Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi
Frontline wa Ukraine wakifika Uwanja wa Mapambano
Hizi ni HIMARS nne zilishambulia Warusi walipo. Tuliwapa mtego wao wakawa wanajua HIMARS zinatumika usiku tu sababu zina uwezo wa kuona Adui alipo hata kama ni giza totoro. Sasa hajaami walivyoshambuliwa M142 HIMARS kwa kutumia M31A1 GMLRS. Kirefu cha GMLRS ni Guided Multiple Launch Rocket System.
Jeshi la anga la Ukraine bado linafanya kazi kama kawaida. Urusi walijaribu kuharibu mifumo ya anga, ila sasa kila kitu kipo poa. Hizi picha zimetumwa na kikosi cha anga cha Ukraine cha 831st Tactical Aviation Brigade kikiwa airbase ya Myrhorod Mkoani Poltava
Ndege za Ukraine zinazoonekana hapa ni Su-27/S1M na MiG-29/MU1 fighter aircraft zikiwa na Makombora ya R-27R na R-73 AAMs. Hii R-73 wenyewe ndo wanaita short-range air-to-air missile
Hii ndo R-27R na 73 ya air to air missile
Hapa ni Poland, mzigo ukiwa tayari kuletwa Ukraine. Hizi ni MLS SHIELD 4×4 za Italia
Hili gari la Urusi sijui lilibeba nini. Linalipuka tu
Hapa Ukraine wameharibu UR-77 Meterorit mine clearing vehicle ya Urusi. Tukipata picha ya karibu tutapost
Kifaru cha Urusi aina ya BTR-82A APC, kilikamatwa na Ukraine. Hapa kinapelekwa gereji kikitoka kitaanza kuwawinda Warusi
BTR-82A APC yenyewe ndo hii
Mwezi ulopita, Urusi walifanikiwa kukamata Ukraine kwa 30% wamefukuzwa kinyama, sasa wanashikilia 20 ya Ukraine. Mwezi ujua wanaweza bakiwa na 5%. Lengo la Urisi ni kuiteka Ukraine 100%. Wameshindwa fika malengo yako kwa miezi 3. Ukitaka kujua Warusi hawajielewi, February walisema wanaiteka Ukraine ndani ya siku tatu. Na baada ya siku 15 wanabadilisha Uongozi kwani walidai ni Operation maalum. Sasa wanajuta. Wamebaki uchi kwani dunia ilijua Urusi ina nguvu kumbe ni Mandonga tu
Kifaru cha Urusi aina ya BMP-3 IFV, kikiharibiwa na Drone ya Ukraine
Yaani Udhaifu wa Urusi ulianza kujulikana ilipozamishwa hii meli walodai ina uwezo wa kuzuia makombora. Yaani ukituma kombora, linalipuliwa kabla haijafika. Baada ya kuzamishwa Urusi inawauma hadi leo, meli nyingine kubwa za kijeshi iliwalazimu wazirudishe Urusi
Angalia Azov alivyo lipua kifaru cha Urusi aina ya BMP IFV kwa kutumia FGM-148 Javelin
Huko Antonovsky daraja la treni Mto Dnieper limekwenda na mani Mkoani Kherson.. Urusi kazi wanayo..
Huko Donetsk, ghala la mafuta la Urusi limekwenda na maji. Vifaru vyao vitatumia nini?
Kikosi hatari cha Ukraine kinachotumia drone cha 93rd Brigade wanauwezo wa kubadilisha hizi drone za kawaida za kwenye Maharusi kufanya kazi kama kamikaze. Ila zinabeba makombora madogo yakuharibu vifaru kama vya kubebea wanajeshi na Majeruhi.
Hiki ni Kikosi cha Azov cha 98th Battalion wakiwa wanatumia SPG-9M. Ukiangalia hapo chini pia kuna PG-9V HEAT-FS na OG-9V FRAG-HE projectiles
Urusi wanaingiza vifaru vingine kupitia daraja la Crimea. Vilivyoletwa mara ya kwanza vyote vimeteketea.. Hadi waishiwe
Azov wetu. Huyu ni Mwanajeshi wa kujitolea, kaja kuisaidia Ukraine kujikomboa kutoka kwa Wakoloni Wavamizi orcs