Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

cruise missile ya Urusi ikielekea Kyiv
View attachment 2417637
Katika makosa ambayo Russia anayafanya na kufanya kila nchi imlaumu (condem)ni kurusha makombora maeneo ambayo hakuna vita, kwa Lengo la kuharibu miundo mbinu na kuua raia. Angekuwa inaelekeza makomba yake kwenye military base, maghala ya silaha na kwenye battlefield hakuna ambaye angemlaumu.

Hii ndo inamfanya awahishwe kufurushwa maeneo aliyovamia kwa sababu washirika wa Ukraine ndo wanapata concern ya kumpa silaha nzito zaidi ili ajilinde. Kwa kifupi ni kama analisaidia jeshi la Ukraine kuwa imara zaidi na kuwa na system za ulinzi nzuri zaidi.
 
Ni muda UNO na USA kumkabidhi Ukraine makombora ya kufika Urusi maana hii ni dharau...
Kweli mkuu. Angeonjeshwa kidogo tu ili naye ayasikie maumivu na ajifunze. Ila sasa raia wa kawaida (wasio wanajeshi)wa Urussi sio walengwa. Kwa mantiki hiyo Tutakuwa nasi tumefanya kosa sawa na Mrussi na hivyo hatutaweza tena kumlaumu Mrussi kwamba hazigatii sheria za vita na tutampa Mrussi fursa ya kutupa makombora randomly nchini Ukraine.
 
Wakimkabidhi makombora ya masafa marefu ya zaidi ya 300km, Ukraine kwa hasira alizo nazo atapiga Moscow na miji mingine muhimu.
Hasira -Hasara. Hilo Ukraine akifanya hivyo litampa Urussi Uhalali wa hicho anachofanya kwa sasa i.e. urushaji wa makombora kwenye maeneo yasiyo na vita.
 
Tunapiga maeneo yenye nukes ili aonje utamu wake
 
UN hana makombora

US naona kakubali mpatia Drone zinazoweza ruka hadi Moscow na kufanya mashambulizi, ila kwanza anataka toa technology kadhaa ili hata ikikamatwa basi reverse engineering isifanyike
Safi sana
 
Wakimkabidhi makombora ya masafa marefu ya zaidi ya 300km, Ukraine kwa hasira alizo nazo atapiga Moscow na miji mingine muhimu.
Ndiyo ili waonge radha ya vita ...yaani akipiga vyanzo vya nishati nasi tunajibu
 
Kyiv hakuna Umeme. Wananchi hawalalamiki sababu wanajua Nchi ipo Vitani. Ni vyema hatuna umeme na hatuna Warusi hapa kuliko tuwe na umeme na Warusi wawepo. Urusi leo ilituma missiles 100 kwenye miundombinu na Makazi ya watu. Nisisikie mtu anawalaumu Azov
 
Hakuna wakulalamika kabisa. AZOV wanatekeleza jukumu lao kwa weledi wa kiwango cha juu. Mrussi hastahili kuonewa huruma hata kidogo kama punje ya haradali.
 
Pamoja na kupiga makombora zaidi ya 85, lakini mengi yamedakwa. Yaliyo penetrate ni machache sana.

Siku NASAMS zote zikitua Ukraine, Makombora yake hayatamsaidia tena. German nao wakituongezea IRIS-T waliyoahidi Anga litakuwa salama zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…