Tunashuhudia uthubutu wa hali ya juu unaofanywa na CCM, hii kwa mtazamo yakinifu unaweza kusema ndio kujivua gamba, kama nyoka afanyavyo ili kuonekana mpya na safi.
Kwa yanayoendelea kutokea hakika discipline itakuwa ya hali ya juu, watu wataheshimu katiba na miiko ya chama chao.
Ni kweli haiingii akilini mtu kusaliti chama chake kisibebe dola halafu abaki kuwa muaninifu bila kujutia na kuomba msamaha halafu kujirekebisha.
Nina imani yule aliyesamehewa aliomba msamaha na kuonyesha mwenendo mwema km alivyosema Katibu Mwenezi wa chama hicho. Hii inatafsiri kwamba waliobaki wote walionekana kuendeleza vigisu za chinichini, ambayo ni hatari sana.
Hongera ccm, mnaonekana kuwa bora kila wakati na kwa mwelekeo huu wa kuweza kujitathmini ktk kipindi fulan na kutoa maamuzi mazito, basi mnaweza kuwa chama bora wakati wote kama sio kwa Afrika mzima.
You are a Giant CCM! [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122]