Hili ni tatizo au tuseme ni changamoto kwa baadhi ya washiriki kutokusoma Utangulizi wa uzi huu au page # 1. inayoeleza na kufafanua lengo na madhumuni ya kuanzishwa kwa uzi huu.
Mimi nia ya Uzi ni kupost picha za vitani. Sema nimechagua upande wa Ukraine. Mimi sina tatizo na Urusi, sema sijapenda Urusi kuvamia Nchi ndogo kama Ukraine. Pia nimefurahiahwa na jinsi Ukraine ilivyo simama imara kutetea ardhi yake kuchukuliwa na Urusi.
Urusi ilitaka iteke Ukraine yote na iweke viongozi wake. Kama ambavyo walikuwa wamefanya Kherson.
Urusi arudi kwake. Kama kuna tatizo la mipaka, Ashitaki umoja wa mataifa.
Ukraine haiwezi ichokoza Urusi sababu haina uwezo na haiwezi kuigopa Urusi sababu Ukraine ni Nchi huru.
NOTE: Hii thread sijaianzisha ili kubishana na watu wala kuleta propaganda japo naonekana kama nafanya propaganda.
Nazungumzia kinachoendelea kambi ya Ukraine sio yote bali naongelea mafanikio.
Mfano ndege ya Ukraine imeangushwa sio mafanikio ya Ukraine hivyo siwezi kupost sababu huwa Wanaounga mkono Urusi wanapost.
Lakini chopa ya Urusi ikiangushwa napost. Mimi nimechagua upande. Siwezi kuwa simba na yanga wakati mmoja. Mimi ni Pro Ukraine, ukinikata damu itatoka imejiandika Ukraine.
Hii ni thread yetu sisi Pro Ukraine. Watu watuache tujadili jambo letu.
Urusi ana uwezo wa kuipiga Ukraine, lakini hii Vita Urusi hatashinda. Quote me. 💪