Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Hii ni SPECIAL THREAD itakayozungumzia ziara nzima kwenye mchakato wa kampeni za mgombea Urais Dr. John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Samiah Suluhu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nitakuwa naweka muendelezo kwa kila kampeni nchi nzima.
23 Agosti 2015: Uzinduzi wa Kampeni Viwanja vya Jangwani

24 Agosti, 2015: Kampeni Mkoa wa Katavi

Dr. Magufuli akihutubia wakazi wa Ifumbura wilaya ya Mpanda, Katavi

Mgombea uraisi kwa tikieti ya CCM, Dr. Magufuli akiwa Katavi leo ameahidi kufufua viwanda vilivyokufa na kujenga viwanda vipya, huku akiwapiga mkwara wawekezaji waliovinunua kuwa wakishindwa kuviendesha wavirudishe serikalini.
My take:
Miaka ya 1995 serikali ilijitoa katika biashara na CCM ikiongoza serikali iliviuza viwanda hivyo, je leo hii wataweza kutekeleza ahadi hii ya kuvifufua na kuviendesha??
Je serikali inakiri kiutu uzima kuwa ilifanya makosa kuvibinafsisha viwanda hivyo????
Hatua gani serikali yake imechukua kuwafikisha mbele ya sheria wale walioviuza kimakosa, na je wale ambao wameshindwa kuviendesha kwanini hawajafikishwa makamani kwa zaidi ya miaka 20. Je kweli kuna nia ya dhati katika hizi kauli za magufuli
Karibuni wadau kuchambua ahadi hii ya Dr. Magufuli
Source; AZAM TWO NEWS
![]()
TATHMINI; siku 10 za Kampeni ya Dr John Magufuli.
Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dr John Pombe Magufuli amehitimisha mzunguko wa Kwanza wa Kampeni yake kwa mikoa 6 ya kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Kusini ambayo ni KATAVI, RUKWA, MBEYA, NJOMBE, RUVUMA na MTWARA.
Katika kampeni zake Dr Magufuli amefanya mikutano ya hadhara takribani 49 pamoja na mikutano midogo ya kusalimia wananchi zaidi ya 126 ambapo katika mikutano yote wananchi walijitokeza kwa Maelfu kumsikiliza akiwasilisha Ilani ya CCM ya 2015-2020.
Dr Magufuli ametembea takribani Kilometa 5,900 kwa kutumia gari na maeneo mengine akitembea kwa miguu ili kukutana na Wananchi wa Makundi mbalimbali akinadi sera za CCM.
Tafiti za awali za Mashirika mbalimbali ya nje na ndani ya nchi yalionyesha kuwa CCM itashinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa zaidi ya asilimia 60, lakini baada ya kuanza kwa Kampeni na mgombea kuzunguka akifanya mikutano mikubwa ya hadhara ambayo imekuwa ikirushwa moja kwa moja (live) kupitia vituo mbalimbali vya televisheni, magazeti, redio pamoja na mitandao ya kijamii na kuwafikia watanzania takribani milioni 30, Umaarufu wa CCM na uwezekano wa kushinda umeongezeka kufikia asilimia 85 (tafiti za ndani)
Mambo yaliyopelekea CCM kuongeza umaarufu wake ni pamoja na rekodi nzuri ya uadilifu na uchapakazi aliyonayo mgombea wake, pamoja na uwezo mkubwa wa mgombea (Dr Magufuli) katika kutambua na kutoa suluhu ya matatizo yanayowakabili wananchi wa kada zote na maeneo yote ya Mijini na Vijijini.
Ilani ya CCM na namna mgombea anavyoinadi (Body language) imeongeza imani ya wananchi kwa CCM, mfano Dr Magufuli akisema anaichukia rushwa, mwili, haiba na sura yake vinaonyesha kuwa anamaanisha anachokizungumza. Ilani ya CCM imejikita katika kuleta mabadiliko kwa kuondoa Umasikini na kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira hasa kwa Vijana, kuendeleza Vita dhidi ya Rushwa na Ubadhirifu, Kuboresha huduma za jamii na kuendeleza Umoja wa Kitaifa pamoja na kudumisha Ulinzi na usalama.
Wakati Umaarufu na kukubalika kwa CCM kunaongezeka, bado inapata upinzani hafifu ktk kampeni zake. Rekodi zenye mashaka za wagombea wao zinazohusisha kashfa za rushwa, ufisadi, utendaji mbovu na uzembe. Hali tete na migogoro ya ndani ya vyama vya Upinzani ambayo imeshika kasi ktk kipindi hiki hasa kuhusu wagombea kwa nafasi ya Urais na baadhi ya majimbo. Hali ya Afya za wagombea wao ambazo zimewafanya kutoweza kufika katika baadhi ya maeneo waliyopanga kufanya mikutano mfano Ludewa na Tunduru ambapo wananchi walishakusanyika na mgombea akashindwa kutokea. Vyama vya upinzani kukosa Ilani madhubuti na hivyo wananchi kupunguza imani yao kwao.
NB;
Katika moja ya utaratibu bora kabisa wa Chama Cha Mapinduzi ni ule wa kujifanyia tathmini katika kila hatua ya mpango ama jambo lake lolote, utaratibu huu umeiwezesha CCM kubaki kuwa relevant na kuendelea kuaminiwa na kupendwa na watanzania walio wengi.
Hii ndio ilani ya CCM uchaguzi mkuu 2015!
Uchambuzi wa ahadi za John Magufuli
Maelfu wampokea Magufuli na kuhutubia Tunduma
John Magufuli akiwa katika Kampeni Mbeya
Magufuli Apokewa kama MFALME => CHUNYA
Samia: Tanzania ina chuma itakayovyunwa miaka milioni 200
Samia ateka Singida
Yanayojiri mkutano wa Mgombea Urais wa CCM, John Magufuli viwanja vya Majimaji, Songea
Dodoma: Mwendelezo wa Kampeni za Mgombea Mwenza wa CCM, Samia Suluhu baada ya kuiteka
Hotuba ya Magufuli na Sekta ya Elimu
Kutoka Uwanja wa Mashujaa Mtwara: Mkutano wa Kampeni za mgombea Urais CCM
Hii kauli ya Magufuli imenitisha sana
Magufuli: Nilikwepa vishawishi vya rushwa
Ziara ya Mgombea Mwenza Samia Suluhu kwa Tiketi ya CCM jijini Dar es Salaam
Tathimini: Siku 10 za kampeni ya Dr. John Magufuli
Morogoro: Magufuli - Elimu Bure kuanzia Msingi hadi Kidato cha Nne; Makamba awavaa Lowassa,
Samia Suluhu ahaidi Umeme kila Kijiji Ruvuma
Yaliyojiri uwanja wa Tangamano, Tanga: Mkutano wa Mgombea Urais wa CCM, John Magufuli
Yaliyojiri mkutano wa Mgombea Urais wa CCM, John Magufuli wilaya za Mkinga, Korogwe na Lushoto
Ziara ya Dr. Magufuli wilaya ya Handeni, awanadi Mboni Mhita na Dr. Kigoda
Ziara ya Dr. Magufuli Mkoani Mara; Atembelea kaburi la baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere
Kutoka Mkendo: Mkutano wa kampeni wa chama cha Mapinduzi mjini Musoma
Maelfu ya wanachama wa CHADEMA wampokea Dr. Magufuli na kujiunga na CCM
Igunga yazizima kumsikiliza Magufuli
Kutoka Tabora: Kampeni za chama cha mapinduzi uwanja wa Ali Hassa Mwinyi
Yaliyojiri kampeni Tabora: Mikutano ya Magufuli kutoka Sikonge, Kaliua na Urambo
CCM: Magufuli yupo tayari kwa Midahalo; tuna kila dalili ya Ushindi
Yanayojiri Mikutano ya Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dr. John Magufuli mkoa wa Kigoma
Yanayojili mkutano wa Dr. Magufuli Jimbo la Buhingwe -Kigoma 17 Septemba, 2015
Yanayojili mikutano ya Samia Suruhu, Newala Vijijini, Newala Mjini na Nanyamba
Yaliyojiri: Mkutano wa Mgombea wa CCM, Dr. Magufuli jimboni Chato, Geita - Septemba 20, 2015
Yaliyojiri: Mkutano wa Mgombea wa CCM, Dr. Magufuli jimboni Bukoba Mjini, Kagera - Septemba 21,
Yaliyojiri: Mkutano wa Mgombea wa CCM, Dr. Magufuli jimboni Karagwe - Septemba 22, 2015
Yaliyojiri kampeni za Magufuli wilaya ya Misenyi- jimbo la Nkenge
YALIYOJILI: Mkutano wa mgombea urais wa CCM Dr John Pombe Magufuli wilayani Ngara
Yaliyojiri: Mkutano wa Mgombea wa CCM, Dr. Magufuli jimboni Geita - Septemba 23, 2015
Mama Samia aziteka Handeni, Kilindi, Kiteto na Nchemba -Tanga
Mkutano wa Dr. Magufuli kutoka uwanja wa Kwaraa-Babati Manyara, Oktoba 4, 2015
DR. Magufuli atinga Monduli, atembelea kaburi la aliyekuwa waziri mkuu hayati Moringe Sokoine
Yaliyojiri Jijini Arusha: Mkutano wa Mgombea wa CCM, Dk. Magufuli – Oktoba 6, 2015
[URL="https://www.jamiiforums.com/uchaguzi-tanzania/949288-ziara-ya-magufuli-jimbo-la-vunjo-lyatonga-mrema-aungana-na-ccm-kwenye-kampeni.html"]
Ziara ya Magufuli jimbo la Vunjo: Lyatonga Mrema aungana na CCM kwenye kampeni
[/URL]
Last edited by a moderator:





