Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Mh! Inaelekea kuna dalili za upotoshaji wa habari. Ni vyema kuchuja na kupata uhakika wa ukweli wa Taarifa kabla mtu hajaituma hapa.esp. zile taarifa zinazokinzana na Lengo kuu la kuanzishwa kwa Uzi huu.Tumekuwa tukiziamini Taarifa zitolewazo na Figganigga kwani tangu mwanzo yupo na sisi kutuhabarisha ikiwemo kutuma picha za uthibitisho wa kile anachokisema/andika. Tunawaomba wale wanaosaidia jukumu hilo, basi wajiridhishe kwanza na Uhalisia/Ukweli wa Taarifa wanayoitoa. Mkuu Figga, tunakuomba Uendelee na majitoleo yako - tunakusikiliza na tunaziamini zaidi Taarifa zako. Asante; Ni hayo tu.
Tumekuwa pamoja siku zote na umekuwa ukinitia moyo. Siwezi kucover nchi yote ya Ukraine sababu kila sehemu ni vita. Mtu anaweza akapata taarifa mapema kabla yangu. Hivyo ni vizuri ataje sehemu na muda ili tuweze kuhakiki. Kuna sehemu majeshi ya Ukraine yanazidiwa na Kuretreat, Ila hadi rais aseme. Kwa wiki sasa sijapata taarifa ya Ukraine kuretreat Donetsk ndo maana nikaomba chanzo cha habari ili tuweke kumbukumbu sana. Tangu August hakuna Frontline ya Ukraine imerudi nyuma bali wanaonga mbele. Japo kuna sehemu unakuta kusonga mbele ni mtihani. Mfano Luhansk kuna wiki ilichukua siku 10 kusonga mbele Km 20. Urusi wana Vifaa na nguvu ila hawana akili na hii ndo bahati ya Ukraine.
 
Huyu bwana yupo makini sana - kwa kweli anastahili pongezi. Hii shughuli ni ngum' ati na halafu ni ya hatari sana. Kongole Figganigga.
Pamoja sana. Mfano Mariupol tangu Danny apoteze maisha, kumekuwa giza, hatujui kinachoendelea japo leo tulipata Video za Wanajeshi wa Urusi wakitokea Mariupol kwenda Donetsk kuongeza nguvu
 
Colonel Serhiy Cherevaty wa Ukraine upande wa Mashariki, amesema wameua Warusi 100 leo huko Bakhmut. Ni chanzo changu cha kuaminika
20221107_203107.png
 
Bakhmut hakuna Umeme, maji wala Gesi leo. Ila sio tatizo kwa Frontline.. Mambo yatakaa sawa. Ukraine wakiwa katikati ya Mji jioni ya leo
Line 4 za Frontline, Urusi hawajatoboa hata moja
 
Ila Warusi wanakufa sana. Kuzunguka Makaburi kutafutwa Mpendwa wako, inabidi utumie gari. Watajua hawajui. Hawa ni mbali na wale wanaobaki maporini
View attachment 2409583
Haya ndio matokeo ya maamuzi ya mwendawazimu mmoja kutaka kujionesha ni mwamba na mbabe.Ametweza roho za waliolala hapo bila sababu za msingi - eti hataki nchi yake iwe karibu au ipakane na nchi yenye influence ya NATO/USA. Mwoga sana huyo jamaa.
 
Back
Top Bottom