SPECIAL THREAD-Baraza la Famasi Tanzania: Maoni, Mirejesho, Ushauri au Malalamiko yanayohusu huduma zetu

SPECIAL THREAD-Baraza la Famasi Tanzania: Maoni, Mirejesho, Ushauri au Malalamiko yanayohusu huduma zetu

Meza unayotingisha ina vinywaji vya gharama sana mkuu 😂😂😂😂😂
Mimi ni mende tu mkuu, hata nikipita kwenye meza ya vinywaji Sidhani Kama nitaidondosha, labda waamue tu kunikanyaga na viatu kichwani 😅😅.
 
Habari wana JamiiForums, Baraza la Famasi limeanzisha ukurasa huu kwa lengo la kutoa taarifa mbalimbali, kuelimisha umma pamoja na kupokea maoni, mirejesho au malalamiko yanayohusu huduma zetu.

Utangulizi:
Baraza la Famasi ni taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Afya iliyoundwa kwa Kifungu Na. 3 cha Sheria ya Famasi (Sura 311) na kupewa jukumu la kusimamia taaluma ya famasi na utendaji wa wanataaluma nchini.

Dira
Kuwa mdhibiti wa utendaji wa taaluma ya famasi anayetambulika kimataifa

Dhima
Kusimamia na kudhibiti kwa ufanisi taaluma ya famasi na utendaji wake

MAADILI YA MSINGI
A: Uadilifu

Kuzingatia misingi ya utawala bora, uwazi, uwajibikaji na kufuata maadili katika utekelezaji wa majukumu
B: Weledi
Kufanya kazi kwa ujuzi wa hali ya juu kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za maadili na mwenendo wa kitaaluma
C: Ufanisi
Utendaji unaoleta matokeo makubwa kwa gharama nafuu
D: Kipaumbele kwa Wateja
Katika juhudi zake zote, Baraza litazingatia kulinda na kuendeleza afya ya umma
E: Ubunifu
Kuimarisha ubunifu katika utoaji wa huduma

Majukumu ya Baraza
Majukumu ya Baraza la Famasi ni pamoja na;
  1. Kusajili, kuorodhesha na kuandikisha wanataaluma (wafamasia, fundi dawa sanifu, fundi dawa wasaidizi) na kuidhinisha watoa dawa na wawakilishi wa makampuni ya dawa;
  2. Kusajili majengo ya kutunzia na kutoa huduma za dawa (famasi, maghala na maduka ya dawa muhimu);
  3. Kusimamia maadili ya taaluma ya famasi;
  4. Kuweka na kutunza taarifa za wanataaluma wote waliosajiliwa;
  5. Kutoa mitihani ya taaluma kwa wahitimu wa kada ya famasi kwa ajili ya usajili;
  6. Kuratibu mafunzo kwa vitendo (internship) kwa wahitimu wa shahada ya famasi kabla ya kusajiliwa pamoja na kutambua vituo vinavyotoa mafunzo hayo;
  7. Kuratibu na kutoa mafunzo ya kujiendeleza kitaaluma (Continuing Professional Development) kwa lengo la kuboresha huduma zinazotolewa;
  8. Kuandaa Kanuni na Miongozo katika kusimamia taaluma ya famasi;
  9. Kujibu na kushughulikia masuala yote yanayohusu taaluma ya famasi;
  10. Kushirikiana na mamlaka za ithibati (TCU & NACTVET) katika kusimamia na kuhakiki viwango na ubora wa mafunzo ya kozi ya famasi yanayotolewa na vyuo mbalimbali nchini.
  11. Kuidhinisha vyuo na mitaala ya mafunzo ya kozi za famasi
  12. Kufanya ukaguzi wa vyuo vinavyotoa mafunzo ya taaluma ya famasi ili kuhakiki uzingatiaji wa viwango;
  13. Kufanya ukaguzi wa maeneo yanayotoa huduma za dawa;
  14. Kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuendeleza taaluma ya famasi;
  15. Kuhamasisha matumizi sahihi ya dawa;
  16. Kufuatilia na kushughulikia malalamiko ya wadau yanayohusiana na huduma za kitaaluma, na;
  17. Kumshauri Waziri mwenye dhamana ya Afya katika masuala yote yanayohusu taaluma ya famasi.
Mawasiliano
Msajili Baraza la Famasi,
Barabara ya Jakaya Kikwete,
S.L.P 1277,
Dodoma.


Tovuti: www.pc.go.tz
Barua pepe: [email protected]
Simu: 0736222515
Simu bila Malipo: 0800110015
Maoni/Malalamiko: 0736222513
Mmekuwa vyema kuwa na Baraza na account yake hapa.

Hii ni Tabia njema ya Uwazi ma Uadilifu pia.
 
Mmefanya jambo jema sana kujiunga na mtandano huu wa JF.
Hakika nyie mmefanya uthubutu, Kongole kwenu.

Nina swali moja tu kwenu kama mlivyojieleza kwenye majukumu yenu ya Famasia, namba 15 hapo.

Tatizo la kuwashwa ukeni limekuwa tatizo sugu sana na lisilosikia dawa.
Wengi hulalamika kutopona ugonjwa huo hata wakitumia dawa mara 2 na zaidi.
Hapo No.15 mmesema mnahamasisha matumizi sahihi ya dawa.
Haya, tunaomba mtuelekeze dawa ipi bora na sahihi kimatibabu, maana tunadhalilika huku mitaani.

Tunajikuna sana na hatuponi hata, uke zetu zinaharibika sana, hatuna hamu na tendo la ndoa tena.
Tendo la ndoa kwetu limekuwa kama adhabu wakati kiuhalisia ni jambo la starehe.

Tunaomba muingilie kati kunusuru hii hali.

Asanteni.
madam B heshima yako dada,, naomba ujisemee wew ndo hauna ham ya tendo,, mimi ni mwanamke ila hamu bado ninayo 🤗🤗
 
Tanzania kuna pharmacy nyingi kuliko wafamasia na sheria inasema kila FAMAS lazima isimamiwe na mfamasia mmoja je hizo nyingine nani anasimamia??

Ina maana kuna watu wanasimamia FAMAS zaidi ya moja??

Hii taarifa haina ukweli
 
madam B heshima yako dada,, naomba ujisemee wew ndo hauna ham ya tendo,, mimi ni mwanamke ila hamu bado ninayo 🤗🤗
Marahabaaaa!!
Hamu ya tendo mbele ya kujikuna, we acha kabisa mdogo wangu, basi una hisia kali sana, mie nimeshindwa. Yaani utadhani kisu kimepita huku ukeni.

Huu ugonjwa unatesa sana. Na mbaya zaidi mashuhuda kibao wanasema huwa hawaponi, ila dawa zinapooza tu ugonjwa.

Watupe majibu.
 
Mna mpango gani wa kujenga ofisin zenu wenyewe??
Muache kupanga??
Habari! Ujenzi wa ofisi mpya za Baraza Jijini Dodoma unaendelea na unakaribishwa kuweza kutembelea na kujionea maendeleo yake.

Ahsante
TM
Jengo la Baraza la Famasi.jpg
 
Kwa nini dawa kama dawa3, mifupain zinauzwa madukani na watu wasio na ujuz wa dawa?
Tunajitahidi kufanya kaguzi za mara kwa mara ili kubaini watoa huduma ambao hawana sifa. Tafadhali tupatie taarifa kupitia namba zetu hapo juu endapo utakutana na changamoto kama hizi kwenye duka lolote
 
Mmefanya jambo jema sana kujiunga na mtandano huu wa JF.
Hakika nyie mmefanya uthubutu, Kongole kwenu.

Nina swali moja tu kwenu kama mlivyojieleza kwenye majukumu yenu ya Famasia, namba 15 hapo.

Tatizo la kuwashwa ukeni limekuwa tatizo sugu sana na lisilosikia dawa.
Wengi hulalamika kutopona ugonjwa huo hata wakitumia dawa mara 2 na zaidi. Hapo No.15 mmesema mnahamasisha matumizi sahihi ya dawa. Haya, tunaomba mtuelekeze dawa ipi bora na sahihi kimatibabu, maana tunadhalilika huku mitaani.

Tunajikuna sana na hatuponi hata, uke zetu zinaharibika sana, hatuna hamu na tendo la ndoa tena. Tendo la ndoa kwetu limekuwa kama adhabu wakati kiuhalisia ni jambo la starehe.

Tunaomba muingilie kati kunusuru hii hali.

Asanteni.
Pole sana na changamoto hii. Ni vema ukaenda kwenye kituo cha afya kilicho karibu na wewe kwa uchunguzi zaidi. Matumizi ya dawa bila ushauri wa kitaalam unaweza kusababisha kutokupata matokeo sahihi ya tiba.
 
Tanzania kuna pharmacy nyingi kuliko wafamasia na sheria inasema kila FAMAS lazima isimamiwe na mfamasia mmoja je hizo nyingine nani anasimamia??

Ina maana kuna watu wanasimamia FAMAS zaidi ya moja??
Mpaka kufikia leo tarehe 15 Aprili, 2025, takwimu zinaonyesha idadi ya Wafamasia ni 3939 na famasi ziko 3297. Taratibu za usimamizi ni mfamasia mmoja atasimamia famasi moja na idadi inaruhusu.
 
Kuna changamoto kubwa kwenye kutoa certificate za premise permits kwa majengo mapya baada ya kuwa mmeidhinisha. Mathalani, mimi ni mwaka na miezi 3 sasa sijapata, na mkija kwenye ukaguzi mnaidai ilihali ninyi ndiyo mlipaswa kunipa mimi. Tafadhari rekebisheni hili suala. Hai make sense ninyi ndiyo regulators mnaopaswa kunipa hicho cheti then ninyi hao hao mnakuja kunihoji kwanini sina. Na niliwahi kuja pale Mabibo mkanipiga kiswahili eti next time wakija kugagua waambie hawajakupatia.
 
Naomba mshirikiane na TBS na TMDA kufuatilia uuzwaji holela wa madawa nchini, hasa yanayohusu uzazi na nguvu za kiume. Ukipita Instagram siku hizi kila mtu ni mfamasia/daktari, na wanatangaza bila kufuata misingi ya utangazaji wa bidhaa za afya. Kwa sheria zenu wenyewe, mtu haruhusiwi kujiita mfamasia unless awe amesajiliwa na baraza, na anayefanya kinyume sheria anapaswa kuwajibishwa. Sijawahi kusikia mnafuatilia, au hata kuchukua hatua.
 
Back
Top Bottom