Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Toka kuanza kampeni za urais mwaka huu, Mgombea urais wa CCM, John Pombe Magufuli amekuwa akiomba kura kwa kuelezea zaidi mapungufu makubwa ya serikali ya CCM toka kupata uhuru kwa namna ilivyoshindwa kuondoa Umaskini, Ujinga, Magonjwa, Rushwa na Uonevu katika kipindi cha zaidi ya miaka 50.

Mtindo huu wa kujinadi, watanzania waliuzoea zaidi kuusikia kutoka kwenye vyama vya Upinzani kwa sababu wao hawana serikali hivyo ni vigumu kuwaelezea watanzania mafanikio yaliyoletwa na Upinzani.
Jambo la kushtukiza na kushangaza kabisa mgombea urais wa CCM, Magufuli ameamua kuchagua upande wa kukosoa utawala wa CCM wa miaka zaidi ya 50.

Je, mtindo huo wa Magufuli, una tija yoyote kisiasa kwa CCM kwa wakati huu wa Uchaguzi?

Hii ni mada nzuri sana mkuu. Changamoto anayokumbana nayo mgombea huyu wa ccm ni kwamba ataiuzaje ilani yake kwa wapiga kura bila kuzungumzia matatizo mengi ya watanzania? Mengi hayajatendeka so ana kazi kubwa!
 
Wanaukumbi

Nimefuatilia hotuba ya umimi ya Magufuli toka viwanja vya Majimaji Songea nikabaini kuwa hakuitaja ccm hata mara moja.

Badala yake utasikia Songea hoyeee..mimi Magufuli...Mniamini,mimi magufuli najua kazi...mimi..magufuli nataka..UKAWA wanadanganya mimi ntawatumikia..

Je kuna ugombea binafsi hapo?

Mgombea kuweka umimi yaonekana katumwa,baada ya hapo watamremot sana tu..nadhani ifike sehemu wagombea tuwapime kwa UONGOZI SHIRIKISHI..
Sio mimi nilifanya nikiwa wapi kwa hiyo naweza.

Yajionyesha tutampata kiongozi wa kutekeleza mawazo yake hata akiamka asubuhi bila kushirikiana na wananchi waliomchagua.

Kusema sana,kujua kilomita za barabara sio uongozi..kichwa kinatakiwa kitulie.

TAHADHARI.
 
Anajitangaza kuwa achaguliwe yeye huku akielezea matatizo lukuki ya utawala wa ccm, amekuwa hataji sana ccm na hata kuchomekea kibwagizo cha ccm hoyeee. Anajitangaza yeye kama mgombea binafsi.
 
Hili ni Taifa laifa la kulalamika, wananchi wanalalamika na hata wale wanaolalamikiwa nao wanalalamika, hii ni kuthibitisha bila ya chembe isiyo na shaka kwamba wameshindwa lazima waondoke waachie wengine watakao tafuta suluhu ya matatizo yetu mungu ibarik Tanzania tuiweke pembeni CCM
 
Toka kuanza kampeni za urais mwaka huu, Mgombea urais wa CCM, John Pombe Magufuli amekuwa akiomba kura kwa kuelezea zaidi mapungufu makubwa ya serikali ya CCM toka kupata uhuru kwa namna ilivyoshindwa kuondoa Umaskini, Ujinga, Magonjwa, Rushwa na Uonevu katika kipindi cha zaidi ya miaka 50.

Mtindo huu wa kujinadi, watanzania waliuzoea zaidi kuusikia kutoka kwenye vyama vya Upinzani kwa sababu wao hawana serikali hivyo ni vigumu kuwaelezea watanzania mafanikio yaliyoletwa na Upinzani.
Jambo la kushtukiza na kushangaza kabisa mgombea urais wa CCM, Magufuli ameamua kuchagua upande wa kukosoa utawala wa CCM wa miaka zaidi ya 50.

Je, mtindo huo wa Magufuli, una tija yoyote kisiasa kwa CCM kwa wakati huu wa Uchaguzi?

Mtaji wa ccm ni umbumbu wa watanzania, kama watanzania wakiweza kuhoji hilo, hakika ccm itashindwa vibaya sana, lakini hofu yangu ni upumbavu wa watanzania!
 
Pole sana Mkuu. Kwani Lowasa alipohutubia pale Jangwani aliitaja CHADEMA ama UKAWA? Magufuli amekuwa mtiifu kwa CCM siku zote. Huwezi kuanzisha propaganda za kipuuzi wakati huu
 
Magufuli kawaacha UKAWA wakiwa ndembendembe. Wanamgwaya sana. Ndani ya wiki tu kawachakaza ile mbaya
 
Sera zilishaisha zamani CCM kilichobbaki ni kuongea hovyo hovyo ndicho anafanya magufuli kwa sasa
 
kweli yeye ndo wa kusimamia kuzoa taka mjini?
manispa iko wapi tatizo hamjielewi mnachanganya mambo,kwa namna yoyote magufuli ndo rais ule mtandao wa majizi yaliyokalia kiti cha dr slaa kamwe hautaingia ikulu,


ni selekeli ya ccm, ndo inayo kusanya kodi
 
EL alitaja neno UKAWA na kibwagizo cha Peopleees Mara nyingi tu na hiyo ndiyo CHADEMA! au ilikuwa unaucharaza wa pono?!

Pole sana Mkuu. Kwani Lowasa alipohutubia pale Jangwani aliitaja CHADEMA ama UKAWA? Magufuli amekuwa mtiifu kwa CCM siku zote. Huwezi kuanzisha propaganda za kipuuzi wakati huu
 
Kupiga kura sio kujaza nafasi inayoachwa wazi, bali wanachagua mtu wa kufanya kazi kwa miaka mitano inayokuja. Anamshangaa Sumaye kwa kuthibitisha tetesi kuwa Lowassa ni mgonjwa, badala ya kukanusha!

Kikwete hakufanya siri ugonjwa wake, tena ametibiwa katika mwaka wa kumi wa utawala wake! Anashangazwa na maneno kuwa 'Ikulu hatuendi kubeba zege'! Rasi ni kiongozi, sio meneja!

Rais wa Tanzania sio nembo, bali ni mtu anayetakiwa kuongoza na kusimamia! Lazima tuoanishe aina ya mtu tunayemtuma na matatizo yetu. Mgombea wa CCM amezunguka mwenyewe mikoa kadhaa ya Tanzania akiomba kura yeye mwenyewe, hilo linafanya tumuamini!

Tusinunue kila kile tunacholetewa, kuleta mabasi kutoka kote kuja kushuhudia hotuba ya dakika kumi! Kuwaambia masikini wakaangalie hotuba kwenye website, hiyo ni dalili ya mtu kuchoka! Lowassa amechoka kiafya na kifikra.

Baraza la Mawaziri halitaki mtu aliyechoka, alishawahi kusahau hata jina la mke wake kwenye hotuba!

Wapiga dili wote wanaambatana na Lowassa, wakishamuanika juani wao wakapige dili. Lowassa ni mpiga dili tangu akiwa Shule ya Sekondari!

Sumaye anasema kuwa ufisadi umeendelea hata baada ya Lowassa kutoka madarakani, hafahamu kila siku wanazaliwa Watanzania wema na wabaya. Hatuwezi kuchagua fisadi papa eti kwa kuwa tu ufisadi upo nchi hii.

WanaCCM wanawafahamu wagombea wote, wapinzani wamewapokea watu ambao hawawafahamu! Magufuli ana rekodi ya uadilifu tangu akiwa naibu waziri.

CCM sio kwamba haijui kuwa kuna mafisadi, vyombo vya chama viliangalia mtu anayefaa kwa nafasi ya urais. Licha ya umaarufu wake, Lowassa ana sifa ya kuwa mpiga dili! Hata kwenda CHADEMA na kupata nafasi ya kugombea urais ni dili.

Mungu anatuacha tuishi kwa kuwa anaamini ipo siku tutabadilika, pengine Kikwete alikuwa na uhakika kuwa Lowassa atabadilika, miaka miwili tu akapiga dili!

Kilichowapatanisha CHADEMA na Lowassa sio shida za watanzania, bali ni maslahi yanayofanana! Anauliza kama leo Lowassa angekuwa mgombea wa CCM wapinzani wangetoa kauli gani?

Wanatumia pesa nyngi kuhakikisha wanamweka madarakani, shida yao sio matatizo ya Watanzania! Wanajua pesa waliyotumia itarudi!

Sumaye alipora viwanja Morogoro, na kusababisha mtafaruku mkubwa. Leo hii anadiriki kuwahadaa watanzania!
 
Makufuli atuambie kwanini ameshindwa kulipa wakandarasi wa barabara, pia atuambie kwanini ameitia Hasara serikali kwa limbikizo la riba ya wakandarasi kifisadi, aje pia atueleze nyumba zetu za serikali kwanini aliziuza kwa bei poa, atoke mbele aleze pia kwanini awauzie ndugu zake tena ambao hawapo serikalini je huyu akichukua Ikilu itakuaje tuome ajibu hoja hii kabla hatujamuuliza maswali mengine
 
Kwanini Lowassa amegoma kuvaa gwanda wala neno ufisadi haliwezi kusikika mdomonimwake ?
 
Pole sana Mkuu. Kwani Lowasa alipohutubia pale Jangwani aliitaja CHADEMA ama UKAWA? Magufuli amekuwa mtiifu kwa CCM siku zote. Huwezi kuanzisha propaganda za kipuuzi wakati huu
Lizabon umebaki mwenyewe tu hata Musa allani analijua hilo
 
Last edited by a moderator:
Makufuli atuambie kwanini ameshindwa kulipa wakandarasi wa barabara, pia atuambie kwanini ameitia Hasara serikali kwa limbikizo la riba ya wakandarasi kifisadi, aje pia atueleze nyumba zetu za serikali kwanini aliziuza kwa bei poa, atoke mbele aleze pia kwanini awauzie ndugu zake tena ambao hawapo serikalini je huyu akichukua Ikilu itakuaje tuome ajibu hoja hii kabla hatujamuuliza maswali mengine
 
wanaukumbi

nimefuatilia hotuba ya umimi ya magufuli toka viwanja vya majimaji songea nikabaini kuwa hakuitaja ccm hata mara moja.

Badala yake utasikia songea hoyeee..mimi magufuli...mniamini,mimi magufuli najua kazi...mimi..magufuli nataka..ukawa wanadanganya mimi ntawatumikia..

Je kuna ugombea binafsi hapo?

Mgombea kuweka umimi yaonekana katumwa,baada ya hapo watamremot sana tu..nadhani ifike sehemu wagombea tuwapime kwa uongozi shirikishi..
Sio mimi nilifanya nikiwa wapi kwa hiyo naweza.

Yajionyesha tutampata kiongozi wa kutekeleza mawazo yake hata akiamka asubuhi bila kushirikiana na wananchi waliomchagua.

Kusema sana,kujua kilomita za barabara sio uongozi..kichwa kinatakiwa kitulie.

Tahadhari.

acha utoto wewe, kila siku magufuli husema kidumu chama cha mapinduzi,
 
Back
Top Bottom