1. Kwa nini tunaishiishi tu, ili ufanikiwe ni lazima ukubali kuachana na mazoea uliyonayo sasa, Pigania kuwa Jua ukishindwa unakuwa nyota – Ruge
2. Hatukuumbwa ili tuwe maskini, tumepewa talanta na uwezo wa kufikiri, Kama wewe ni msomi usiwe na tabia ya kuwaza vitu vidogo vidogo, fikiria kufanya mambo makubwa ili ufike mbali – Ruge
3. Usibweteke, Dunia inakwenda kasi sana nawe pambana uende nayo sambamba. Kwa chochote ufanyacho ni muhimu sana uache alama yako- Ruge
4. Kama kuna jambo unalifanya na halina changamoto yoyote basi tambua kuna sehemu unakosea - Ruge
5. Hakuna ushahidi kuwa watu wanaweza kuwa matajiri kwa kuwezeshwa kwa vikundi vya pamoja, bali ni muhimu upokee wazo la mtu moja mmoja ukimuwezesha ni rahisi sana kuja kutoboa - Ruge
6. Kwenye siasa hakuna adui wa kudumu – Mbowe
7. Akili za kuambiwa, changanya na zako – Kikwete
8. Kauli yangu ya bao la mkono, inaniumiza sana na itaendelea kunitesa hadi Mungu atakaponitwaa - Nape