Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Wananchi wa Georgia waaandamana mpakani mwa Georgia na Russia wakiwananga Warusi wanaokimbia kupelekewa Ukraine. Wanawaambia Vita ilipoanza mlikuwa mkishangilia na kuingua Mkono Nchi yenu, leo mnaenda wapi?

Huyo Mjojia alojifunika Bendera ya Ukraine ameandika kwenye bango lake ‘In surveys, most of you support the war. So why now are you leaving?’
 
Safi sana. Msg wameipata.
 
Sheria imepitishwa Urusi, ukionesha dalili za kujisalimisha unafungwa jela miaka 10. Hata ukionesha huna nia ya kushambulia adui
Duh!Chap unaonesha hizo dalili na kuingia jela kwa hiyo miaka 10 ambayo kwa uhakika watawala nunda walioko kwa sasa baada ya kitambo kidogo hawatakuwepo tena na sheria hiyo itakosa nguvu itakuwa haina meno. Itatupiliwa mbali na waathirika na sheria hiyo watakuwa huru labda baada ya mwaka mmoja tu.
 
HIMARS zimeongezwa 18

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Nadhani zitachukua muda kufika, maana ndo zinatengenezwa kiwandani.

Mzigo huo (18 HIMARS) ukifika warusi wajiandae tu kuondoka maana watakatiwa supply routes zote kila pembe ya eneo walilojimilikisha

Natamani wangetoa makombora ya masafa marefu (long range) ili washenzi hawa washughulikiwe. Wao wanarusha makombora ya masafa marefu kutokea Russia kwa nini Ukraine isiwajibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…