Special thread: Kwa waliosoma shule moja na viongozi mbali mbali tukutane hapa kujua vituko vyao shuleni

Special thread: Kwa waliosoma shule moja na viongozi mbali mbali tukutane hapa kujua vituko vyao shuleni

Is true kwa upande wangu sikusoma naye Hussein mwinyi ila nimebahatika mwaka 1982 kuwa nalinda kwao baada ya kutoka JKT , kwasababu mwanzo kabisa nilipangwa kigoma, baada ya kumaliza PUGU,lakin matokeo yakaja ya kidato cha sita nikawa nime pass kwa kiwango cha juu mno, watu 72 tu ndo tulichaguliwa kwenda chuo kikuu, nikapangwa dar es salaam nikisubiri muda wa kujoin chuo lakin nikawa bado kambini, mwanzo nilipelekwa wazo kulinda mashine ya maji, baadae nikahamishiwa kwa mzee MWINYI akiwa waziri, nikawa nalinda pale getini wanakuja nawafungulia ,

Nadhani kama mdogo wangu Hussein Mwinyi atapita hapa atakumbuka nimemsaidia sana hesabu akiwa anarudi toka shule by that time alikuwa form three nakumbuka, namsaidia hesabu,

Ila nikachaguliwa kusoma chemical and process engineering UDSM, tumeachana hivyo lakin mzee MWINYI akaja kunikuta sehem Fulani akauliza kwanini hatukuendelea kuwasiliana,
Shikamoo Mkubwa
 
Nilisoma na Mkurugenzi wa TANESCO katika shule sekondari Azania. Jamaa alikuwa mpole, kichwa kizuri kwa masomo, mchagamfu na mwenye kutoa msaada muda wowote kwa mhitaji. Hand writing yake ilikuwa nzuri sana. Ni kati ya majiniasi tuliokuwa nao wakati ule.
 
MWIGULU NCHEMBA alikuwa anaweza sana darasani, na aliwaogopa sana aanawake, nakumbuka alipenda sana economics, mwalimu kabla hajamaliza kufundisha anauliza nchemba unasemaje , anasimama na kitabu chake anaanza kudondosha nondo, kwa kifupi jamaa ni bright sana,
Siku moja kwenye paper wengine tumetumia booklet Moja ye anaandika uku amenyoosha mkono wa kushoto anaomba ya tatu inamaana ya pili pia Imejaa,
Ahahahaha watu ka ao ni sheedah loh umenikumbush mbal
 
Deo Filikunjombe(RIP) John Nchimbi,Kichele(tra) wapo kama walivyo sasa ila more advanced.
Pia nimesoma na majambazi napaswa kuwataja maana nao ni viongozi katika himaya zao?japo wengi marehemu sasa na marehemu hatajwi kwa mabaya
Mkuu, ulikuwa Forest Hill Moro? Nilisoma F5 & 6 na Filikunjonbe, akiitwa Deo Haule. Alijiunga nasi akitikea Seminari, jamaa alikuwa mpole sana. Head prefect wetu alikuwa John Nchimbi, jamaa alikuwa mwembamba mno, kweli duniani hakuna mtu mwembamba ila shida tu.

Vv
 
Rtd General Davis Mwamunyange......Mawenzi Secondary School:1967 to 1970.
Alikuwa mpole na kichwa yake imejaa vitu....ni namba moja tu miaka yote hiyo,hajawahi kuwa wa pili.
Hekima na busara tokea shule alikuwa nazo.
Duh hata mama yangu hajazaliwa!! Shikamoo bibi...
 
Uzi huu umeanzishwa kwa lengo zuri tu la kushare tabia ama sifa za viongozi wetu kwa wale waliobahatika kusoma nao ila kuna baadhi ya wadau wanauharibu kwa kukebehi na kuandika uongo
Ni aina ya ujinga uliojitokeza hivi karibuni mkuu uvumilie tu mi nimechagua kuwasoma walioandika kwa umakini wengine unaruka tu maana bashite sijui John na mengine wala sikuona kama ni sehem ya uzi anyway nimemaliza juzi sana so wengi niliosoma nao bado tuko tunapambana sku moja tutasimulia
 
Me mimesoma na John,nakumbuka alikua mchoyo sana darasani

Siku moja bhana ilikua mtihani wa mid term nimekaa nyuma yake nikaomba anisaidie swali la 3(nafikiri atakumbuka hili tukio)akasema hajajaza kumbe kamaliza maswali yote,sasa cha ajabu siku majibu yanarudi ana 0% kumbe alikariri paper lililopita akidhani yatakuja vile vile
.
.
Ni mchoyo tangu shule hataki mwingine afanikiwe ilihal mwenyewe anaharibu
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Dah! nimekumbuka mbali sana,miaka ya 1980 nilikuwa nchini korea nikichukua masomo fulani na huyu Rais wa sasa mnaemwita KIDUKU jamaa alikuwa mkorofi balaa alikuwa anatembea na bastola! jamaa alikuwa hana demu kabisa...Yeye ukikaa nae story zake ni vita tu.
Hapa umetudanganya jamaa kazaliwa 1984. sasa kutoka 1980 alienda shule na miaka 4 na bastola alitembea nayo vipi
 
Nilisoma na JPM jamaa alikuwa anakula sana maharage

Mwalimu wa hesabu akipita kukagua homework jamaa anajibana kwa mfumo wa kifutu anatoa kitu hicho mwalimu anarudi mwenyewe hapiti tena upande huo

Sijui kwa sasa Juma Maharage yuko wapi
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Me nimesoma na mzee wa Msoga primary 1968. Jamaa alikuwa ana akili za kuzaliwa, walimu wakikosa jibu wanamfata awafanyie calculation. Jamaa nilichoamini kuwa genius ni alipotufundisha almentary canary Yaani darasa zima hatujawahi kulisikia hili neno ila alitupigia pindi tukaelewa na nalikumbuka hadi Leo. Jamaa alikuwa bitozi sana kwa siku anaoga hata Mara nane akiguswa tu mbio kuoga.

Yeye stori zake nyingi ni bata bata tu, Yeye ndo mwanafunzi WA kwanza kula pizza shuleni. alisema akiwa Rais kila mtu atakuwa mpiga dili tu pesa nje nje
Chai yako sukari imekolea sana hasa huko mwishoni
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mkuu, ulikuwa Forest Hill Moro? Nilisoma F5 & 6 na Filikunjonbe, akiitwa Deo Haule. Alijiunga nasi akitikea Seminari, jamaa alikuwa mpole sana. Head prefect wetu alikuwa John Nchimbi, jamaa alikuwa mwembamba mno, kweli duniani hakuna mtu mwembamba ila shida tu.

Vv
Ilikuwa mwaka gani kaka?
 
Back
Top Bottom