T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 12,362
- 41,886
Urusi atakuwa na mbinu za kivita ila hakui kiteknolojia wala hana budget. Uchumi wa Urusi hauna mpango wowote kukua zaidi ya sasa, wawekezaji ndio hao wamekimbia na gesi ndio hiyo Ulaya hawatanunua tena. Hakuna namna jeshi la Urusi litakua, watabaki na mbinu kwenye makaratasi.Ila China hajawahi kuwa kwenye vita yoyote ya maana hivi karibuni, hivyo hana uzoefu.
Urusi baada ya hii vita miaka 20 ijayo atakuwa vizuri
Hatavamia kama alivyovamia hivi juzi
Jambo kubwa zaidi linaloathiri jeshi lao ni rushwa na ubadhirifu wa bajeti. Fedha zinazotengwa kufanya modifications na kununua zana zinapunguzwa na maofisa. Vita inafika vifaru vingine havina ERA blocks vingine wameweka fake kuficha wizi au wamenunua cheap materials ambazo ni deadly kwa wanajeshi.
Na siasa zinaliharibu jeshi, matamko ya tambo ambayo hayatekelezeki. Niliwaambia watu mwaka jana pale ilipozinduliwa Sukhoi 75 Checkmate kwamba ile ndege hata tukae miaka 10 ijayo haitotengenezwa wakati serikali mwanzo ilisema itaanza first flight mwaka 2023. Mwaka huu wamesogeza first flight iwe 2024 na initial production iwe 2027. Nina uhakika hata 2031 hiyo ndege haitokuwa tiyari kabisa. Kama Mig-35 Fulcrum F imewashinda mass production walikuwa wanambembeleza Mchina ainunue wapate additional funds kusawazisha price per unit, sembuse ndio waifanikishe Chekmate mapema hivi.
Wanataka iwe for export ila majeshi duniani hayanunui silaha isiyotumika sana maana hata modifications hakuna, critical spare parts zinaweza kosa, na gharama kubwa ya hizo spare kwa vile hakuna economy of scale.
Urusi inahitaji kiongozi mzuri kiuchumi na kiteknolojia kwa sasa, habari ya kuwa superpower bila uchumi na teknolojia wakubali haiwezekani. Spirit yao ni ileile wakipata nguvu katika hayo ndio waje kusumbua tena miongo ijayo.
China haijawahi pigana ila ina teknolojia kubwa, population kubwa na muhimu zaidi ina nguvu kiviwanda. Ukiivamia China inaweza ita hata watu milioni 30 wapewe mafunzo wakati wanajeshi wake zaidi ya milioni 2 wanakukabili. Unaharibu silaha zake kwenye battle ila huku nyuma viwanda viko busy kuunda nyingine na uzuri population yake ni very skilled ikiwa na uzoefu na mwamko wa kuchapa kazi, kwanza serikali inaweza lazimisha wafanye kazi hata masaa 14 kwa siku na wakakubali jinsi walivyozoea kuburuzwa.
Marekani iliingia WW2 haikuwa imepigana vita kabla ila ilifanya vizuri. Imperial Russia ilipigwa na Japan wakasuruhishwa na Marekani kisha ikaingia WW1 ikapigwa tena na experience yake. You see