Mabadiliko ndani ya CCM ni lazima yatokee khasa baada ya miaka 40 tangu kuundwa kwake.
Nafasi katika halmashauri kuu zimepunguzwa kutoka 388 hadi 158, wakati nafasi katika kamati kuu zimepunguzwa kutoka 34 hadi 24.
Mabadiliko kama haya au kwa kiingereza "reforms " ni muhimu, khasa ukiwa na kiongozi anaejali kupunguza matumizi na kuleta nidhamu na uwajibikaji hata katika chama chake.
Pia mabadiliko kama haya kutakiwezesha chama cha CCM kutekeleza shughuli zake kwa ufanisi zaidi na kuondokana na wanachama wasohitajika lakini wanaolipwa fedha za mishahara bure.
Ila kumvua uanachama Sophia Simba ni uamuzi sahihi na balozi Nchimbi kukaa nje akiwa balozi ni adhabu tosha.
Kwa umri alokuwa nao mama Sophia Simba alipaswa kuchunga kauli zake na ile kauli yake aloitoa kwenye harakati za kuchuja wagombea uraisi mwaka 2015 ya kwamba, yeye ni mjumbe wa kamati kuu na hatakubali kuona mgombea mwenye sifa kama Edward Lowasa akikatwa jina kwasababu za kijinga na kwamba wote wanaomchafua Edward Lowasa ni wajinga na wapumbavu.
Hii ni sawa na mtu kutapika kabisa halafu baadae anakuja kula matapishi yake mwenyewe.