Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Baada ya kuona muda kuretreat umeisha na Azov wanasonga kwa nguvu, kikosi cha anga cha Urusi 76th division kiliamua kulipua Vifaru vyao ili visiangukie mikononi mwa Azov. Kumbuka Azov ndo walitangulia kusafisha njia
Your browser is not able to display this video.
 
walikuwa kwenye utawala wa kijeshi under Russia. Sasa wako huru, walilazimishwa kufanya vitu ambavyo hawataki.
Sasa watafanya vitu vile ambavyo wamekubaliana kwa pamoja au vile vitu roho binafsi inavitaka alimradi haviendi kinyume na matakwa ya wenzako au sio vinavyokinzana na Taratibu mlizojiwekea.
 
Hilo tuwaachie wazee wa HIMARS waliamulie; lakini kiukweli ni kwamba Mrussi hapo alipo tayari keshapata kipanda uso, suruali hazienei tena kiunoni-wote ni mlegezo mtindo mmoja. Anaswagwa kama mbuzi goigoi anayepelekwa mnadani. 😁
 
Kuna Warusi waliamua kujichanganya na Raia wa Kherson. Sasa leo wameanza kuwachomoa mtaani. Bora Warusi wajisalimishe. Huyu sijui kapelekwa wapi.
View attachment 2414596
Watasema nia yao ni nini:- Hawataki kurudi Urussi au
Wafuate Taratibu zilizopo sio kujichanganya / kufichama kwenye raia. Lakini wapewe japo mkongoto wa uhakika sio mbaya ili wateme nyongo.
 
Denys Myronov alikuwa deputy commander wa Kherson defence unit. Alikataa kushirikiana na Urusi, wakamtesa sana. Amefia mikononi mwa Warusi walipokuwa wamemshikilia. Huyu ni Mfungwa wa Kivita, kwanini wamuue? Mbona sisi wanaojisalimisha tunaachia wanarudi kwao? Ndo maana nawaelewa Azov
 
Dah! Wanapasua raha katika msitu wa huzuni na simanzi kwani wapo walioondokewa na wapendwa wao na uharibifu mkubwa uliofanyika bado ukingalipo unaonekana wazi machoni. Lakini wanayo kila sababu ya kufurahi kwa vifijo na nderemo kwa kuwa wamevipiga vita kwa ujasiri mkubwa na mwendo wameumaliza. Sasa ni kuamka na kuvaa mavazi na mataji ya ushindi na furaha kuu. Adui amebwagwa chini na kutokomezwa mbali kabisa. Mungu ibariki Ukraine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…