Special thread: Kwa waliosoma shule moja na viongozi mbali mbali tukutane hapa kujua vituko vyao shuleni

Special thread: Kwa waliosoma shule moja na viongozi mbali mbali tukutane hapa kujua vituko vyao shuleni

Kuna kiongozi mmoja sitamtaja alikuwa anaoga amejificha kisa Ana ****** , sasa tukamvizia kwamba kwanini yeye huwa anajificha wakati wa kuoga?

Au anasubiri tumemaliza ndo anakuja kuoga,

Ndo tukagundua hayo,

Lakin bahati nzuri ilikuwa mtu social sana na anajiweza darasani na alikuwa anapendwa sana na walimu,

Salamu zuwafikie mtama,
Taja jina shule basi br
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Dah! nimekumbuka mbali sana,miaka ya 1980 nilikuwa nchini korea nikichukua masomo fulani na huyu Rais wa sasa mnaemwita KIDUKU jamaa alikuwa mkorofi balaa alikuwa anatembea na bastola! jamaa alikuwa hana demu kabisa...Yeye ukikaa nae story zake ni vita tu.
Hiyo 1980 sio ndio alikua kwenye hatua za kuzaliwa huyo kiduku
 
Dah! nimekumbuka mbali sana,miaka ya 1980 nilikuwa nchini korea nikichukua masomo fulani na huyu Rais wa sasa mnaemwita KIDUKU jamaa alikuwa mkorofi balaa alikuwa anatembea na bastola! jamaa alikuwa hana demu kabisa...Yeye ukikaa nae story zake ni vita tu.
Brother umesoma Korea??? Mbona kiduku kasoma Switzerland?? hujanishawishi bado
 
Me mimesoma na John,nakumbuka alikua mchoyo sana darasani

Siku moja bhana ilikua mtihani wa mid term nimekaa nyuma yake nikaomba anisaidie swali la 3(nafikiri atakumbuka hili tukio)akasema hajajaza kumbe kamaliza maswali yote,sasa cha ajabu siku majibu yanarudi ana 0% kumbe alikariri paper lililopita akidhani yatakuja vile vile
.
.
Ni mchoyo tangu shule hataki mwingine afanikiwe ilihal mwenyewe anaharibu
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Habari za wana jf naona ni vema

Tukiwa wanafunzi tuliamini kwamba labda kijana Fulani kutokana na usmartness wake atakuwa kiongozi Fulani wizarani, au anaweza kuwa kiongozi mkubwa baadae,

Kwa upande wangu nimebatika kusoma shule moja na ridhiwani kikwete

Huyu sifa zake ni kwamba
1. Alikuwa anajituma sana na ni mtu anaye weza sana masomo darasani,

2. Alikuwa Ana hekima ya kulelewa, haikuwa rahis kugundua kama ni mtoto wa waziri kipindi kile, na aliweza sana kuficha identify hiyo,

3. Sikuwahi kuona anapewa adhabu au kuadhibiwa kwa makosa ya siyo kuwa ya msingi. Kama anapata adhabu basi hiyo ilikuwa ya kulikumba darasa zima,

4. Kuna mwalimu mmoja alikuwa anatwambia kwamba siku akikuta waliofanya makosa na ridhiwani yumo basi alikuwa na kigugumizi hata kutoa adhabu, na kama anasamehe kundi basi ni kwa sababu kuna kijana mwenye adabu,

Nakumbuka siku moja tulikuwa na utani sana darasani tukafoji muhuri Fulani ili tuwatanie vijana tarehe moja April siku ya wajinga, tukaandika kuwa wamelipa Ada yote hawadaiwi, sasa kwa ujinga hatukujua kama ni kosa ,

Mimi nikawa nagawa zile receipt kwa wanafunzi tunaoona ni mazuzu, wakapeleka nyumbani lakin wajanja wajagundua tunawatania,wakazichana, sasa ziku ya kufukuza Ada ikafika akaja mwalimu maarufu kwa jina Walter wakaanza kusoma ambao hawajalipa Ada, kuna mdada mmoja mjinga mjinga kumbe Ile receipt kaiweka kwenye shati. Akasema nimeshalipiwa na ridhiwani na **** , msaala ukaanza tukaitwa mpaka kwenye ofis ya mkuu wa shule naye alikuwa mtata kweli, alivyoanza kutuadhibu mwalimu mmoja akaja kwakuwa alimuona ridhiwani pale akasema hata barua zile tulizokuwa tumeandikiwa kufukuzwa wakakaa kujadili. Wakatusamehe ila viboko tukapokea, na mwalimu akatwambia kuwa mmesamehewa kisa huyu,

Si kwamba kwa kuwa ni mtoto wa waziri bali nidhamu yake
Wakati huo tulikuwa na watoto wa vigogo wengi wanafukuzwa tu,

Hivyo tunaomba waliosoma na Makonda,

Waliosoma ma magufuli

Waliosoma na kikwete

Waliosoma na Nape

Au kiongozi yeyote weka hapa na tabia yake ya utotoni
Na ww umesoma na nani huko kajambanani!???
 
Me mimesoma na John,nakumbuka alikua mchoyo sana darasani

Siku moja bhana ilikua mtihani wa mid term nimekaa nyuma yake nikaomba anisaidie swali la 3(nafikiri atakumbuka hili tukio)akasema hajajaza kumbe kamaliza maswali yote,sasa cha ajabu siku majibu yanarudi ana 0% kumbe alikariri paper lililopita akidhani yatakuja vile vile
.
.
Ni mchoyo tangu shule hataki mwingine afanikiwe ilihal mwenyewe anaharibu
Unamaanisha John huyu huyu tunayemuita Yohana?
 
Dah kumbe kufoji mmeanza kitambo Lumumba. Anyway mi nilisoma na kingunge, alikuwa anakuja na ngozi ya mkia wa mbuzi siku ya mtihani ili kupigia mstari kwenye mtihani mana alikuwa ameinyoosha ngozi ile na kuikausha kama rula,
Hahahahah nimeshindwa kujizuia kucheka kwa sauti...
 
Heshima kwake kabisa mungu amsaidie aendeleze hekima hiyo

Na aliyekuwa anakuwa wapili ni wewe baba ?
Sio yeye ni Jamaa alikuwa anaitwa Edwin Mulokozi wakibadilishana na Nathan ( sikumbuki jina lake la mwisho) walikuwa wanabadilishana hizo nafasi ya pili na ya tatu.
Mimi nlikuwa sina muda na NAFASI ZAO, Nilikuwa naendeleza uchagga, kuwauzia sabuni na mafuta ya kujipaka + Biskuti na pipi kifua ( nyie mnaita tropical siku izi)..
 
Back
Top Bottom