SPECIAL FEEDBACK: JF members niliowasajilia Business Names na Company Limited 2013-2014

SPECIAL FEEDBACK: JF members niliowasajilia Business Names na Company Limited 2013-2014

nahitaji kubadili jina la Kampuni ,naomba unifahamishe utaratibu ukoje hapo brela
 
nahitaji kubadili jina la Kampuni ,naomba unifahamishe utaratibu ukoje hapo brela
inawezekana,iwe ni jina la biashara ama company limited, kwa upande wa company limited utatakiwa kwanza uandike barua ya kuomba jina (company search name) kisha utaandika barua ya kuomba kubadili jina ambayo huambatanishwa na special resolution pamoja na ile barua ya kupitishwa jina ,special resolution huandaliwa na wanasheria na kusainiwa na secretary and chairperson wa company utalipia bank sh 15000/ baada ya kuandikiwa risiti brela, na kwa upande wa business name ni sh 5000/ pia kuna form unajaza ya kubadili jina
 
nimetoa updates page 1 kazi ya company limited nilisajilia mwanzoni wa mwezi huu wa nne ,karibuni
 
licence za biashara mbalimbali vp au una~conection gani?endapo nahitaji leseni quickly!
 
Mkuu mimi nipo mkoani na nataka kufungua duka la dawa.ila ndo sina tin number wala chochote.je utanisaidiaje?
 
Mkuu mimi nipo mkoani na nataka kufungua duka la dawa.ila ndo sina tin number wala chochote.je utanisaidiaje?

vibali vinavyohusiana na madawa sina utaalam navyo, japo waweza kusajili jina la biashara la hilo duka lako la madawa, pia ukiasajili kama company limited biashara yako unataka iwe pana zaidi na ikihusisha usambazaji wa vifaa vya pharmacy na uuzaji wa jumla na rejareja wa madawa,baada ya hapo sasa,TIN na aina nyingine ya vibali vitafuata, pia waweza nipigia kwa no yangu rejea post ya kwanza
 
Bado nafanya shughuli za usajili wa business name n Limited Company,wengi nimewasajilia ,hao niliowataja ni baadhi yao, pia napenda kuwashukuru kipekee wale jf members niliowasajilia na baadaye wakaniunganisha na watu wengine ambao awali hawakunifahamu
 
Jamani napenda kutoa mrejesho wa kijana huyu Singo..niliiona hii thread nikamtafuta na akanisaidia.

Kanisajiria limited company bila shida yoyote.so wengine wenye uhitaji mnaweza mtumia pia.

Thanks.

Spray
 
Last edited by a moderator:
Mwaka unaisha ,ilikuwa faraja kwangu kufanya kazi nanyi,kifupi nimefanya kazi nyingi kwa upande wa limited na businessname zilizotokana na uzi huu, nilizo orodhesha ni baadhi tu kwa ajili ya rejea, Mungu akijaalia mwaka ujao nitaendelea .

Asanteni.
 
Jukwaa la Wajasiriamali linataka watu waaminifu wa aina hii, maana huyu jamaa anapotray real life, na si virtual world kama wengine wengi tunavyofanya.

Mahusiano ya nyuma ya screens yanatakiwa hatimaye yawe productive kama hivi alivyofanya mwanajamvi.
Kwa wenye shaka bado, huyo member Chasha ni jamaa yetu tuko nae Arusha na mjasiriamali aliyepiga hatua.
Binafsi nakupongeza sana mkuu Singo kwa kufaidisha wanajamii kwa kwenda hatua ya ziada nje ya computers.



Nimeipenda sana post hii PakaJimmy......... Singo hakika nitakutafuta Best!
 
Last edited by a moderator:
Sasa fixer mtu unakaa mbeya utaenda kukomaa na elfu 18 huku unatumia malaki ya pesa kwa nauli na matumizi mengine? binafsi Naona jamaa anasaidia sana. Wakati mwingine waweza Kuwait Dsm ila ukakosa mda kabisa. Huo ni mtazamo wangu tuu. Nipo taya kukosolewa ikibidi.
 
Sasa fixer mtu unakaa mbeya utaenda kukomaa na elfu 18 huku unatumia malaki ya pesa kwa nauli na matumizi mengine? binafsi Naona jamaa anasaidia sana. Wakati mwingine waweza Kuwait Dsm ila ukakosa mda kabisa. Huo ni mtazamo wangu tuu. Nipo taya kukosolewa ikibidi.
Asante kwa kuliona hilo,halafu kibaya zaidi alidanganya kwa sababu hakuna company ya aina yoyote brela (iwe by shares or guarantee )ambayo gharama yake ya usajili ni 18,000.
Halafu pili hakuelewa nilikuwa namjibu member aliye uliza kusajili jina la biashara ambaye alitaka kufahamu ghrama zangu mimi kwa jumla ambapo gharama zake brela ni sh 6000,na hiyo nikamjibu jumla akinipa arobaini ambayo nimejumlisha na gharama zangu ikawa arobaini.
Ila watu kama yeye(The Fixer )ni kuwasamehe .
 
Gharama za usajili wa Company Limited by Shares

capital 200,000---------not more than 500,000 = Tsh 111,200(registration,filling fee +stamp duty)

'' 500,000---------not more than 1,000,000 = '' 141,200 ''

'' 1000,000------- '' 2000,000 = '' 161,200 ''

'' 2,000,000------ '' 3000,000 = '' 181,200 ''

'' 3000,000------- '' 5000,000 = '' 211,200 ''

'' 5000,000------- '' 10,000,000 = '' 241,200 ''

'' 10,000,000----- '' 30,000,000 = '' 262,200 ''

above 30,000,000 na kuendelea = '' 361,200 ''

NB; Gharama hizi ni kwa mujibu wa Brela, pia ikiwa umewasilisha vitabu vitatu(Memorandum and Articles of Association),ukiwasilisha vitabu zaidi ya viatatu, bei yake itaongezeka sh 5000,kwa kila kitabu ,hizi ni gharama za stamduty

Malipo yangu

nitakuchaji 180,000 ,mpaka unapata Certificate of Incorporation. Kazi niatazokufanyia itajumuisha kuandika barua ya Company Name Search(kwa kawaida majibu hutoka baada ya siku tatu) ,kuandaa vitabu vitatu(Memorandum) ambavyo vinagongwa na wanesheria sehemu 6 ambazo Directors mmesaini kugawana share za company, maelekezo ya ujazaji wa form itayoambatana na vitabu na gharama za ufuatiliaji mpaka document ina kamilika ambayo kwa uzoefu wangu ndani ya week mbili usajili unakuwa umekamilika
.

kama vitabu mtataka viwe vingi gharama zangu zitaongezeka kidogo,sababu gharama za printing na binding zitaongezeka,pia gharama nitazowalipa wanasheria zitaongezeka
Mkuu Singo kuna updates zozote tena kuhusiana na hili jambo?
Gharama za Brela
Gharama zako?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Singo kuna updates zozote tena kuhusiana na hili jambo?
Gharama za Brela
Gharama zako?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mabadiliko brela yapo kama ifuatavyo

Mtaji 5 million 247,200

Mtaji zaidi ya million tano hadi 20 ni 332,200

Mtaji zaidi ya miillion 20 hadi 50 ni 362,200

Mtaji zaidi ya mil 50 na kuendelea bei yake ni 512200

Zangu pia zimebadilika ,kama uko Dar nicheck ofisini posta mtaa wa Jamhuri karibu na hotel ya Golden Tulip.
Au nipigie 0712742233
 
NIkinagalia Jedwali la Brela naona Gharama ni Almost the same.Labda kwenye cost zake kunaweza kuwa na mabadiliko.Binafsi nimefurahi kukutana na uzi huu wa wakongwe ambao wamefanya kazi kwa muda mrefu
Kuna mabidiliko kidogo brela nimeanisha hapa baada ya kuulizwa.
 
Back
Top Bottom