Special thread: Interesting (best) Quotes | Misemo yenye hekima ndani yake, Nukuu
Mwalim Nyerere: Kuendelea kusikiliza upumbavu hali ya kuwa unatambua ni upumbavu basi wewe unakuwa zaidi ya upumbavu
 
8defee9c185cabfbc94a504158cf5f64.jpg
 
Worth to share

1. "Ni afadhali kuwa na jeshi la kondoo linaloongozwa na Simba, kuliko jeshi la simba linaloongozwa na kondoo." *Napoleon_Bonaparte.*

2. "Lengo la kwanza la vita sio kufa kwa ajili ya nchi yako, hapana. Bali ni kuua mtu mwingine kwa ajili ya nchi yake." *George_Patton.*

3. "Lazima nisome siasa na vita ili mwanangu apate uhuru wa kusoma hesabu na falsafa." *John_Adams.*

4. "Washindi wanashinda kwanza halafu wanakwenda vitani, wanaoshindwa huenda vitani kwanza halafu ndio wanatafuta ushindi." *Sun_Tzu.*

5. "Inafahamika vizuri katika vita, majeruhi wa kwanza ni ukweli. Kwamba, wakati wa vita, ukweli huharibiwa vibaya na propaganda." *Harry_Browne.*

6. "Propaganda ikitumiwa vizuri inaweza kumfanya mtu aone kuwa paradiso ndio jehanam na jehanam ndio paradiso." *Adolf_Hitler.*

7. "Mtu mwenye ufahamu wa kweli, si tu kwamba atawapenda maadui zake wanapofanya vizuri, bali pia atawachukia marafiki zake wanapokosea." *Friedrich_Nietzsche*

8. "Madaraka ni kama mchanga. Jinsi unavyoyakumbatia kiganjani ndivyo yanavyokuponyoka." *Confucus*

9. "Tofauti kati ya akili na ujinga ni kuwa, akili ina kikomo, ujinga hauna kikomo." *Albert_Einstein.*

10. "Kuna watu wawili tu wasioweza kubadili mawazo. Mpumbavu kuliko wote na mwenye hekima kuliko wote." *Plato.*

11. "Rais ni mtu wa kushutumiwa kila mara. Ukiona hataki kushutumiwa, ujue hajui sababu ya kuwa hapo." *Harry_Truman*

12. "Sote tumezaliwa wajinga, tunahitaji bidii kidogo ili kuwa na maarifa, au bidii kubwa sana ili kuendelea kubaki wapumbavu. Baadhi huchagua njia ya pili." *Benjamin_Franklin*

13. "Unajisi wa sheria hutokea pale ambapo mahakmu/majaji, hujiweka mikononi mwa watawala na kuamini watawala wana nguvu kuliko sheria" *Lamar_Smith*

14. "Kuliko kuwapa wanasiasa ufunguo wa maisha yako, ni bora ubadili kitasa" *Doug_Larson*

15. "Siasa ni hatari kuliko vita. Kwenye vita mtu hufa mara moja tu, lakini kwenye siasa mtu hufa na kufufuka mara nyingi kadri iwezekanavyo" *WinstonChurchil*

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wana JF,

Mimi ni mmoja kati ya ambao napata hamasa kubwa na motisha kupitia nukuu (quotes) za watu mbali mbali wa maana hasa wale wa kale kama wachumi, wanasiasa, wajasiriamali, wanaharakati na hata watu wa dini tofauti tofauti.

Hivyo nimeona sio mbaya tukashirikishana hivi vimisemo vya watu wa maana narudia watu wa maana.Tujifunze tutiane moyo tuoneshane njia.

NB: Lugha yoyote sawa ila tusipoelewa tutafsiriane.

Unaweza kutupa na nukuu (quote) yako wewe mwenyewe.

-"If you don't risk anything, you risk even more." — Erica Jong

-"Wealth is not simply about having [HASHTAG]#money[/HASHTAG]; it is about having the freedom to choose how to live your life." - R. Kiyosaki

-"The idea that success can happen overnight is crippling the financial future of generations. You have to work for it." - R. Kiyosaki
 
Habari wana BUU,
Mimi ni mmoja kati ya ambao napata hamasa kubwa na motisha kupitia "quotes" za watu mbali mbali wa maana hasa wale wa kale......kama wachumi, wanasiasa, wajasiriamali, wanaharakati na hata watu wa dini tofauti tofauti,

Hivyo nimeona sio mbaya tukashirikishana hivi vimisemo vya watu wa maana....narudia watu wa maana.
Tujifunze....tutiane moyo....tuoneshane njia.

NB: lugha yoyote sawa ila tusipoelewa tutafsiriane ili mtu atoke na kitu, mfn hata mm nimeshindwa kujua kiswahili cha neno "Quote"

-"If you don't risk anything, you risk even more." — Erica Jong

-"Wealth is not simply about having [HASHTAG]#money[/HASHTAG]; it is about having the freedom to choose how to live your life." - R. Kiyosaki

-"The idea that success can happen overnight is crippling the financial future of generations. You have to work for it." - R. Kiyosaki
Kiswahili cha neno Quote ni NUKUU (kama sijakosea)
 
Back
Top Bottom