SPECIAL THREAD-Baraza la Famasi Tanzania: Maoni, Mirejesho, Ushauri au Malalamiko yanayohusu huduma zetu

Joined
Mar 27, 2025
Posts
33
Reaction score
45
Habari wana JamiiForums, Baraza la Famasi limeanzisha ukurasa huu kwa lengo la kutoa taarifa mbalimbali, kuelimisha umma pamoja na kupokea maoni, mirejesho au malalamiko yanayohusu huduma zetu.

Utangulizi:
Baraza la Famasi ni taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Afya iliyoundwa kwa Kifungu Na. 3 cha Sheria ya Famasi (Sura 311) na kupewa jukumu la kusimamia taaluma ya famasi na utendaji wa wanataaluma nchini.

Dira
Kuwa mdhibiti wa utendaji wa taaluma ya famasi anayetambulika kimataifa

Dhima
Kusimamia na kudhibiti kwa ufanisi taaluma ya famasi na utendaji wake

MAADILI YA MSINGI
A: Uadilifu

Kuzingatia misingi ya utawala bora, uwazi, uwajibikaji na kufuata maadili katika utekelezaji wa majukumu
B: Weledi
Kufanya kazi kwa ujuzi wa hali ya juu kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za maadili na mwenendo wa kitaaluma
C: Ufanisi
Utendaji unaoleta matokeo makubwa kwa gharama nafuu
D: Kipaumbele kwa Wateja
Katika juhudi zake zote, Baraza litazingatia kulinda na kuendeleza afya ya umma
E: Ubunifu
Kuimarisha ubunifu katika utoaji wa huduma

Majukumu ya Baraza
Majukumu ya Baraza la Famasi ni pamoja na;
  1. Kusajili, kuorodhesha na kuandikisha wanataaluma (wafamasia, fundi dawa sanifu, fundi dawa wasaidizi) na kuidhinisha watoa dawa na wawakilishi wa makampuni ya dawa;
  2. Kusajili majengo ya kutunzia na kutoa huduma za dawa (famasi, maghala na maduka ya dawa muhimu);
  3. Kusimamia maadili ya taaluma ya famasi;
  4. Kuweka na kutunza taarifa za wanataaluma wote waliosajiliwa;
  5. Kutoa mitihani ya taaluma kwa wahitimu wa kada ya famasi kwa ajili ya usajili;
  6. Kuratibu mafunzo kwa vitendo (internship) kwa wahitimu wa shahada ya famasi kabla ya kusajiliwa pamoja na kutambua vituo vinavyotoa mafunzo hayo;
  7. Kuratibu na kutoa mafunzo ya kujiendeleza kitaaluma (Continuing Professional Development) kwa lengo la kuboresha huduma zinazotolewa;
  8. Kuandaa Kanuni na Miongozo katika kusimamia taaluma ya famasi;
  9. Kujibu na kushughulikia masuala yote yanayohusu taaluma ya famasi;
  10. Kushirikiana na mamlaka za ithibati (TCU & NACTVET) katika kusimamia na kuhakiki viwango na ubora wa mafunzo ya kozi ya famasi yanayotolewa na vyuo mbalimbali nchini.
  11. Kuidhinisha vyuo na mitaala ya mafunzo ya kozi za famasi
  12. Kufanya ukaguzi wa vyuo vinavyotoa mafunzo ya taaluma ya famasi ili kuhakiki uzingatiaji wa viwango;
  13. Kufanya ukaguzi wa maeneo yanayotoa huduma za dawa;
  14. Kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuendeleza taaluma ya famasi;
  15. Kuhamasisha matumizi sahihi ya dawa;
  16. Kufuatilia na kushughulikia malalamiko ya wadau yanayohusiana na huduma za kitaaluma, na;
  17. Kumshauri Waziri mwenye dhamana ya Afya katika masuala yote yanayohusu taaluma ya famasi.
Mawasiliano
Msajili Baraza la Famasi,
Barabara ya Jakaya Kikwete,
S.L.P 1277,
Dodoma.

Tovuti: www.pc.go.tz
Barua pepe: [email protected]
Simu: 0736222515
Simu bila Malipo: 0800110015
Maoni/Malalamiko: 0736222513
 
Baraza la Famasi ni taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Afya iliyoundwa kwa Kifungu Na. 3 cha Sheria ya Famasi [Sura 311] na kupewa jukumu la kusimamia taaluma ya famasi na utendaji wa wanataaluma nchini.

Mmefanya vyema kuja kwenye Mtandao huu.
Lakini lazima muhakikishe kwamba hamuutelekezi huu Ukurasa wenu ili muweze kuja hapa Mara kwa Mara na kujibu hoja mbalimbali za Wachangiaji.
 
Kwa nini wahudumu wa maduka ya dawa muhimu wanauza antibiotics bila indications?
Nimewahi ona mtu ana dalili za common cold akaenda duka la dawa kuulizia Amoxicillin na akauziwa!!!
 
Karibuni sana sana sana...
14. Kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuendeleza taaluma ya famasi;

Wazo langu hizi dawa za kuongeza nguvu za kiume ambazo zinakua kwenye vichupa vidogo (mkongo) kwanini visiwe officials tukaanza kupatiwa kwa maduka ya dawa kwa mfumo wa vidonge......
 
Screenshot_20250414-141120.png
 
Kwa nini vigezo vya kusoma FAMAS ni D 2?? Tofauti na coz nyingine??
 
Tanzania kuna pharmacy nyingi kuliko wafamasia na sheria inasema kila FAMAS lazima isimamiwe na mfamasia mmoja je hizo nyingine nani anasimamia??

Ina maana kuna watu wanasimamia FAMAS zaidi ya moja??
 
Mna mpango gani wa kujenga ofisin zenu wenyewe??
Muache kupanga??
 
Kwa nini msipunguze ada ya kulipia leseni maana ni kubwa sanaa
 
Habari wana JamiiForums, Baraza la Famasi limeanzisha ukurasa huu kwa lengo la kutoa taarifa mbalimbali, kuelimisha umma pamoja na kupokea maoni, mirejesho au malalamiko yanayohusu huduma zetu.

Utangulizi:
Baraza la Famasi ni taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Afya iliyoundwa kwa Kifungu Na. 3 cha Sheria ya Famasi (Sura 311) na kupewa jukumu la kusimamia taaluma ya famasi na utendaji wa wanataaluma nchini.

Dira
Kuwa mdhibiti wa utendaji wa taaluma ya famasi anayetambulika kimataifa

Dhima
Kusimamia na kudhibiti kwa ufanisi taaluma ya famasi na utendaji wake

MAADILI YA MSINGI
A: Uadilifu

Kuzingatia misingi ya utawala bora, uwazi, uwajibikaji na kufuata maadili katika utekelezaji wa majukumu
B: Weledi
Kufanya kazi kwa ujuzi wa hali ya juu kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za maadili na mwenendo wa kitaaluma
C: Ufanisi
Utendaji unaoleta matokeo makubwa kwa gharama nafuu
D: Kipaumbele kwa Wateja
Katika juhudi zake zote, Baraza litazingatia kulinda na kuendeleza afya ya umma
E: Ubunifu
Kuimarisha ubunifu katika utoaji wa huduma

Majukumu ya Baraza
Majukumu ya Baraza la Famasi ni pamoja na;
  1. Kusajili, kuorodhesha na kuandikisha wanataaluma (wafamasia, fundi dawa sanifu, fundi dawa wasaidizi) na kuidhinisha watoa dawa na wawakilishi wa makampuni ya dawa;
  2. Kusajili majengo ya kutunzia na kutoa huduma za dawa (famasi, maghala na maduka ya dawa muhimu);
  3. Kusimamia maadili ya taaluma ya famasi;
  4. Kuweka na kutunza taarifa za wanataaluma wote waliosajiliwa;
  5. Kutoa mitihani ya taaluma kwa wahitimu wa kada ya famasi kwa ajili ya usajili;
  6. Kuratibu mafunzo kwa vitendo (internship) kwa wahitimu wa shahada ya famasi kabla ya kusajiliwa pamoja na kutambua vituo vinavyotoa mafunzo hayo;
  7. Kuratibu na kutoa mafunzo ya kujiendeleza kitaaluma (Continuing Professional Development) kwa lengo la kuboresha huduma zinazotolewa;
  8. Kuandaa Kanuni na Miongozo katika kusimamia taaluma ya famasi;
  9. Kujibu na kushughulikia masuala yote yanayohusu taaluma ya famasi;
  10. Kushirikiana na mamlaka za ithibati (TCU & NACTVET) katika kusimamia na kuhakiki viwango na ubora wa mafunzo ya kozi ya famasi yanayotolewa na vyuo mbalimbali nchini.
  11. Kuidhinisha vyuo na mitaala ya mafunzo ya kozi za famasi
  12. Kufanya ukaguzi wa vyuo vinavyotoa mafunzo ya taaluma ya famasi ili kuhakiki uzingatiaji wa viwango;
  13. Kufanya ukaguzi wa maeneo yanayotoa huduma za dawa;
  14. Kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuendeleza taaluma ya famasi;
  15. Kuhamasisha matumizi sahihi ya dawa;
  16. Kufuatilia na kushughulikia malalamiko ya wadau yanayohusiana na huduma za kitaaluma, na;
  17. Kumshauri Waziri mwenye dhamana ya Afya katika masuala yote yanayohusu taaluma ya famasi.
Mawasiliano
Msajili Baraza la Famasi,
Barabara ya Jakaya Kikwete,
S.L.P 1277,
Dodoma.

Tovuti: www.pc.go.tz
Barua pepe: [email protected]
Simu: 0736222515
Simu bila Malipo: 0800110015
Maoni/Malalamiko: 0736222513
Mmefanya jambo jema sana kujiunga na mtandano huu wa JF.
Hakika nyie mmefanya uthubutu, Kongole kwenu.

Nina swali moja tu kwenu kama mlivyojieleza kwenye majukumu yenu ya Famasia, namba 15 hapo.

Tatizo la kuwashwa ukeni limekuwa tatizo sugu sana na lisilosikia dawa.
Wengi hulalamika kutopona ugonjwa huo hata wakitumia dawa mara 2 na zaidi. Hapo No.15 mmesema mnahamasisha matumizi sahihi ya dawa. Haya, tunaomba mtuelekeze dawa ipi bora na sahihi kimatibabu, maana tunadhalilika huku mitaani.

Tunajikuna sana na hatuponi hata, uke zetu zinaharibika sana, hatuna hamu na tendo la ndoa tena. Tendo la ndoa kwetu limekuwa kama adhabu wakati kiuhalisia ni jambo la starehe.

Tunaomba muingilie kati kunusuru hii hali.

Asanteni.
 
Mmefanya jambo jema sana kujiunga na mtandano huu wa JF.
Hakika nyie mmefanya uthubutu, Kongole kwenu.

Nina swali moja tu kwenu kama mlivyojieleza kwenye majukumu yenu ya Famasia, namba 15 hapo.

Tatizo la kuwashwa ukeni limekuwa tatizo sugu sana na lisilosikia dawa.
Wengi hulalamika kutopona ugonjwa huo hata wakitumia dawa mara 2 na zaidi.
Hapo No.15 mmesema mnahamasisha matumizi sahihi ya dawa.
Haya, tunaomba mtuelekeze dawa ipi bora na sahihi kimatibabu, maana tunadhalilika huku mitaani.

Tunajikuna sana na hatuponi hata, uke zetu zinaharibika sana, hatuna hamu na tendo la ndoa tena.
Tendo la ndoa kwetu limekuwa kama adhabu wakati kiuhalisia ni jambo la starehe.

Tunaomba muingilie kati kunusuru hii hali.

Asanteni.
Umetisha mkuu hadi mimi mwenyewe nimetishika
 
Back
Top Bottom