Special Thread: Tujikumbushe matukio ya zamani ya wasanii wa Bongo Fleva

Special Thread: Tujikumbushe matukio ya zamani ya wasanii wa Bongo Fleva

Yeah aisee lile kundi lao alikuwepo Steve k alikuwepo john mjema na spider man ,

Lakini mwisho wa Sikh Steve 2k aliuwawa alichomwaga kisuu alikuwa ugomvi yeye na meneja wakee badae john mjema nae alijiuwaa kwa kujichoma kisu kichwanii hili lilikuwa tukio LA kusisimuaaa bila kusahahauu.

Father g yule wa arusha yeye pia alichomwaga kisu akafaa kama unamfahamu alitoaga wimbo hii ni dhambi kwa mwenyezii ukienda YouTube utaukutaa.

Halafu ivi wimbo wa Mimi sio mwizi wa alikuwepo john mjema ivi naweza kuupata wapi
Aliyemuua steve 2k ni producer wake anaitwa Castro Ponela, alitoka kwa msamaha wa rais mwaka juzi kama sikosei.
Huyo wa Arusha ni Father Nelly mzee wa ushanta na nini dhambi kwa mwenye dhiki.
 
Kweli nimezeeka. Kuna vijana wawili walikuwa wakisoma mlimani huku wakifanya muziki. Mmoja alikuwa Engineering akadico alikuwa akitamba na wimbo unaitwa Acquilina. Mwingine aliimba wimbo uliovuma sana "...bure mtakunywa sumu..." aliimba na Stara Thomas. Huyu aliokoka akaacha muziki.
Ehhh K basil...
 
Ilaa daa AFANDE SELE sijui alikuwa ana nini mshikaji maana kuna time alianza kuwa na bifuu

1.nasikia alikuwa na bifuu na PROFESA j hadi kupelekea PROFESA asisusiee ile shooting ya wimbo wa mtazamo.

2.bifuu badae akawa yeye na yule dogo ditoo hadi dogo ditoo akajitoa kundi LA watu pori .

3.bifuu LA yeye na o ten

4.bifuu LA yeye na madee

5.bifuu LA yeye na ney wa mitego

Badae akaingia katika siasa akiwa chadema badae akajiunga ACT.

ILA MZEE afande nae katoka mbali sanaa kuna story pia niliwahi kusikia kabla ya kuwa mwanamuzki alikuwa msaidizi wa sugu kimuziki yaani sugu alikuwa anamtuma Fanya hivi Fanya vilee
Alishakuwa mwanajeshi pia alifukuzwa
 
Unique sistaz walikuwa wanazindua albam yao pale Pool Side, Kilimanjaro Hotel. Mshereheshaji alikuwa Solo Thang, wasanii waalikwa kibao hadi Jay Dee ndani, kipindi hiyo ana single mbili tu. Inspekta Haroun ndio alikuwa anafunika na Mtoto wa geti kali, wahuni wakamshangilia wakambeba juu juu alivyoshushwa watu wamelamba kila kitu akaanza kupiga kelele, simu yanguuu! Ukiuliza simu yenyewe ni Ericsson. Show ya mwisho akapanda Juma Nature, jamaa kaanza kunywa gongo zamani... Juma Nature akapanda stage na P Funk, kipindi hiyo watu hawamjui ndio nani. Wakati Nature anaimba P Funk akaanza kurusha hela hewani ikawa story mpaka tunaenda Bills tunasema yule jamaa, hata jina lake hatumjui. Pale Billicanas P Funk alikuwa anapanga foleni kama watu wa kawaida tu. Dah, miaka ile mi nilikuwa nakesha kama popo, events zote nipo.
Hahahhahah umenikumbusha kuna wajinga walikwapua barua iliyokua inasomwa kwenye nyimbo ya barua ya daz nundaz pale kwenye shoo diamond
 
Hiyo ilitisha sana halafu hayo mabifu yanilinogesha sana mziki enzi hizo Eti siku hizi bifu ni insta pekee ake daaaa nazitamani hizo Enzi
Ahhhh kweli bhana.. mi nilikua team east coast... shoo ikiwa diamond mpeto... cku ikihamia temeke kina gk wanahenya hatari..!!!
 
Hahahhahah umenikumbusha kuna wajinga walikwapua barua iliyokua inasomwa kwenye nyimbo ya barua ya daz nundaz pale kwenye shoo diamond


Daz Nundaz enzi zao walikuwa wakipanda stage wanatisha! Nilikuwa nawakubali sana kwenye show tena kipindi hiyo walikuwa machalii tu. Kweli ngada noma.
 
kwenye mkali wa rymes nakumbuka inspector harun aliingia kavaa yeboyebo na ajisifia ile mbaya eti mkali wa pamba, kipindi hicho yebo ndo yebo kweli bila 15000 huchukui!
[emoji15] [emoji15] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Salama Jabir kutekwa na Kikosi cha Mizinga na kunyolewa nywele zote.

Crazy GK alipanda na gwanda za jeshi kuzindua albamu yake, aliposhuka jukwaani tu akadakwa na Wajeda wakampeleka Ngome.

Kalapina kupeleka posa ya kutaka kumuoa Mr Blue na Voice Wonder.

Rais Ben Mkapa kumpa gari msanii Feruz kwa wimbo wake wa Starehe kutokana na ujumbe mzito ndani ya wimbo huo.

Bifu la Master Jay na P funk Majani hadi wakakutana kwenue msiba wa Steve 2k wakachuniana.

Kwaleo niishie hapo...nitarudi
uko vzr wewee...mzee mwenzangu
 
Hilo shindano lilifanyikaga diamond jubilee kiingilio ilikuwa buku mbili ila mwisho wa shindano ngoma walitoka droo ila yote Tisa kumi shindano LA kumtafuta mfalme wa rymes sijui ni wangapi wanaokumbuka
Alishinda Afande Select
 
Hahahshs tena akasema live kwenye redio mi cjaliwa kiboga wanaipakazia.... nadhani ndo akatoa ule wimbo wa hunifahamu
hunifahamu aliutoa baada ya skendo ya demu,kama siyo Dodoma basi Moro
alikopa hakulipa dully akawa anapiga chenga
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ahhhh kweli bhana.. mi nilikua team east coast... shoo ikiwa diamond mpeto... cku ikihamia temeke kina gk wanahenya hatari..!!!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] acha tu yaani kuna siku TPA walipopolewa pale acha kabisa
 
Back
Top Bottom