Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Huyu Magufuli kweli hafai hata kuwa mwenyekiti wa Kitongoji kila sehemu anako zunguka ana zungumzia shida za wananchi na kujifanya kuwa na huruma nao,halafu hao hao anaojifanya kuwa ana huruma nao ndio anaosema waende China wakajifunze,sijui China watakwenda kwa miguu.

Kwa kuwa wanaosema kuwa hatafanya kitu ndio haohao anaojifanya kuwahurumia na wengi wao wanashindwa hata nauli ya kuwafikisha DSM.
 
MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli, amewataka wanaosema kuwa hataweza kuleta mabadiliko kwa kuwa yuko ndani ya mfumo wa chama hicho, wakajifunze China.

Akizungumza katika mikutano, Dk Magufuli alisema China imefanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi, kiteknolojia na kijamii, kwa kutumia chama cha Kikomunisti chenye mfumo wa kijamaa kama CCM.

Kwa mujibu wa Dk Magufuli, walichofanya katika nchi hiyo ni kutumia watu wa ndani ya chama hicho cha Kikomunisti, kuleta mabadiliko yanayoonekana dunia nzima leo mpaka Marekani imeshangazwa.

“Nchi ya China ilikuwa chini ya Chama cha Kikomunisti chini ya Mwenyekiti Mao, walipopata uzoefu wakafanya mabadiliko bila kuondoa chama kilichokuwepo madarakani,” alisema.

Dk Magufuli pia aliwaonya Watanzania kuwa uongozi wa nchi haujaribiwi na hata yeye alipochukua fomu za kuwania urais, alijua kuwa haombi urais kwa ajili ya majaribio, ndio maana alichukua fomu na kutafuta wadhamini kimya kimya, huku akimtanguliza Mungu mbele.

Aliwahadharisha Watanzania uwezekano wa kutokea watu watakaowapa fedha, ili wawachague na kuwataka wawaepuke kwa kuwa watakuwa na deni watakalotakiwa kulipa huko walikotoa fedha.

Alisema yeye deni lake ni kutumikia Watanzania wote bila kujali vyama vyao, lakini si deni la fedha kwa watu wenye fedha kwa kuwa hatoi fedha mahali popote ya kuomba kuchaguliwa.

02.JPG

01.JPG

Magufuli akielekea uwanjani ili kujinadi katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya Ruanda Nzonve, Mbeya
03.JPG

Magufuli akiwa na watoto ambao walikuwa na hamu ya kutaka kumsalimia kwa kumpa mikono.
07.JPG

Magufuli akijinadi kwa wananchi katika mkutano
_MG_8166.jpg

Wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mgombea Urais kwa Tiketi ya CCM, John Magufuli

JPM

Yeye alienda lini China kujifunza Ukomunist? Unaona kabisa kakosa la kuongea! China na Tanzania wapi na wapi. China kila kitu ni mali ya umma. Kule makaz mengi ni nyumba za serikali, kule mfumo wa utawala ni majimbo, yeye alijifunza lini utawala wa majimbo?

Kule adhab za maximum penalt ni kawaida, yeye anaweza hayo?! China hatuendi, yeye tunamkubali mfumo wake tunasema ni BIG NO!
 
Huyu Magufuli kweli hafai hata kuwa mwenyekiti wa Kitongoji kila sehemu anako zunguka ana zungumzia shida za wananchi na kujifanya kuwa na huruma nao,halafu hao hao anaojifanya kuwa ana huruma nao ndio anaosema waende China wakajifunze,sijui China watakwenda kwa miguu.

Kwa kuwa wanaosema kuwa hatafanya kitu ndio haohao anaojifanya kuwahurumia na wengi wao wanashindwa hata nauli ya kuwafikisha DSM.

usiwe na akili ya kukariri katolea mfano tu na amejibu hoja zenu za mfumo.
 
wadau kesho magufuli wapi??? muwe mnatu-updates safari zake jamani
 
Ili wanaJF wafungue hii thread lazima heading isomeke kinyume! Kweli CCM imefika pabaya!

UMEME HAKUNA, MAJI HAKUNA, HUDUMA ZA AFYA HAKUNA, MIUNDOMBINU HAKUNA, halafu wanataka tuwape kura tena! OVER MY DEAD BODY..........!!!!!!!!!!!!!!!!!

CCM imeshachoka, ipumzike kwa Amani! HAKUNA NAMNA TENA!!!!!!!
 
Magufuli akifananisha na China ajue kama ukomunisit wa china ungekua hapa Tanzania ajue angekua keshahukumiwa kifo kwa kuuza nyumba za selikari na kununua vivuko vibovu angekua duniani tumesha msahau . kwahiyo hatudanganyiki kitu.
 
Back
Top Bottom