Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Sasa unawaelewesha watu kuhusu Magufuli au unaponda watu? Kweli CCM mmechoka? Kama issue ni kafanya nini jimboni kwake, kwani Nyerere aliifanyia nini Butiama?
 
Kweli unambeba mv dar es salaam mbovu tangia ununuliwe imefanya safari mara moja tu deni la makandarasi trilion moja faini ya kuchelewa kulipa billion tisa malipo hewa wizara ya unjenzi billion 253 vilevile hasara billion 3 na kauza nyumba za serikali kwa bei ya kutupa na wamejiuzia wenyewe kweli utendaji wake umetisha.
 
1.Magufuli arudishe kwanza nyumba za serikali alizowauzia maswahiba wake kwa bei ya kuku na kusababisha watumishi wa umma kuishi hotelini hivyo serikali kupata hasara ya mamilioni ya shilingi.

2.Magufuli aliisababishia serikali hasara ya mabilioni ya shilingi kwa maamuzi yake ya kukurupuka ya kukamata Meli ya uvuvi ya Wachina matokeo yake serikali ilishindwa kesi mahakamani na kutakiwa kulipa fidia.

3.Barabara nyingi za Magufuli zimeanza Kubomoka kabla hata hazijamaliza miaka miwili kwa kuwa zimejengwa chini ya kiwango kutokana na rushwa.
 
Bora nilale kuliko kumpa kura magufuli! mfumo dhalimu na ahadi zisizotekelezeka mwisho tarehe 25/10. Tulitegemea mengi kwa Jakaya mwishowe tumeambulia kuitwa Malofa!! Mtaelewa ulofa tarehe 26/10.
 
Waandishi Wetu Toleo la 420 28 Aug 2015

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, ‘amepora' ajenda kuu ya aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Ajenda kuu ya Dk. Slaa kwa wakati huo, na ambayo alidumu nayo hata kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, yaani akiwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwakilisha Jimbo la Karatu na vile vile, akiwa Naibu Kiongozi Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, katika Bunge la Tisa lililokuwa likiongozwa na Samuel Sitta, kama Spika, ilikuwa ni vita dhidi ya ufisadi.

Ni ajenda hiyo hiyo ambayo, ilikitambulisha Chadema kama taasisi ya kisiasa yenye uwezo wa kudhibiti ufisadi kupitia kwa Dk. Slaa, ndiyo sasa imevaliwa njuga rasmi na Dk. Magufuli, ambaye, kupitia Ilani ya CCM ya sasa, amesema mafisadi wataundiwa Mahakama Maalumu ya kuharakisha mwenendo wa kesi zao.

Ilivyokuwa kwa Dk. Slaa 2010

Ilikuwa wakati wa kampeni za mwaka 2010, (Septemba, 2010), katika mwendelezo wa kuwahamisha wananchi kuchukia ufisadi na kumuunga mkono ili aukomeshe nchini, Dk Slaa alihutubia mikutano mikubwa ya hadhara kadhaa mkoani Mwanza.


Akiwa katika majimbo ya Geita, Buchosa na Nyamagana, kwa wakati huo kama mgombea urais, Dk. Slaa alijigamba kiasi cha kudai, aliyekuwa mgombea mwenzake wa urais kwa wakati huo, sasa Rais Jakaya Kikwete, alikuwa akiukabili ufisadi katika serikali yake kutokana na shinikizo lake (Slaa).


Dk. Slaa alidai Kikwete ni saizi yake kwa kuwa alikuwa akitekeleza maagizo yake (Dk Slaa) katika kipindi cha miaka minne iliyopita, kwa kuwa alikuwa akikabiliana na ufisadi aliokuwa akiuibua yeye. Karibu katika kila alikokuwa akifika kwa ajili ya mikutano yake ya kisiasa, Dk. Slaa alikuwa akikutana na mabango ya wananchi wanaoelezea namna wanavyokerwa na ufisadi.


Mbali na ajenda ya ufisadi, ajenda nyingine aliyokuwa akiisimamia Dk. Slaa katika kampeni zake za mwaka 2010 ni elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu na katika hilo, kwa sasa, Dk. Magufuli ameahidi kutoa elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne, huku akiahidi kukomesha kero zinazojitokeza katika upatikanaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.


Masuala hayo mawili, yaani kuanzishwa kwa Mahakama Maalumu ya kushughulikia wale ambao Dk. Magufuli, katika uzinduzi wa kampeni zake Jangwani, jijini Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita, aliwaita "majizi na mafisadi" na suala la elimu bure, si tu ahadi ya mgombea huyo pamoja na mgombea wake mwenza, bali ni ahadi ya Chama Cha Mapinduzi, kupitia Ilani yake.


Hali hiyo inajitokeza katika wakati ambao, mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na umoja wa vyama vingine vitatu – Chama Cha Wananchi (CUF), NLD na NCCR-Mageuzi, Edward Lowassa, akitarajiwa kuzindua kampeni zake za urais Jumamosi, wiki hii, Jangwani jijini Dar es Salaam, ambako ndiko Dk. Magufuli alikofanya uzinduzi wake.


Msimamo wa Chadema dhidi ya ufusadi

Tayari Chadema kimekwishakutoa msimamo wake kuhusu ufisadi unaoendelea nchini na kwa sasa, kati ya majukumu ya mgombea wake wa urais, Edward Lowassa, wakati wa kuomba kura ni kujenga imani kwa wapiga kura kwamba ataibeba ajenda hiyo, zaidi ya Dk. Magufuli au hata Dk. Slaa ilivyokuwa mwaka 2010, hali ambayo, hata hivyo, inamuweka Lowassa katika wakati mgumu kwa kuwa naye amekuwa akihusishwa na ufisadi.

Katika msimamo wa Chadema, kwa mfano, Mei mwaka huu, 2015, walikemea kwa kurejea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ambaye pamoja na mambo mengine, ripoti yake iliibua ufisadi uliohusisha upotevu wa takriban shilingi trilioni


1.151 ndani ya Serikali Kuu pekee.
Na zaidi ya upotevu huo, ilibainika vile vile kwamba, hata makusanyo yote yaliyotokana na kuongezeka kwa kodi katika mwaka wa fedha 2013/2014 yaliyeyuka.

Katika taarifa yake hiyo ya Mei, Chadema kilieleza; "Chadema kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za ufisadi wa kutisha uliofanyika kwenye matumizi ya fedha za umma kama ilivyobainishwa kwenye ripoti za ukaguzi wa fedha kwa mwaka 2013/2014 zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).


"Tunapenda kutoa taarifa ya awali kama ifuatavyo; Wizara tatu, Trilioni 1.151 zimepotea. Tumebaini kuwa kwa upande wa Serikali Kuu pekee zaidi ya shilingi trilioni 1.151 zimepotea au kuliwa na wajanja walioko serikalini, kiwangio hiki ni sawa na asilimia 5.231 ya Bajeti yote ya serikali kwa mwaka ujao wa fedha 2015/2016."


Ni kutokana na taarifa za namna hiyo, Lowassa pamoja na mgombea mwenza wake, Juma Duni Haji watahitaji kuwashawishi wananchi kwamba wao, vile vile, wanaweza kuongoza vita dhidi ya ufisadi na wananchi wakawaelewa na kisha kuwapigia kura, kinyume chake, inaelezwa na wachambuzi wa masuala ya siasa kwamba, Chadema itakuwa imepiga teke rasmi ajenda yake ya vita dhidi ya ufisadi, iliyoongozwa vyema na Dk. Slaa.


Maoni mchanganyiko kwa Magufuli

Wakati Lowassa akisubiriwa kuzindua kampeni zake na hasa kuweka bayana ahadi zake katika kuomba kura, tayari watu mbalimbali wamezungumzia ahadi za Magufuli, zikiwamo hizo zinazotafsirika kuwa "zilizokuwa ajenda" za Dk. Slaa.

Ni kwamba, pamoja na ajenda hizo, hata ile kauli ya Dk. Magufuli, Jangwani Dar es Salaam ya kuwatahadharisha maofisa wenye kukwamisha wawekezaji nchini kutafuta kwa kwenda endapo ataingia madarakani, imeonekana kuwavutia zaidi wawekezaji wazawa.


Kauli hiyo aliitoa akizungumzia uwekezaji kwenye viwanda kama moja ya vipaumbele vyake, akisema; "Maofisa wataokwamisha uwekezaji viwanda watafute kwa kwenda."


Inaelezwa kwamba eneo la uwekezaji ni kati ya sekta zinazotajwa kuwa uchochoro wa ufisadi.


Akitoa maoni yake kuhusu vipaumbele vya mgombea huyo, Makamu wa Rais TCCIA, Julius Kaijage, alisema kuwa kauli ya mgombea huyo inaonyesha dhamira yake katika kusimamia utekelezaji wa majukumu waliyokabidhiwa.


"Tatizo la nchi hii si sera au ilani, tatizo hapa ni utekelezaji na usimamizi wa karibu wa utekelezaji huo," anasema Kaijage.


Makamu huyo wa TCCIA anabainisha kuwa mgombea huyo ameweka wazi kuwa katika uongozi wake, mbali na kuukabili ufisadi, atasimamia kwa karibu utendaji serikalini na kuchukua hatua stahiki kwa wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao, utamaduni aliosema ulitoweka, huku watendaji wakifanya watakavyo na vitendo vyao hivyo viliudhi wananchi lakini hawakuchukuliwa hatua.


Usimamizi wa karibu wa utendaji kwenye serikali, unaelezwa ndio utakaowezesha kuleta mapinduzi ya viwanda nchini, kwamba katika hotuba yake, Dk. Magufuli amefanikiwa kuonyesha mikakati ya kiutendaji katika kuendeleza sekta ya viwanda nchini.


Katika eneo la kodi, Makamu huyo wa TCCIA ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya fedha, anaichukulia kauli ya Magufuli kwa uzito wake akiamini kuwa anao uwezo kusimamia anachokiamini, kwamba watu wote walipe kodi, wafanyabiashara wakubwa na wadogo, wafanyakazi na viongozi, hususani wanasiasa wakiwemo wabunge anaosema haoni mantiki ya viongozi ya kupewa misamaha wakati vipato vyao ni vikubwa.


Mtaalamu wa biashara za mazao ya kilimo na uongezaji wa thamani ya mazao ya kilimo, Kanyiki Sokolo anakubaliana na mtazamo wa mgombea huyo wa urais kupitia CCM, kuhusu uendelezaji wa sekta ya kilimo na viwanda, akisema ni sekta zinazotegemeana katika kuleta mapinduzi ya kiuchumi.


Hata hivyo, Kanyiki anatoa angalizo moja, kwamba kipaumbele katika uendelezaji sekta hizo mbili kiwekwe kwa wawekeaji wa ndani badala ya kutegemea wawekezaji toka nje.


"Huwezi kuleta watu wa nje kuja kununua mtama, wanauongeza thamani kisha wanauza nje na kupiga mapesa, yale mamitambo yapo na hayana gharama kubwa, benki zikopeshe wazawa, wawekeze, pesa ibaki ndani," anasema Kanyiki.


Kanyiki anamuona mgombea huyo kuwa na uwezo wa kusimamia yale anayoyaamini, akizingatia utendaji wake ndani ya serikali kwa kipindi cha takribani miaka 20.


"Wakati umefika Tanzania kutotegemea viongozi aina ya Mwalimu Nyerere, hatuhitaji wana falsafa sasa, tunahitaji watendaji, watu aina ya Hitler, anaagiza kutengenezwa gari, linatengenezwa, inashindikana wahusika wanaenda na maji, hapo ndipo tutapata maendeleo, huyu bwana anazo hizo sifa," anasema Kanyiki.


Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), Profesa Joseph Msambichaka amevutiwa zaidi na mtazamo wa mgombea huyo kuhusu mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu, akisema itasaidia kusukuma maendeleo ya elimu, hususani sayansi na teknolojia.


Kwa mujibu wa Profesa Msambichaka usimamizi makini wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, utaondoa usumbufu na kusukuma uzalishaji wataalamu watakaotumika kusukuma maendeleo ya nchi.


Makamu Mkuu huyo wa Chuo, amejenga imani kufanikiwa kwa suala la mikopo kwa wanafunzi kutokana na rekodi nzuri ya mgombea huyo katika usimamizi wa utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara nchini akiwa Waziri wa Ujenzi.


"Kwa rekodi yake tunatarajia atatekeleza ahadi yake," anasema Profesa Msambichaka.


Katika hotuba yake wakati wa uzinduzi wa kampeni zake, Dk. Magufuli aliainisha vipaumbele mbalimbali, kama vilivyoainishwa kweye ilani ya uchaguzi ya CCM, miongoni mwake ikiwemo kuendeleza sekta za viwanda, kilimo na mifugo kukuza uchumi na ajira.


Vipaumbele vingine ni pamoja na umoja wa kitaifa, muungano, ulinzi na usalama, utawala bora, kodi, madini na gesi, miundombinu ya barabara na reli, bandari, usafiri wa anga, maji, elimu na afya.


Pamoja na yote hayo aliweka bayana vita yake dhidi ya ufisadi akisema atauda mahakama maalumu kushughulikia wezi wa mali ya umma na mafisadi, ili kesi zao ziharakishwe na wahalifu wachukuliwe hatua pasipo kucheleweshwa.


- See more at: Raia Mwema - Dk. Magufuli abeba ajenda ya Dk. Slaa


 
Kama yupo vizuri si mtulie kuna haja gani ya kuitisha vikao vya wakuu serikalini kule Ngurudoto kuzungumzia jinsi ya kumdhibiti mtu mliyemzidi kwa 100%?
 

Huyu mamvi ni msakatonge tu anataka mabadiliko gani mbona kwao wamasai wanalalamika maji hakuna wanateseka kwa kua na hudumambovu za kijamii kam afya elimu sasa kwa nchi nzima ataweza?
Suala la ajira ukiangalia kwa jamii yake ya kimasai ndio wanaongoza kwa umasikini na kupata ajira mbaya za kua walinzi wa majumba ya watu tu mbona hajawatatulia? ndio aje aweze kutoa ajira kwa watanzania wote
Huyu mamvi anavodai anachukia umasikini mbona alishawahi kua waziri mdogo wa kupandana na umasikini kwenye ofisi ya makamu wa rais na hakufanya lolote. Watanzania tubadilike na tumchukie huyu kidudu mtu wa nchi yetu ya tanzania
Namaliza kwa kusema upawa expitre date yao ni 0ct 25
#HAPAKAZITU
 
Pamoja na kwamba mnadai kumzidi kwa 100% bado mnaonekana mna hofu na kupaniki kusiko kwa kawaida huku mkiporomosha matusi makubwa pasi na kujali utu! Mpaka hapa tunapata mashaka kuwa mmemzidi au mmezidiwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…