Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

kawaulize watu wa kitengo matokeo ya utafiti wao yanaonyesha hali ikoje..... wenzio hapo Lumumba wengi wamesoma alama za nyakati kwa nini wewe? inaonyesha bado kijana mdogo uliyeshauriwa vibaya, plz acha kufifisha ndoto yako huko hakukufai rafiki
 
Uongo kama huo mlituambia kuhusu Kikwete.Oh mchapa kazi, anajua matatizo ya Wananchi na sifa nyingine nyingi. Matokeo yake kila mtu anayajua. Rais mbovu kuliko wote walio mtangulia.
 
Kwa taarifa za uwakika nilizo nazo hakuna gamba litaweza kumpiku Dr Magufuli, magufuli uwenda akashinda kwa asilimia 85% mpaka 90% ktk uchaguzi unaokuja. Iman ya watanzania wengi ipo kwa Dr Magufuli kutokana na record yake yakuchapa kaz nakutimiza sera za maendeleo ya taifa, sio muoga kutetea ukweli wala sio muoga kusimamia ukweli. Mungu akambariki mpaka siku yakumkabidhi taifa. Amen

mmerogwa si buree.jk mwenywe. mwaka 2010 alikomea <65% leo hii iwe 85%makubwa
 
Hatuhitaji rais mchapakazi, ila tunahitaji rais mwenye maamuzi magumu na watendaji wachapakazi. chama alichokuwepo kina watu mizigo ambao hata magufuli angekuwaje bado ataangushwa tu ndio maana tunataka tukipumzishe kwanza.

Mizigo yote inapuputikia UKAWA...unasemaje kuhusu hilo binti?
 
watanzania msidanganyike hatuhitaji mtu tunataka mfumo mpya hivi magufuli ataweza kuimeza ccm yenye mtu kama chenge,tibaijuka,magufuli,wanriz,nk hawezi.
 
maisha ya ccm ndo haya tunayoyaisho tusitegemeee jipya kamwe. ukawa nayo kubna mawili wanaweza kubadilisha au wakaharibu maoni yangu ndo hayo kila mtu anayo akili yake na anajua cha kufanya
 
Hatuhitaji mtendaji bali tunahitaji kiongozi wa kututoa hapa tulipo..Lowassa atosha
 
Wanawake ndyo wakwanza kunyanyapaliwa nchi hii lakin hawajitambui hatq kdgo wakipewa vinguo tayar kwishaa
 
sishangai mnavyo jifariji watu wa Lumumba na hata kujitoa ufahamu.Mwenyekiti wenu kwa makusudi kabisa pale jangwani aliwaambia picha za mikutano ya Lowassa ni za kuunganishwa wakati ukwel anaujua na ccm wote wanajua ila ni unafiki unaozidi uchawi kwa watu wa ccm.Basi hata sasa mnajua Lowassa ndie kipenzi cha wa TZ kwa sasa na ndie rais ajae,mioyoni mwenu mnakiri hilo ila mbele ya macho ya watu mnajitoa ufahamu.
 
Kwa taarifa za uwakika nilizo nazo hakuna gamba litaweza kumpiku Dr Magufuli, magufuli uwenda akashinda kwa asilimia 85% mpaka 90% ktk uchaguzi unaokuja. Iman ya watanzania wengi ipo kwa Dr Magufuli kutokana na record yake yakuchapa kaz nakutimiza sera za maendeleo ya taifa, sio muoga kutetea ukweli wala sio muoga kusimamia ukweli. Mungu akambariki mpaka siku yakumkabidhi taifa. Amen

Ahadi za JK kwenye kampeni za kusakaurais 2010
============================

1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora

2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini

3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria- Igunga

4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga

5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma

6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini

7. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma

8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera

9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi- Kagera

10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba- Bukoba Mjini

11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini

12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera

13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera

14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu- Kagera

15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya

16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba- Kagera

17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali

18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika- Mwanza

19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza

20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita

21. Kulinda muungano kwa nguvu zote- Pemba

22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro

23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa- Mbeya mjini

24. Kujenga bandari Kasanga ¨CRukwa

25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea

26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya

27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga

28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa

29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani ¨CKihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro

30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini

31. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora

32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu

33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini

34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)- Hydom Manyara

35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa-Musoma

36. Kulinda haki za walemavu- Makete

37. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini

38. Kujenga barabara Musoma¨CMto wa Mbu Arusha-Arusha

39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini

40. Kujenga barabara ya lami Manyoni- Kigoma¨C Kaliua,Tabora

41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi- Arusha Mjini

42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma

43. Kuwafidia wanakijiji ng¡¯ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido

44.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga

45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha ¨C Arusha mjini

46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo- Busekera, Wilaya ya Musoma, .

47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido

48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti ¨C Ngorongoro

49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara

50. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini

51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa

52. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa

53. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania- Iringa

54. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda

55. kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara

56. kuwapa wanawake nafasi zaidi- Kilolo ,Iringa

57. ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar

58. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa- Kabandamaiti mjini Zanzibar

59. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti

60. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma

61. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma

62. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) ¨CRuvuma

61. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania ¨CRuvuma

62. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam

63. Mtwara kuwa mji wa Viwanda ¨CMtwara

64. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha

65. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa- Kibaha

66. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha

WEKA USHABIKI PEMBENI NIAMBIE SERIKALI YA CCM IMEFANIKIWA VIPI KATIKA HAYA ILI TUIPE RIDHAA YA KUTUONGOZA TENA
 
Hahahahahaha matumaini tu hayo hapa hakuna cha 85 wala 90 hapa km atashnda atapata 35% maana si ndo mnapinduaga?
 
Back
Top Bottom