Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Ila China hajawahi kuwa kwenye vita yoyote ya maana hivi karibuni, hivyo hana uzoefu.
Urusi baada ya hii vita miaka 20 ijayo atakuwa vizuri
Hatavamia kama alivyovamia hivi juzi
Urusi atakuwa na mbinu za kivita ila hakui kiteknolojia wala hana budget. Uchumi wa Urusi hauna mpango wowote kukua zaidi ya sasa, wawekezaji ndio hao wamekimbia na gesi ndio hiyo Ulaya hawatanunua tena. Hakuna namna jeshi la Urusi litakua, watabaki na mbinu kwenye makaratasi.

Jambo kubwa zaidi linaloathiri jeshi lao ni rushwa na ubadhirifu wa bajeti. Fedha zinazotengwa kufanya modifications na kununua zana zinapunguzwa na maofisa. Vita inafika vifaru vingine havina ERA blocks vingine wameweka fake kuficha wizi au wamenunua cheap materials ambazo ni deadly kwa wanajeshi.

Na siasa zinaliharibu jeshi, matamko ya tambo ambayo hayatekelezeki. Niliwaambia watu mwaka jana pale ilipozinduliwa Sukhoi 75 Checkmate kwamba ile ndege hata tukae miaka 10 ijayo haitotengenezwa wakati serikali mwanzo ilisema itaanza first flight mwaka 2023. Mwaka huu wamesogeza first flight iwe 2024 na initial production iwe 2027. Nina uhakika hata 2031 hiyo ndege haitokuwa tiyari kabisa. Kama Mig-35 Fulcrum F imewashinda mass production walikuwa wanambembeleza Mchina ainunue wapate additional funds kusawazisha price per unit, sembuse ndio waifanikishe Chekmate mapema hivi.
Wanataka iwe for export ila majeshi duniani hayanunui silaha isiyotumika sana maana hata modifications hakuna, critical spare parts zinaweza kosa, na gharama kubwa ya hizo spare kwa vile hakuna economy of scale.

Urusi inahitaji kiongozi mzuri kiuchumi na kiteknolojia kwa sasa, habari ya kuwa superpower bila uchumi na teknolojia wakubali haiwezekani. Spirit yao ni ileile wakipata nguvu katika hayo ndio waje kusumbua tena miongo ijayo.

China haijawahi pigana ila ina teknolojia kubwa, population kubwa na muhimu zaidi ina nguvu kiviwanda. Ukiivamia China inaweza ita hata watu milioni 30 wapewe mafunzo wakati wanajeshi wake zaidi ya milioni 2 wanakukabili. Unaharibu silaha zake kwenye battle ila huku nyuma viwanda viko busy kuunda nyingine na uzuri population yake ni very skilled ikiwa na uzoefu na mwamko wa kuchapa kazi, kwanza serikali inaweza lazimisha wafanye kazi hata masaa 14 kwa siku na wakakubali jinsi walivyozoea kuburuzwa.

Marekani iliingia WW2 haikuwa imepigana vita kabla ila ilifanya vizuri. Imperial Russia ilipigwa na Japan wakasuruhishwa na Marekani kisha ikaingia WW1 ikapigwa tena na experience yake. You see
 
Kama kuna nchi itawekeza kupitiliza katika jeshi kwa kutambua aina ya jirani iliye naye basi nchi hiyo ni Ukraine. Huenda wakafufua hadi nyuklia walizo-abando miaka ya 90. Inaenda kuwa one of the military super powers.
Zile nukes waliziharibu na ni Marekani ilitoa hiyo budget. Ukraine at that time haikuwa na bajeti ya kufanya maintenance ya zile silaha zingeleta ajari siku moja. Kumbuka Chernobyl ni ya kwao hivyo walikuwa ba wasiwasi. Marekani yenyewe iliona wasivyo na hela wanaweza uza teknolojia kwa rogue states kama North Korea na Iran au wakauza warheads. Tatizo Marekani hakuruhusu Ukraine wabaki angalau na missiles chache au warheads. Na silos zote waliharibu. Wataalamu wenyewe washazeeka na kufa na wengine walinunuliwa China uko.

Nchi pekee inayoweza kutengeneza nuke kwa haraka from scratch ikiamua ni Japan ila katiba hairuhusu. Hawana maandalizi yoyote ila wakianza leo within 2 years nuke wanayo.
 

Baridi ina athali pande zote ukraine na urusi pia, na itakuw na faida kwa ukraine zaidi kuliko russia kwa sababu tayari ukraine amem contain russia hana madhara tena ya kuharibu miundombinu ambayo russia alitaka aitumie kushinikiza wa ukraine hasa raia wa kawaida .

Kuikamata kherson na logistics hub nyingi kama iziyum itamfanya urusi apate tabu ku deliver ammo , fuel na hata food shelter supplies

Kwa jinsi urusi alivyokurupuka sidhani kama amejiandaa kwa majira ya baridi na ndo maana recently alitaka kupiga miundombinu hasa energy na maji ili ukraine apate tabu (hajafanikiwa)

Wale mobilised wa urusi hawana morale na hawana uzoefu , hii ni hatari sana maana baridi itawaongezea mazingira magumu itapelekea wapigwe sana au wajisalimishe

All in all baridi ita slow down vita na since urusi anaelekea kuwa na hali mbaya kiuchumi basi ni wazi ukraine ana ka advantage, kumbukeni ana support kubwa toka EU

Note: Hali ya hewa ilikuwa ni factor moja kubwa iliyo mslow down hitler kuikamata moscow , bila baridi ile na mvua nyingi hitler angeikamata moscow vizuri kabisa na russia ingekuwa chini ya germany
 
You nailed it. πŸ‘Œ
 
You made a point.
 
Kitakachofuata ni vikwazo vya nguvu na kuilipa Ukraine compensation for the next 100 years, Russia atalipa hili deni kwa miaka mingi sana ijayo hata baada ya Putin kuondoka, Germany kamaliza juzi tuu kulipa deni lake la ukorofi wa Hitler na ndio maana Germany hana hamu na vita na mtu yeyote, Iraq bado wanalipa ingawaje naona wameonewa tuu lakini ndio hivyo ukiingia anga za US right or wrong lazima akukomeshe tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…