Special Thread: Tujikumbushe matukio ya zamani ya wasanii wa Bongo Fleva

Special Thread: Tujikumbushe matukio ya zamani ya wasanii wa Bongo Fleva

DAR YA KIPINDI KILE MKUU ILIKUWA NI DAR KWELI KWELI
MIMI NILIANZA KUPANGA CHUMBA KODI NALIPA ELFU 2,

ASUBUHI CHAI ILIKUWA INAUZWA SH.50 NA VITUMBUA SH.10.

2.MCHANA UBWABWA MAHARAGE BEI 500 UKITAKA CHIPS YAI 700 NA SODA 200._

3.USIKU HIVO HIVO KAA MCHANA

4.SIKU ZA WEEKEND CLUB ILIKUWA BILICANAS , MAMBO CLUB, FM CLUB HII ILIKUWA KINONDONI KIINGILIO ILIKUWA 500 NA UKIINGIA BIA ILIKUWA 500 TENA ILIKUWA NI SAFALI LAKINI KULIKUWA NA BIA KAMA BIGWA, THE KICK BEI MPAKA 300.

HAYA NDO MAISHA DAR MIAKA YA TISINI KUJA ELFU MBILI
silent Inn ilikua bado.....?
 
Hivi wale vijana wa University Corner waliishia wapi, waliwakalisha sana na tshirt na jeans. Ali Choki aliingia na kijiko ktk uzinduzi sikumbuki wa albam gani vile. Pia Twanga pepeta ndio bendi ya kwanza kurekodi kwa mfumo wa kisasa wa maeneo toauti tofauti, East African melody nao wakaanza staili mpya ya kurekodi video kuachana na zile za kukaa na kunesa nesa vichwa kuna ngoma fisadi kiwembe inanikosha sana. Hapo nimetoka nje kidogo ya mada. Sasa kuna Binti alikuwa anaitwa Jack Maria nadhani alitoa nyimbo moja ilibamba sana Itv2, Sugu alipotka Mbeya alifikia Mbagala kabla ya kuhamia Kinondoni. Mr Blue aliacha Shule akiwa form two pale Kidongo Chekundu
 
Album Kali ya The late Albert Mangwair iliyojulikana kwa jina la a.k.a Mimi chini ya producer mkali P funk majani.
one of the best bongo fleva album...nakumbuka nilikuaga natoka likizo miaka hiyo mambo ya boarding school...kufika shy town mtu mzima mmoja akiwa na prado akaamua kutusogeza rock city sasa njia nzima kaweka hiyo cassette ya aka Mimi inaisha inajirudia...akasema naona siku hizi vijana mnaimba nyimbo za akili na ujumbe kumbe hizo rap rap zenu ukisiklza vizuri ni nzuri....
 
Kipindi hicho ktk outro wasanii walikuwa wanataja majina si chini ya 20
 
Sir Kibla Nature Kassim Kiroboto alishinda tuzo ya channel O
na lile Goma lake la mgambo wanaruka na kukanyaga.....enzi hizo team hakuna sijui [HASHTAG]#teamkiba[/HASHTAG] [HASHTAG]#teamdai[/HASHTAG].....hapo ilikuaga East Cost vs Temeke hakuna kuremba
 
Kuna mwingine alivaa tshirt ya Von Dutch kila kona von dutch zikauzwa kama karanga
 
Ray C kupigana na Kajala kisa P funk, jamaa alimuacha Ray c akahamia kwa Kajala, Dataz na Joha wimbo wao mume wa mtu ni hatari uliwapa shavu sana, mwanamuziki wa dansi Muumini mwinjuma kwenda kuoa kwao bagamoyo ndoa haikudumu hata mwezi akamuacha mke kisa eti mke mshamba, Bifu la Vicky Kamata na mrehemu Amina chifupa kisa marehemu Med mpaka Njia, Amina akimtuhumu Vicky kuingilia ndoa yake na Vicky akidai mpakanjia ni meneja wake tu kwenye bongo fleva, Juma Nature kubadili jina la wachawi na kuanza kuitwa mzee wa busara, baada ya kutoa ngoma akimtuhumu mzee wa busara kwenye masuala ya ulozi.
 
King Crazy GK kuna kikofia cha matobomatobo alikuwa anapendelea kukivaa basi nakumbuka wakati huo nipo sekondari ikageuka kuwa fasheni kwa vijana, 'kikofia cha GK'. Na pia kundi la ECT liliwashika sana vijana miaka kama ya 2002-2004, ikatokea vijana sehemu mbalimbali hasa mashuleni wakiunda vikundi na kujiita East Coast, huku wakitumia majina ya members maarufu kama GK, AY na Mwanafalsafa. Mfano ni shule yetu, kulikuwa na kikundi cha namna hiyo, East Coast baadae walikuja kufunikwa na TMK Wanaume baada ya ujio wao wa ngoma kama NYUMBANI NI NYUMBANI wakitumia style ya kucheza iliyobamba sana miaka ya 2004-2005 (Mapanga Shaaa), huku ikiwa na members maarufu kama Juma Nature, Temba, Chege, KR Mullar, Dollo, Luteni Kalama, YP & Y'DASH, Mabaga Fresh, etc. Hiyo style ya mapanga ilishika ile mbaya kwenye clubs/madisco, ikipigwa ngoma ya NYUMBANI ni NYUMBANI mademu wanakaa pembeni, tunabaki washkaji tumejipanga line tunapiga mapanga huku tukichombezwa na slogan ya (WANAUMEE.....EEEHHH).
Na kutokana na kukubalika sana kwa kundi hili ilipelekea kutumika sana kwenye kampeni za uchaguzi wa mwaka 2005 huku wakizunguka sehemu mbalimbali za nchi na mgombea wa wakati huo wa CCM Jakaya Kikwete.
Unakumbuka na suruali kubwa walizokuwa wanafavaa,ingekuwa sasaiv sidhani Kama wangekubali
 
Back
Top Bottom