Kiongozi ni mtu aliyejitoa muhanga kwa ajili ya kulisaidia taifa lake, kwa MWL hakuogopa kuzuiliwa misaada, kuwekewa vikwazo alipambana na wakoloni kweli kweli. Tuungane na viongozi wenye nia ya dhati ya kulifikisha taifa letu kwenye nchi ya ahadi.
Tukiingia moja kwa moja katika mada iliyopo mezani siku ya leo ni msemo/quote ipi ya mwalimu Nyerere ambayo unaikubali na kukufikirisha ambayo aliwahi kuitoa enzi za uhai wake? Share nasi hapa chini.
“Inawezekana tatizo la paka kwa panya lingekwisha kama paka angefungiwa kengele shingoni: taabu ni kumpata panya wa kuifanya kazi hiyo. Na panya watakuwa wajinga sana wakidhani kuwa paka watajifunga au watafungana kengele shingoni" -
Mwl. J. K. Nyerere
View attachment 1457973