki itendeke.
Makosa ya kimaadili na nidhamu yanapotokea au kutendwa, wanaoumizwa ni jumuiya sio aliyetenda na ndio maana ili kuponya nafsi zilizoumia ni muhimu hatua za kimaadili na nidhamu zifuatwe.
Na hili la kufukuza halikuanza ccm na halitaishia ccm: kwa sababu maadili na nidhamu ni kwa jumuiya zote za kibinadamu.
Vikundi vyote vina maadili yake.
Kwa mfano katika dini, shekh au mchungaji akitenda kosa la kimaadili uma utaumizwa na kuuponya lazima hatua zichukuliwe kwa mtu huyo. Kwa hiyo tunajua hatua kama hazichukuliwi wanajumuiya watasambaa na hawatakuwa na imani tena na jumuiya yao.
Ila hatua zikichukuliwa, wanajumuiya wanafurahia umoja wao na kuwavutia wengine.
Mapadri wanafukuzwa, Mashekh kadhalika.
Wanafunzi wanafukuzwa na walimu kadhalika
Wakuu wa mikoa wanafukuzwa na wa wilaya kadhalika
Mawaziri wanafukuzwa na hata marais wapo
Baba nyumbani anafukuza mtoto na ukoo unawatenga ndugu.
Kubwa zaidi hata habari za mbinguni muziki ni huohuo.
Malaika walifukuzwa tunasoma leo hii ni mashetani na tunao hapa tuniani.
Mungu akamuumba Adam na baadaye amkamfukuza kwenye bustani ya edeni!! Pamoja na kufukuzwa bado kila mtu anapigana kwenda mbinguni.
Kwahiyo kwa kitendo cha kamati ya maadili kuwaonya na kuwafukuza waliokutwa na makosa ya kimaadili na nidhamu ni kuponya nafsi zilizoumia kutokana na makosa hayo lakini pia kufanya watu wengine wengi kuvutiwa sana na ccm.
Niwakaribishe mjiunge ccm na kufurahia umoja wetu.