Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

Special Thread: Taarifa za Kampeni za Mgombea urais kupitia CCM, Dr. Pombe Magufuli na Samiah Suluhu

kimsingi lizaboni , ukumbuke hakuna mgombea binafsi sheria inatamka mgombea kubebwa na chama.hapa twende mbele serikali hii kule Ruvuma imekopa watu mahindi na mengine wakatakataa kuyanunua kutaja ccm maanake ni kaa la moto.

Lowasa mabadiliko, mabadiliko Lowasa, au siyo "kupelwa"!
 
Magufuli anazo tabia hizo za kutaka kutukuzwa. Popote anapopita haachi mfumo unaojiendesha,ni yeye tu. Nitampa kura yangu,lakini tunayo kazi huko mbele. Duu!! Nasikia amempa hawara yake nyumba ya serikali. Ni hatari, sijui mshauri wake wa ubavuni ni nani. Nadhani ndo maana hakutaka kumtambulisha mke wake siku ya ufunguzi wa kampeni,hadi JK akamshtua
 
Acheni ushabiki jadilini kwa hoja, suala hili ni zaidi ya Usimba na Uyanga au Manchester na Liverpool ni kuhusu mustabakali wa taifa letu mama Tanzania. Watu tunakosa umeme zaidi ya masaa 24 kwa nchi masikini kama Tanzania ni hatali kwa taifa letu na wananchi wetu imagine mchomea magrill anakosa nini yeti mnaleta ushabiki. Tujipime wakuu.
 
Jesca yupo on fair kule kwa wanyiramba wenzeka..

Mwache aendelee kuwatia hasira vijana wa kitanzania

Amemtukana baba yetu.....sasa asubir october 25
 
Watanzania wamechoka na maneno ya wana ccm kilichobaki ni kuwaondoa tu, tujitahdi kutunza vitambulisho vyetu october 25 maneno yetu yakawe matendo
 
Kwa kweli hakuna namna Lowasa tutamuingiza hivyo hivyo ikulu, hatutajali afya mgogoro wala upgaji dili aliofanya.
 
Kitandachako kikiwa na kunguni wawili....huchomi godoro...wauwe alafu endelea kuuchapa usingizi...ccm.imeshauwa mafisadi
 
Kupiga kura sio kujaza nafasi inayoachwa wazi, bali wanachagua mtu wa kufanya kazi kwa miaka mitano inayokuja. Anamshangaa Sumaye kwa kuthibitisha tetesi kuwa Lowassa ni mgonjwa, badala ya kukanusha!

Kikwete hakufanya siri ugonjwa wake, tena ametibiwa katika mwaka wa kumi wa utawala wake! Anashangazwa na maneno kuwa 'Ikulu hatuendi kubeba zege'! Rasi ni kiongozi, sio meneja!

Rais wa Tanzania sio nembo, bali ni mtu anayetakiwa kuongoza na kusimamia! Lazima tuoanishe aina ya mtu tunayemtuma na matatizo yetu. Mgombea wa CCM amezunguka mwenyewe mikoa kadhaa ya Tanzania akiomba kura yeye mwenyewe, hilo linafanya tumuamini!

Tusinunue kila kile tunacholetewa, kuleta mabasi kutoka kote kuja kushuhudia hotuba ya dakika kumi! Kuwaambia masikini wakaangalie hotuba kwenye website, hiyo ni dalili ya mtu kuchoka! Lowassa amechoka kiafya na kifikra.

Baraza la Mawaziri halitaki mtu aliyechoka, alishawahi kusahau hata jina la mke wake kwenye hotuba!

Wapiga dili wote wanaambatana na Lowassa, wakishamuanika juani wao wakapige dili. Lowassa ni mpiga dili tangu akiwa Shule ya Sekondari!

Sumaye anasema kuwa ufisadi umeendelea hata baada ya Lowassa kutoka madarakani, hafahamu kila siku wanazaliwa Watanzania wema na wabaya. Hatuwezi kuchagua fisadi papa eti kwa kuwa tu ufisadi upo nchi hii.

WanaCCM wanawafahamu wagombea wote, wapinzani wamewapokea watu ambao hawawafahamu! Magufuli ana rekodi ya uadilifu tangu akiwa naibu waziri.

CCM sio kwamba haijui kuwa kuna mafisadi, vyombo vya chama viliangalia mtu anayefaa kwa nafasi ya urais. Licha ya umaarufu wake, Lowassa ana sifa ya kuwa mpiga dili! Hata kwenda CHADEMA na kupata nafasi ya kugombea urais ni dili.

Mungu anatuacha tuishi kwa kuwa anaamini ipo siku tutabadilika, pengine Kikwete alikuwa na uhakika kuwa Lowassa atabadilika, miaka miwili tu akapiga dili!

Kilichowapatanisha CHADEMA na Lowassa sio shida za watanzania, bali ni maslahi yanayofanana! Anauliza kama leo Lowassa angekuwa mgombea wa CCM wapinzani wangetoa kauli gani?

Wanatumia pesa nyngi kuhakikisha wanamweka madarakani, shida yao sio matatizo ya Watanzania! Wanajua pesa waliyotumia itarudi!

Sumaye alipora viwanja Morogoro, na kusababisha mtafaruku mkubwa. Leo hii anadiriki kuwahadaa watanzania!

Kwenye hao wapiga deal sijamuona Chenge..tibaijuka ..ngeleja sijamuona ridhiwani wala kikwete maana hawa ni wapiga deal maarufu na watz wote
 
Kwa tahmini na muonekano wa kisiasa ccm inapumulia gas maana kuna mambo mengi mno hayajajibiwa mfano kwann wakaazi wa dar hawaruhusiwi kwenda feri na daladala moja mpka uende na uda pekee?hizi ni kero moja wapo ;kila mahala watu wanalalamika kero kero , ghiriba, hila.sasa kama chama cha siasa ccm inajitapa na kujigamba kushinda kwa kutumia doala kama usalama wa taifa kama wasimimazi wa tume ya uchaguzi , ndo hilo pekee lakini kana hoja na namna ya kuondoa kero halipo.
 
CCM wamejikataa wanatamani wabadili hadi jina. Nembo yao wameitelekeza haitumiki kwenye kampeni za urais.
 
Issue sio magufuli ni Ccm magufuli angehamia ccj tungempa kura ..miaka hamsini unajivunia kujenga shule zisizo na vyoo wala walimu..hospital zisizo na dawa.. khaa ccm haijafikia malengo ya wananchi.. mnataka miaka mingapi muweke dawa mahospitalin barabara hata tungewaachia wakoloni wangekuwa weshamaliza kote lami kama south africa
 
Kwanini aitaje CCM wakati ana kazi ya kunadi sera, ama CCM imegeuka sera? mnakuwa vipofu hata kwnye mambo madogo kiasi hiki nyinyi malofa? Hapa kazi tu na kumwaga sera ndo kampeni yenyewe, vyama mpelekee msajiri wa vyama ndo anashughurika na vyama na magufuri anakazi ya kuelezea sera tu, za chama gani? kila mtanzania anaelewa
 
Magufuli haoneshi kwamba CCM haijafanya kitu hapo awali, ila anaonesha sehemu ambazo zinahitaji kushughulikiwa. Marekani ina zaidi ya marais 40 lakini kila anayekuja anatangaza sera mpya, ina maana kuwa Marais wa Marekani waliopita hawakufanya kitu chochote? la hasha bali hakuna uongozi unaoweza kufanya kila kitu na utambue kuwa mahitaji ya wanadamu hayaishi kamwe.

Magufuli ni mgombea mzuri na anafaa zaidi kuiongoza Tanzania kuliko mgombea mwingine yeyote; tumchague kwa maendeleo ya Taifa letu
#hapakazitu
Sasa kwani Tanzania ni Marekani?pumba tu hizi.


Swissme
 
Back
Top Bottom