MBOKA NA NGAI
JF-Expert Member
- Jan 31, 2025
- 350
- 576
Wakati nchi wanachama wa SADC na EAC wakikubaliana kuhakikisha amani inapatikana mashariki mwa Congo, taarifa za chini chini zinaeleza kuwa wanajeshi kati ya 700 na 800 tayari walishawasiri nchini Congo kuongezea nguvu jeshi la serikali hiyo. Chanzo cha habari, Reuters, kimesema kwamba, ndege ya mizigo aina ya IL-76, ilitoka kwenye kambi ya jeshi la anga Pretoria kuelekea Lubumbashi, na kufanya safari tano kati ya tarehe 30 Januari na tarehe 7 Februari, 2025.
Mbunge Chris Hattingh wa Afrika kusini, alisema wanajeshi waliopelekwa, ni kati ya 700 na 800.
Kuna wanajeshi wa Afrika kusini waliopo chini ya ulinzi wa M23 huko Goma.
Waziri wa mambo ya nje wa Afrika kusini, alipinga mawazo ya bunge, kurudisha wanajeshi hao, na kusema kuna umuhimu wa kuongeza nguvu, na watarudi tu amani itakapopatikana nchini humo.
Pia soma: Rais wa Malawi amuagiza kamanda wa jeshi la nchi hiyo kujiandaa kuondoa wanajeshi wake mashariki mwa DRC
Wakati huo, katika ziara ya raisi wa DRC, Felix Tshisekedi nchini Tchad, aliomba msaada wa kijeshi, na serikali hiyo imetangaza kwamba, kwa muda wa wiki mbili kuanzia sasa, wanajeshi kutoka Chad, watawasiri nchini DRC kwa msaada wa kijeshi.
Inaelekea, vita vinaenda kuanza upya