OSEFUKANY
JF-Expert Member
- Jan 16, 2011
- 2,437
- 3,896
Ni kweli kwamba kwa Mapito anayopitia Mrusi kwa sasa, nchi nyingine zilizodhulumiwa ardhi yao sasa watahamasika kwa yanayojitokeza kwenye hii vita baina ya Mrussi na Ukraine na wao watasimama na kudai ardhi yao iliyopokonywa kiubabe kutoka kwa Mrussi.Akiendelea na kiburi atasababisha wanajeshi wake wengi kuuwawa. Mizoga tunayoshuhudia ilitosha kumfanya ajitafakari upya.
Niliwahi kusema kuwa ni Bora angesingizia kuwa operation aliyopanga imekamilika na akaondoa majeshi yake. angepata aibu kuliko fedheha anayopata sasa hivi.
Siku Crimea ikirudi Ukraine, Georgia nao watataka kuyakomboa majimbo yao waliyonyang'anywa na Putin kwa ubabe. Time will tell.
Mrussi kwa sasa ni mchovu na atachoka sana kwani atageuzwa kuwa kichwa cha mwenda wazimu mahali pa kujifunzia kunyoa.