Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Lowasa anachoweza ni ufisadi menginie mtamuonea.

Jamaa ni bingwa wa kupiga madeal na rafiki yake Rostam Azizi. Mpaka leo wanatutesa na biashara yao ya majenereta ya kuzalisha umeme. Jamaa wanavuta pesa ndefu sana toka TANESCO kila siku (around milioni 152 kila siku). Sasa hapo atashindwa kuwanunua akina Mbowe kwa bilioni 10.
 
Watanzania tuna imani na Magufuli

Na hawa hapa chini je? Ni Wachina ama Warusi?

attachment.php

​
 
MAGUFULI NI ZAIDI YA LOWASA KWA 100% KIUTENDAJI:

Mgombea mteule wa CCM, Mh Magufuli ameonyesha uwezo wa hali ya juu kiutendaji akiwa waziri zaidi ya Mzee Lowassa katika kipindi chake akiwa waziri. Mh Magufuli ameonesha uthubutu katika majukumu yake katika wizara alizopita.

Wote hawa wawili wamelitumikia taifa hili katika nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Uwaziri. Kati ya hawa wawili, mmoja ambaye ni Magufuli kote alikopita ameweka record ya kipekee kiasi cha kuwafanya wananchi wengi kutamani apewe majukumu makubwa zaidi.

Mh Magufuli, amekua tunu hata wizara nyingine alizokwenda na kumfanya ang'are zaidi tofauti na mzee Lowassa, katika wizara zote alizopita hakuna jipya alilolifanya zaidi ya kuacha malalamiko ya kero mbalimbali.

Mh Magufuli ndiye aliyeokoa upotevu wa magari ya miradi ya serikali ambayo watumishi wengi walikua wakijimilikisha magari hayo na kuyatumia vibaya kwakua yalikua na namba za kiraia na baadae akaanzisha program kuweka namba mpya za magari yote ya serikali, Mh Magufuli akiwa wizara ya ujenzi Watanzania tumempongeza sana na kwa juhudi,uboreshaji wa miundo mbinu kama barabara za kisasa, hakika huyu ndio kiongozi tunaemhitaji kwa sasa.

Mh Magufuli alipambana na wavuvi haramu waliokua wanatumia mabomu na nyavu haramu ijapokua wengine wachache walimchukia lakini wananchi wengi tumempongeza kwa kazi nzuri hata akiwa wizara ya mifugo, Magufuli mara nyingi ameonekana akiwa sites mbalimbali za ujenzi akisimamia shughuli zinazofanyika iwe usiku au mchana akishirikiana na sisi wanainchi. Hakika huyu ndiye kiongozi tunayehitaji kwa sasa.

Jimboni kwake, Mh Magufuli kupo vizuri barabara za lami, shule, ujenzi vituo bora vya afya na amekuwa karibu sana na wanainchi wake ukilinganisha na Lowassa kule Monduli. Lowassa katika kipindi chake wizarani ametumia fursa hiyo kujilimbikizia mali, kufanya biashara haramu na mataifa ya Ulaya, alijikita katika kutengeneza makundi yasiyokuwa na tija kwetu sisi wanainchi na zaidi kutuongezea umasikini.

Kama wazalendo tujiulize, huyu Lowassa anayedai kuchukia umasikini, katengeneza ajira ngapi kwa vijana wa Monduli? Zaidi ya maigizo anayofanya makanisani na misikitini, atueleze ni bodaboda wangapi kawapa mitaji zaidi ya kuwaburuza hususani wale wasiojitambua, vijana wengi wa kimasai kawapa fursa kiasi gani zaidi ya kukimbilia Dar es Salaam?

Kwa miaka zaidi ya 20 akiwa kiongozi hajaonesha nia ya dhati ya kumkomboa kijana, ataweza vipi kwa sasa na uzee unaomkabili ukiachilia maradhi anayokabiliana nayo. Alipokua waziri Mkuu Wafuasi wake wamekua wakimpongeza sana kwamba ana maamuzi magumu ambayo kama ni shule za kata zimechangiwa na wanainchi chini ya ilani ya chama cha CCM, yeye alikuwa na jukumu la kusimamia zoezi hilo tu.

Jimboni kwake kwenyewe hakuna maendeleo yeyote yale, maisha ni magumu sana kuliko majimbo mengine.
Zaidi ya kujilimbikizia mali hakuna jipya alilofanya mzee Lowassa pamoja na kupendwa na bodaboda wachache wasiojitambua maana ukiwauliza kwanini wanampenda watakujibu basi tumempenda tu"

Ahahahaaa, wengine watakujibu kuwa wanataka mabadiliko, sasa hebu jiulize mabadiliko gani atakayokuletea wakati Jimboni kwake kwenyewe ni njaa tu!!! Ninachokiona kwa babu yetu ni safari ya Matumaini kweli!!

#HapaKaziTu
 
  • Thanks
Reactions: Hel
Tatizo nyota. Anajitahidi kulazimisha kuonyesha kuwa anakubalika kwa kukusanya watu kwa Malori na kuzunguka na wasanii.

Kama unakubalika, kwanini uzunguke na wasanii?

Vijana wamejiandikisha kwa wingi na wana hali ya Uchaguzi. Kila unapopita vijana wanasema 'Wamechoka'. Vijana wanataka mabadiliko.

Mabadiliko sio kuwa bingwa wa kukariri hotuba. Hotuba aliyotoa kijiji A, ameirudia B, ameirudia C, ameirudia D.

Anazungumzia tatizo la mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya juu. Anasema pesa ipo. Mbona mkigoma inatoka? Hata wewe?

Mbona mnatuchanganya?
 
Kiongozi!

Huna haja ya kuchanganyikiwa. Tunza KICHINJIO chako. Wengi tupo tunasubiri 25/10/2015 CCM iingie rasmi machinjioni. Naamini kichinjio chako unaendelea kukipa makali. Asubuhi sana na mapema ya 25/10/2015 ielekeze CCM KIBLA halafu, kitakacho fuata ni Mh. Jaji Lubuva kutangaza rasmi umarehemu wa hiki chama.

Nina hasira kama wewe!
 
Maku ww
 
Chinja CCM kwa Maslahi mapana ya Watanzania .. Umati unaokwenda kwenye mikutano ya CCM wanakwenda kupata burudani ya Muziki wa kizazi kipya tu .. hakuna jipya hapo ..
 
Kiongozi!

Huna haja ya kuchanganyikiwa. Tunza KICHINJIO chako. Wengi tupo tunasubiri 25/10/2015 CCM iingie rasmi machinjioni. Naamini kichinjio chako unaendelea kukipa makali. Asubuhi sana na mapema ya 25/10/2015 ielekeze CCM KIBLA halafu, kitakacho fuata ni Mh. Jaji Lubuva kutangaza rasmi umarehemu wa hiki chama.

Nina hasira kama wewe!

Naona hasira zangu mm zimezidi aisee naisubr 25 octbr kwa hasira zote yan ni kuchnja na kulinda kura kwa nguvu zote
 
Nyie pigeni kelele
bwabwajeni ovyo
Andamaneni
Zomeeni.
Sie ni kupiga kura tuu!
 
Ayaa wee! Mimi kichinjio changu nimeweka makali kama ya wembe. CCM akielekezwa kibla nikikata anakufa kwa sekunde moja! Vivaaaaa UKAWAAAAAAAA! VIVA Lowassaaaaaa! CCM na wasanii wake! UKAWA NA wananchi wake!
 
Kwa taarifa za uwakika nilizo nazo hakuna gamba litaweza kumpiku Dr Magufuli, magufuli uwenda akashinda kwa asilimia 85% mpaka 90% ktk uchaguzi unaokuja. Iman ya watanzania wengi ipo kwa Dr Magufuli kutokana na record yake yakuchapa kaz nakutimiza sera za maendeleo ya taifa, sio muoga kutetea ukweli wala sio muoga kusimamia ukweli. Mungu akambariki mpaka siku yakumkabidhi taifa. Amen
Basi mimi mwenzio nina uhakika 150% Lowassa ndio rais ajaye! CCM imechokwa kila mahali.
 
Back
Top Bottom