Special Thread: Kwa Wazawa wa Singida tukutane hapa

Special Thread: Kwa Wazawa wa Singida tukutane hapa

Uzi huu ni mzuri kwa kutujuza vitu na maeneo mbalimbali ya mji wa Singida.Inapendeza sana,endelea kudadavu.Nitarudi baadae kuongezea niliyoyaona hapo Singida nilipolala kwa siku 6 pale Meatu Hoteli karibu na Mbacho/Kaumba/Madenyaki quest/hoteli.

Ila mji una maduka ya vipodozi mengi kuliko watumiaji wa bidhaa hizo.Ukiangalia kwa umakini watu wa huko ni weupe na hakuna dalili kama wanatumia vipodozi.Vinanunuliwa kweli au ni mapambo kutokana na kuigana biashara?Hata maduka ya nguo za ready made kutoka China yapo kibao lakini ukiangalia watu wanavaa simpo tu mitumba.Sasa hayo maduka wateja wake ni akina nani?

Inanikumbuka wakati nikiishi mitaa ya Kirumba Mwanza mdau akinunua gari aina ya Vitz/Noah/Spacio baada ya muda mfupi kwa atakayezinyaka pesa unakuta mtaa mzima umejaa vitz/noah.

Kiukweli kwa sasa Mji wa Singida unapendeza/unaendelea/unavutia tofauti na miji kama Lindi,Mtwara,Kigoma au Shinyanga iliyodumaa kwa kumezwa na Kahama/Mwanza.
Nimezaliwa singida mjini nimesoma shule ya msingi Mughanga hapo hapo singida mjini.secondary nikasoma hapohapo singida mjini shule za kata alizotuchangia Sana mbunge dewji. high level nikasoma pia hapo hapo singida shule Moja inaitwa ilongero mwisho chuo nikaja nikasomea dar.so nauelewa mkoa wa singida wote,mitaa yote kuanzia minga,karakana,kititimo,Mungumaji,mwenge,stand mpya,misuna,stand ya zamani,kibaoni,majengo,soko kubwa,mji wa zamani,ginnery,sabasaba,mtipa,unyankindi,mitunduruni,Yugo,mnada wa zamani,maduka Saba,ukombozi,sokoine,mandewa na Mitaa yote hunidanganyi,mang'ongo yote na majabali yote ya hapo mjini nayajua
Naujua mji vizuri kwa sababu wale wakina sele ndovu watoto wa chief senge wa pale utemini Ni mabraza zangu ukoo mmoja na kina tajiri mkulima wa kisasida,kipindi tunakua tulikuwa tunatembea nao sana.kwa mtu yoyote aliyekulia singida lazima awajue wakina sele ndovu jamaa ni mkubwa Sana kaenda hewani alipewa Hadi kibali Cha kuwinda porini.amekimbiza Sana miaka ya nyuma hapa pale mkoani wapo watu wengine maarufu Kama kina idada,malingumu,akwii,n.k
Matajiri wengi wa mkoa wa singida Ni wachaga ndio wenye madukwa makubwa makubwa pia hata wenyeji wanyaturu tunamiliki viwanda vya kukamua alizeti
Singida tunakunywa Sana mbege maeneo ya mwenge,mtukuru unapatikana maeneo mengi ikiwemo daima bar na kule kibaoni ndio Chaka la wahuni wote wanakunywa gongo na pia highlife inafanya vizuri sana,sigara tunazotumia Ni Winston na safari na club.msela akinywa bia amekunywa eagle na nzela banana zinafanya vizuri Sana.ukija kuanzia karakana na majengo wanapenda Sana gomba kutokea arusha Yale ma bus yanaingiza mzigo wa mrungi mapema TU saa nne au sa tano. karibu kila kijana anakula dawa wenyewe tunaita kamchongo ugoro.
Nyama pia tunakula Sana kila juma mosi tunaenda njiapanda kula nyama mnadani.matunda yetu sanasana Ni furu,mapera,malala(zambarau),sasati,lade na matogo kutokea nje ya mji au vijijini huko.mayai ya kienyeji yapo ya kutosha ukiomba ukusanyie Ni shilingi Mia mbili tu yai moja.kuku usiulize kutokea mgori au makiungu utapata kuku wa kutosha tu.
Kwa sasa hatuna viwanja vingi vya starehe tuna KBH Ipo singidani.tuna night club kwa nyokaa iko hapa stand ya zamani.sehemu za starehe Kuna Cheyo bar, mbacho, kirima bar, Serengeti, scene lodge, kwa super kitasa kitimoto ya ukweli
Kwa upande wa michezo tuna vipaji vingi Sana hasa kwenye riadha.Alphonse mwanariadha aliyepeperusha mbendera ya Tanzania na kushika nafasi ya tatu London mwaka Jana anatokea mampando tarafa ya mungaa wilaya ya ikungi.wapo wengine wengi pia timu ya singida ilifanya vizuri ilipocheza hapa Kenya.mpira wa miguu bado TUnajivuta.mpira wa wanawake unafanya vizuri Kuna vipaji sana.tuna singida United ipo ligi kuu lakini iko taabani
Kwenye upande wa siasa..kiukweli sgd Ni ngome ya CCM..kwa mfano uchaguzi wa ubunge Jimbo la singida mjini aliloliacha mo dewji mpinzani alipata kura 5000 TU wakati wa CCM alipiga kura zaidi ya 50000.vijana wengi hawana mwamko na Mambo ya siasa
Kwenye upande wa elimu tuna shule maarufu Kama mwenge high school ya advance level..nyingine za shule ya msingi maarufu Ni nyerere, Mughanga,ipembe,sumaye,misuna, sekondari pia zipo kila kata
Afya tuna hospital mpya ya rufaa iko mandewa nje kidogo ya mji
Mji unakuwa Sana hasa maeneo ya kititimo na mungumaji.kuelekea na puma mji haukui Sana
hayo Ni kwa uchache sana kuhusu mkoa wangu wa singida Kama una swali lolote kuhusu mkoa wa singida uniulize hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa hata kama hana hela ila ni smart sana ila sasa kitandani wanajua kutukomesha wanyaturu wamejaliwa mm siwataki kabisaa mtu ana bololoo kama mkono wa mtoto agrrrrr

Sent using Jamii Forums mobile app
aiyaaaaaa hao ni wa kule itigi,ulyampiti,ikungi ila sisi wa DAR mbona hatuna fujo hizo tuko kama watanga TUU
 
Back
Top Bottom