Hiki chama kinakoelekea ukibishana na mwenyekiti unanyongwa
CCM kitaendelea kuwa Chama cha Siasa za kimaendeleo
Vyama vingine vinaendesha siasa za maigizo ya:
1) kususia vikao vya bunge,
2) kuziba midomo,
3) kutoa matamko ya operesheni zisizo na matokeo chanya,
4) kuandamana,
5) kuwapigia deki barabara viongozi wao,
6) kuzungusha mikono ya mabadiliko,
7) kutwa kutoa matusi, kejeli, umbea, unafiki, na uchochezi,
8) kutumia ruzuku kuendesha kesi mahakamani, ambazo wanazitengeza wenyewe,
9) kutumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, kupumua 'frustrations' zao,
10) kuendekeza hoja za watu (km vyeti) na matukio (km fulani kaongea nini leo), badala ya kero za jamii (matumizi ya viroba, madawa ya kulevya, maji, afya, umeme, nk) na masuala ya kimaendeleo.
Kujitambua njia sahihi ni kujitathmini na kuchukua hatua za mabadiliko. CCM kwa hilo inapaswa kupongezwa.
Viongozi wa vyama vya upinzani, kama ni wanasiasa kweli, siyo siasa za umaarufu na kuchumia tumbi, kitendo cha CCM kufanyia marekebisho ya Katiba yake, wanapaswa kujifunza na kuchukua hatua sahihi. Ila wafuasi wao, hasa wa mitandao ya kijamii, ikiwemo JF, watakebehi mabadiliko hayo.
Vyama vya siasa visipojitambua, hakika kutawala nchi hii itakuwa ndoto. Lakini kwa jinsi viobgozi hao walivyo na uchu wa umaarufu, hakuna kitakachofanyika!!!!