Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Mabadiliko ndani ya CCM ni lazima yatokee khasa baada ya miaka 40 tangu kuundwa kwake.

Nafasi katika halmashauri kuu zimepunguzwa kutoka 388 hadi 158, wakati nafasi katika kamati kuu zimepunguzwa kutoka 34 hadi 24.

Mabadiliko kama haya au kwa kiingereza "reforms " ni muhimu, khasa ukiwa na kiongozi anaejali kupunguza matumizi na kuleta nidhamu na uwajibikaji hata katika chama chake.

Pia mabadiliko kama haya kutakiwezesha chama cha CCM kutekeleza shughuli zake kwa ufanisi zaidi na kuondokana na wanachama wasohitajika lakini wanaolipwa fedha za mishahara bure.

Ila kumvua uanachama Sophia Simba ni uamuzi sahihi na balozi Nchimbi kukaa nje akiwa balozi ni adhabu tosha.

Kwa umri alokuwa nao mama Sophia Simba alipaswa kuchunga kauli zake na ile kauli yake aloitoa kwenye harakati za kuchuja wagombea uraisi mwaka 2015 ya kwamba, yeye ni mjumbe wa kamati kuu na hatakubali kuona mgombea mwenye sifa kama Edward Lowasa akikatwa jina kwasababu za kijinga na kwamba wote wanaomchafua Edward Lowasa ni wajinga na wapumbavu.

Hii ni sawa na mtu kutapika kabisa halafu baadae anakuja kula matapishi yake mwenyewe.
Richard Ndio umerudi bongo mazima? Nilidhan bado hupo skendinevia
 
Waende chadema maana chadema ni kama yule myama sijui anaitwaje yeye anakula marudio ya simba
 
Uyoo madabida. Alivyo. Kuwa. Akiipenda. Ccm. Imenibidi. Ni. Cheke. Ngoja. Niendelee. Kutazana. Chakorii
 
Ha ha ha! Sikujua kama ccm imekuwa mdebwedo namna hii! Yaani jamaa katoka bara hata kiswahili chenyewe bado hakija kaa sawa, kwenye chama hata balozi wa mtaa hajawahi lakini Leo anakuja na vitisho na amri wote wanaufyata! Kweli ccm mdebwedo!

Kama wanamwogopa sio wamshawishi Lema au Lissu ajiunge na ccm na wampe ukatibu mkuu kama hajaachia ngazi mwenyewe!
Hiyo lema na lissu kwa mbowe hwana cha kuhoji ije kwa magu
 
MAY THE PARTY THAT BEARS THE GREEN COLOUR FLY HIGH. LET IT TO WHERE THE SKY. MAY IT BE SEEN ON ALL REGIONS. MAY WE END THE DARK DARK DAYS. TOGETHER. WE CAN.
 
Huwezi kuniambia myu aliyepinga maamuzi ya chama mbele ya vyombo vya habari kama Sofia Simba ni msaliti nikakuamini! Tayari najua sisi nchi hizi kupingana na viongozi ni dhambi kubwa.
Una uhakika gani kile ndo kilichofanya afukuzwe?..na kwanini muda wote hadi leo waje wafanye hivo!...naweza amini wamewachunguza hadi kuja fanya hayo maamuzi wana ushahidi wa usaliti wao ni kwanini Nchimbi kapewa onyo na Sophia afukuzwe
 
Eti tunaimani na .......Kuleni jeuri yenu sasa. Tunahitaji mwanaccm kwa imani yake na si kwa kuvutwa na mtu au madaraka fulani.
Waende wakajifunze kwa mwanaccm kindakindaki Dr john Samwel Malechela. Huyu gwiji kwenye kichwa chake hakuna msamiati wa kurudisha kadi ya ccm.
 
Sio CHADEMA wala Sio CCM, tena afadhali huku CCM kwa sasa wanafagia fagia hakuna anaeona vizuri hasa watu wa chini wapo tu tunakoenda ndio huko huko, utamshangaa mtu wa CHADEMA pove linamtoka utadhani kwake hakuna udikteta, tena huyo Tundu Lizu nani wa kupinga wazo lake, semeni ukweli? Na Mbowe nani wa kumkosoa kwa sasa? Si umeona waliojaribu yaliyowakuta, na najua hamna uchaguzi wa Mwenyekiti tena dah...

Siasa za Tanzania ni bora wale wasio na vyama lakini hawa mashabiki uchwara ambao hata katiba za vyama vyao hawazijui ni shida... wako kusubiri nani wa kumtukana na kuongea USHILAWADU badala ya kujadili hoja za msingi kwa maendeleo ya taifa hili..

CCM acha ifagie, wakimaliza tunasubiri kama CHADEMA na nyinyi mtafagia au hayo makombo waliotupa chini CCM ndio mtaokota kama kawaida yenu?

Maana hamtaki kujibidiisha na nyinyi mkae mezani mle chakula fresh sijaona hata program za kuelemisha vijana wenu kuhusu maono ya CHADEMA kila siku viongozi wenu kwenye makorido kulinda nafasi zao kwa kutafuta kashfa ya mahakamani au ya kuuchafua utawala, huku mkipata washabiki badala ya wanachama watakao kijenga chama.
Wewe unasema cha nini sisi tunasema tutakipataje? Wait and see
 
CHADEMA tunawakarbisha kwa Mikono Miwili,hao ni Mtaji Mkubwa sana kwa chama chetu
 
Msidhani waliofukuzwa ni kwasababu ya kuonesha mapenzi yao kwa lowasa waziwazi kipindi cha kampeni la hasha! Baada ya Kampeni mienendo yao ilikuwaje? Vitu gani walikuwa wakivifanya chinichini ili kuhujumu chama? Vikao vya siri na mipango ya siri je? Hatuna shida na waliokuwa wakimsupport lowasa kama mgombea na baada ya hapo wakarudia misingi na itikadi za chama. Tunatatizo na wasaliti, mnajua maana ya usaliti? Btw kama CCM Inakufa nafikiri mnatakiwa mshangilie badala ya kulalamika. Eti CCM inaendeshwa kidikteta, udikteta wa wa huko kwenu msinidanganye hamuuoni!
 
Back
Top Bottom