Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Askari mwenye kuchimba, ameshachoka wakati handaki halijakamilika.Huyo ni askari goigoi sana. Hajui siku wala saa Ukraine atatinga hapo au mtifuano utaanza halafu anakuwa mdebwedo hivo.
Atakuwa ana njaa, yuko hoi . Mtu kama huyo atupiwe bomu moja tu, anaiomba msamaha Drone😂😂😂
 
Poland wamevunja sanamu nne za kumbukumbu za Vita ya pili ya dunia zinazo husiana na Urusi na viongozi wake ikiwa ni moja ya hatua kupinga Urusi kuivamia Ukraine.
Your browser is not able to display this video.
 
Urusi wameomba Nchi za Magharibi zisaidie kuishawishi Ukraine ili iweze kukubali kukaa meza ya mazungumzo. Ukraine haitaki mazungumzo ya kufanya mikoa iliyo mpakani mwa Ukraine na Urusi kuwa Urusi. Ukraine inataka mazungumzo ya jinsi Urusi itaondoka Ukraine na kulipia gharama za Uharibifu

Sergei Lavrov Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi
 
"..............Ukraine inataka mazungumzo ya jinsi Urusi itaondoka Ukraine na kulipia gharama za Uharibifu......."
Excellent. Hilo ndilo la msingi sana. i.e. Mrusi akubali kuAcha vita, ku Ondoka Ukraine, kuLipia gharama za uharibifu then ndio mazungumzo yafanyike.Hizo ndio conditions for enabling the discussions. Tofauti na hapo, kipondo kikali kiendelee. Apigwe kama ngoma.
Yumkini huyu jamaa amechanganyikiwa mazima. Juzi kati hapo kajaribu kusema eti wakubaliane na Ukraine akae katika mikoa 4 aliyoteka kwa muda wa miaka 7 halafu ndo aondoke. Leo ameenda kulia-lia kwa nchi za Magharibi Wamshawishi Ukraine akubali mazungumzo. Kesho atasema nini?-hatujui. Huyo mpuuzi mpuuzeni.
 
Unajua hizi Video tunapost zinaacha alama(geolocation). Hawa Warusi walipost Video wakijitapa huko Bakhmut, Ukraine wakaichunguza na kugundua wapo latitude na Longitude 48°33'27.59"N, 38° 4'55.52"E. Wote wakateketezwa. Hili kosa tu la Technology. Ndo Maana Kherson wanataka picha zisipostiwe muda huo huo majeshi yalipo.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…