Hilo mkuu hata yeye mwenyewe analijua kuwa Watanzania wanamkubali ila Chama chake kiukweli watu wamekichoka. Na ndiyo maana anatumia mfano wa China. Unajua hana namna ila ingekuwa uwezo wake angebadili hata jina la Chama kutoka jina CCM na kuita jina jingine angalau watu wangemfuata huko. Ile tone CCM watu ndo wameichoka, na hapo namuonea huruma, kama akishinda atakuwa ametumia calories/energy/msuli mkubwa jambo ambalo kwa kukubalika kwake haikupaswa iwe hivyo.
Mfumo aliomo ndo tatizo, Dr yeye binafsi anakubalika, chama chake watu ndo wamekichoka. Kama wakivuka salama mwaka huu itabidi jina la chama hata rangi wabadili ili angalau kuwasahaulisha wananchi, huu ni ushauri wa bure kwa CCM, badili sera, mitazamo, mavazi, mfumo na kila kitu ili wananchi wawakubali, hali ilivyo kwa sasa wananchi jina limewakinai na huo ndiyo ukweli, only for those who think broadly and globally can undetstand this fact!