Special thread: Interesting (best) Quotes | Misemo yenye hekima ndani yake, Nukuu
"Siasa ni utaalamu unaoweza kuwaaminisha watu kuwa jehanamu ni peponi".....Adolf Hitler
"Siasa ni ufundi wa kueleza mipango ya baadae halafu hapo hapo kuelezea baadae kwanini imeshindikana.....unknown
"Kwenye siasa ujinga sio ukilema...Napoleon
"Vitani mtu anakufa mara moja lakini Kwenye siasa mara nyingi....Wiston Churchill
"Kuliko kumpa mwasiasa ufunguo wa maisha yako ni aheri ubadili kitasa"...Mark Twain
"Sanduku la kura lina nguvu kuliko risasi"....Abraham Lincoln
"Siasa ni vita bila kumwaga damu wakati vita ni siasa ya kumwaga damu....Mao Zedong

HEBU TIRIRIKENI NA NYIE


Sent using Jamii Forums mobile app
 
*QUOTE OF THE YEAR BY PROF. MOHAMMED JANNABI, DAKTARI BINGWA WA MOYO TANZANIA:*



*"Mambo makubwa yanayosababisha mishipa ya moyo kuziba ni pamoja na ulaji wanga, mafuta na sukari. Watu wengi wanadhani mafuta tu ndio yananenepesha. La hasha, wanga ndio mbaya zaidi. Wengi wananenepeana kutokana na wanga. Ndio maana utafiti uliofanywa unaonesha watu wanaonenepeana wako zaidi nchi za Kiarabu. Mwezi wa Ramadhani waislamu wenzangu wengi huongezeka sana uzito. Hii ni kwasababu ya kula vyakula na mahanjumati yenye wanga mwingi. Pia, vyakula hivyo huliwa muda mbaya (ftari saa 12 na daku kuanzia saa 6 usiku) ambapo mwili unakuwa hauna activities na hivyo metabolism huwa ni kwa kiasi cha chini sana. Kwa siku, Sisi tunakula wanga mwingi asubuhi lakini hatuna activities tunapanda magari na kushinda ofisini tumekaa siku nzima!!!. Lazma tutanenepeana tu, hamna namna. Hii ni tofauti na wenzetu wa vijijini. Wao wanaruhusiwa kula vyakula vya aina zote kwani wana activities nyingi. Hivyo, nashauri mle vyakula stahiki, mfanye mazoezi na mywe maji kiasi. Maji mengi sana hayafai kabisa kwani yanayayusha madini mwilini ambayo ni muhimu. Kunywa lita moja na nusu tu. Mimi sijala mkate, chapati, vitumbua, maandazi nk kwa miaka 10 na sijanywa juisi na soda kwa miaka 3. Pendelea kula matunda badala ya juisi na pia kula sana mboga mbalimbali za majani. Nakusihi sana usisikilize tumbo, mdomo wala macho kwani vitakupotosha, badala yake sikiliza ubongo wako ukikwambia _"Prof. Jannabi aliniambia nile nini?"_. "DIET" ni sawa na SALA. Maana yake ni kuwa unajiandalia huko mbeleni. Uchaguzi ni wako".*
Prof. M. JANNABI, Clouds FM, 25 April 2019.
 
Mitukunyama inakuja,we isubiri tu.labda ita gain something here. 🏃🏃🏃🏃
 
Back
Top Bottom