Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Sophia Simba, Madabida wavuliwa uanachama CCM. Emmanuel Nchimbi apewa onyo kali

Husika na Kichwa cha uzi hapo juu, unafikiri wasaliti hawa waliofungashiwa virago CCM mwisho wao / wataangukia chama gani cha siasa hasa ukizingatia kwasasa tuna vyama vingi vya siasa vyenye ushawishi mkubwa. Karibu utiririke, kejeli hazitakiwi.

Kumbuka siasa haina rafiki wala adui wa kudumu.
Wataenda CHADEMA kumwaongezea nguvu kina Lowasa ya kuififisha CHADEMA ili CCM 2020 ipite kwa kishindo, kwa akili ya haraka utaona wametimuliwa lakini kuna baadhi yao wametumwa kwenda kuvuruga upinzani, CHADEMA tuamke tunaletewa maluki bao la mkono linaandaliwa sasa hivi Hawa ccm sio watu wazuri kabisa
 
mmmmmhh hali mbaya kwa kila mtu aisee... Hata JK huko aliko atakuwa analalama tu maana deals zake nyingi zimepigwa kapuni.

Mambo mtaani hayaendi tunaambiwa hatufanyi kazi ndio maana ngawira mfukoni hazikai, ila Daaaah after 10 years jamaa atatuacha na miundombinu mizuri kabisa kila wilaya ya nchi hii itakuwa imeunganishwa kwa rami na mambo mengine makubwa yaweza kufanyika ila sasa mpaka tufike huko hakuna rangi tutaacha kuona..

Hahahahahahahaha, leo nimecheka kama kichaaaa.
Bruv rangi tutaziona kibao tu, na huu ni mwanzo kabisa.
 
kiukweli chadema wakishindwa kuchukua nchi 2020 basi hawatoweza tena.

hakuna kipindi kitakuwa kirahisi kama hiki.

magufuli kwa staili ya uongozi wake hata msipopiga kampeni, Whitehouse mnayo.

let us wait,
CCM wataiba kura, kumbuka mkuu wa uchakachuaji January makamba yupo ccm bado, wangemfukuza huyo ndipo Wapinzani wangepata ahueni.
 
....maajabu gani haya!.. Anawafukuza waliokipigania chama na kuwakumbatia wenye vyeti feki....double standards na unafiki wa ajabu huu....
 
Unauliza jibu. Kwani hukuliona lile gari aina ya Ford Ranger lililoenda kuwachukua kutoka mkutanoni lilikuwa limeandikwaje ubavuni? Bahati mbaya likapata mkong'oto.
 
We muongo kabisaaaa!!! Kuwa hawakumuunga mkono ili apitishwe ni uongo mikubwa!! Kwanza mheshimiwa hakuwa na makundi ndani ya chama!! Unamsingizia kabisaaaa!!! Wengi wao ni team lowasaa na walimpa muda mgumu wakati wa kampeni mchana CCM usiku chadema!!
kwaiyo waliokuwa wanaimba nyimbo wanaimani na lowasa walikuwa akina nani?
 
Ikiwa chama kimeamua kukufukuza na unataka kuendelea kuwa ndani ya chama huku ukishikilia nafasi yako\zako, mfate msajiri wa vyama ili akurudishe kwenye chama na undelee kushika nafasi zako kama alivofanya kwa Lipumba.

Sofia Simba usipaniki, fata huo utaratibu, ni rahisi sana.
 
Inavyoonekana yale matokeo ya kamati kuu yalichakachuliwa hakushinda, sasa anajua next time matokeo yatakuwa yaleyale.
 
Sawa we mwaga povu kumsifia na kumfagilia nkurunzinza utafikir upo UK ngoja hili jini mnalofuga liishiwe damu halafu iwe zamu yako kunyonywa ndo utaelewa maana wengine mnasubili popobawa ale msambwanda ndo utaelewa alichosema lissu kuwa white house imevamiwa na muumiani! Yaan wewe ndo boga kabisa unaona kabisa chama kinaliwa msembwende na popobawa we bado huamini sasa zamu yako haina muda mrefu
Hujielewi wewe!

Kwa sasa viroba vimekatazwa wewe umevipata wapi?
 
Wakuu ni wazi kwamba hiki chama sasa kinakufa , tena kinakufa kirahisi kuliko tulivyotarajia , cha kufurahisha ni kwamba wanaoiua hawajui hata ilikotokea .

Taarifa zinadokeza kwamba Mwenyekiti wake anayesimamia " Mauaji " hayo , hakuwahi hata kuwa mjumbe wa shina , msaidizi wake aitwaye Humphrey Pole Pole haifahamiki hata alikotokea , bali kumbukumbu zinaonyesha ni mpinzani wa serikali mbili .
 
Back
Top Bottom