Special Thread: Tujikumbushe matukio ya zamani ya wasanii wa Bongo Fleva

silent Inn ilikua bado.....?
 
Hivi wale vijana wa University Corner waliishia wapi, waliwakalisha sana na tshirt na jeans. Ali Choki aliingia na kijiko ktk uzinduzi sikumbuki wa albam gani vile. Pia Twanga pepeta ndio bendi ya kwanza kurekodi kwa mfumo wa kisasa wa maeneo toauti tofauti, East African melody nao wakaanza staili mpya ya kurekodi video kuachana na zile za kukaa na kunesa nesa vichwa kuna ngoma fisadi kiwembe inanikosha sana. Hapo nimetoka nje kidogo ya mada. Sasa kuna Binti alikuwa anaitwa Jack Maria nadhani alitoa nyimbo moja ilibamba sana Itv2, Sugu alipotka Mbeya alifikia Mbagala kabla ya kuhamia Kinondoni. Mr Blue aliacha Shule akiwa form two pale Kidongo Chekundu
 
Album Kali ya The late Albert Mangwair iliyojulikana kwa jina la a.k.a Mimi chini ya producer mkali P funk majani.
one of the best bongo fleva album...nakumbuka nilikuaga natoka likizo miaka hiyo mambo ya boarding school...kufika shy town mtu mzima mmoja akiwa na prado akaamua kutusogeza rock city sasa njia nzima kaweka hiyo cassette ya aka Mimi inaisha inajirudia...akasema naona siku hizi vijana mnaimba nyimbo za akili na ujumbe kumbe hizo rap rap zenu ukisiklza vizuri ni nzuri....
 
Kipindi hicho ktk outro wasanii walikuwa wanataja majina si chini ya 20
 
Sir Kibla Nature Kassim Kiroboto alishinda tuzo ya channel O
na lile Goma lake la mgambo wanaruka na kukanyaga.....enzi hizo team hakuna sijui [HASHTAG]#teamkiba[/HASHTAG] [HASHTAG]#teamdai[/HASHTAG].....hapo ilikuaga East Cost vs Temeke hakuna kuremba
 
Kuna mwingine alivaa tshirt ya Von Dutch kila kona von dutch zikauzwa kama karanga
 
Ray C kupigana na Kajala kisa P funk, jamaa alimuacha Ray c akahamia kwa Kajala, Dataz na Joha wimbo wao mume wa mtu ni hatari uliwapa shavu sana, mwanamuziki wa dansi Muumini mwinjuma kwenda kuoa kwao bagamoyo ndoa haikudumu hata mwezi akamuacha mke kisa eti mke mshamba, Bifu la Vicky Kamata na mrehemu Amina chifupa kisa marehemu Med mpaka Njia, Amina akimtuhumu Vicky kuingilia ndoa yake na Vicky akidai mpakanjia ni meneja wake tu kwenye bongo fleva, Juma Nature kubadili jina la wachawi na kuanza kuitwa mzee wa busara, baada ya kutoa ngoma akimtuhumu mzee wa busara kwenye masuala ya ulozi.
 
Unakumbuka na suruali kubwa walizokuwa wanafavaa,ingekuwa sasaiv sidhani Kama wangekubali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…