Verse 1
Ukweli sina chuki nawe, kusema nikukinai,
Huu wimbo mahususi kwako, mi siruki hako, kamtego kako baby.
Achana na mamluki nawe,waletao uzushi wale,
Maneno mkuki, usije ukanishuti, uniache mahututi darling.
Kumbikumbi wanaopaa, levo moja tunafatana,
Mchina na mjapan, wakituona tunafanana,
Inawezekana ndo sababu wanaona wivu sana,
Wanasema tutaachana tu(Oh no!)
Waambie hawatutishi, kuachana sio rahisi,
Mtoto we ni pisi, na bado uko peace,
You give me that peace of mind
Bridge
Nakumbuka ile kipindi, naanza kukujua
Enzi zile sina kiki, bado tupo chuo
Sina boom nina dhiki, hukujifaragua
Hukunipiga bluetiki, hukuwahi nizingua
Na wivu haujifichi, kuna lecture alijua
Akaweka vizingiti, usimalize chuo
Lakini bado haukuchiti,
Ndomaana nashangaa unaponiuliza
Do you love me? Coz
Hook
How can I not*4
Verse 2
Sasaivi tunakiwasha kama pilipili
Kila pozi kwenye picha tuna kili kili
Unanipenda na unaonyesha sio siri siri
Nishacheza ngoma yako ya makirikiri
Penzi bila kipimo (Baby kama lipi hilo?)
Kama wafilipino
(basi Usifanye igizo, penzi lisiwe na likizo,
Mi nakupa kipimo,Twende home utie wino.
.
Bridge
Coz nakumbuka ile kipindi, naanza kukujua,
Enzi zile sina kiki, bado tupo chuo,
Sijasuka bila wigi, Ulinisifia,
Ukanipa ile gifti, nlipougua)
Saivi Michongo imetiki,Jipange kutanua
Nitakupa kila kitu ushindwe kuchagua
(Na mimi staki kitu,Nimeshaamua
Ni wewe nachagua, Kwakuwa
Hook
How can I not*4