Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Mkuu,tunaomba utupatie walau rough figure ya askari wa Urussi waliouawa kwenye hilo la wimbi baada ya wimbi la askari wengi wa Urussi wanaotumwa licha ya vifo vingi. Unataka kutuambia kwamba ni kweli askari wa Urussi wanakufa kama sisimizi lakini bado Mrussi anatuma wengine tena na tena kana kwamba hapo Mrussi ameamua askari wake wakateketezwe tuu hakuna shida???!! Ni uamuzi au mkakati wa namna gani huo? 😳
 
Kweli Mashabiki wa Urusi hamjielewi. Yaani hata Frontline wa Ukraine wakipiga picha zao inawauma? Na ntaendelea kupost na ntaendelea kupost za Mizoga ya Urusi ili mvimbe hadi mpasuke. Hata hivyo hii ni thread ya picha na Video sio ya propaganda.
Hili ni tatizo au tuseme ni changamoto kwa baadhi ya washiriki kutokusoma Utangulizi wa uzi huu au page # 1. inayoeleza na kufafanua lengo na madhumuni ya kuanzishwa kwa uzi huu.
 
Hili ni tatizo au tuseme ni changamoto kwa baadhi ya washiriki kutokusoma Utangulizi wa uzi huu au page # 1. inayoeleza na kufafanua lengo na madhumuni ya kuanzishwa kwa uzi huu.
Mimi nia ya Uzi ni kupost picha za vitani. Sema nimechagua upande wa Ukraine. Mimi sina tatizo na Urusi, sema sijapenda Urusi kuvamia Nchi ndogo kama Ukraine. Pia nimefurahiahwa na jinsi Ukraine ilivyo simama imara kutetea ardhi yake kuchukuliwa na Urusi.

Urusi ilitaka iteke Ukraine yote na iweke viongozi wake. Kama ambavyo walikuwa wamefanya Kherson.

Urusi arudi kwake. Kama kuna tatizo la mipaka, Ashitaki umoja wa mataifa.

Ukraine haiwezi ichokoza Urusi sababu haina uwezo na haiwezi kuigopa Urusi sababu Ukraine ni Nchi huru.

NOTE: Hii thread sijaianzisha ili kubishana na watu wala kuleta propaganda japo naonekana kama nafanya propaganda.

Nazungumzia kinachoendelea kambi ya Ukraine sio yote bali naongelea mafanikio.

Mfano ndege ya Ukraine imeangushwa sio mafanikio ya Ukraine hivyo siwezi kupost sababu huwa Wanaounga mkono Urusi wanapost.

Lakini chopa ya Urusi ikiangushwa napost. Mimi nimechagua upande. Siwezi kuwa simba na yanga wakati mmoja. Mimi ni Pro Ukraine, ukinikata damu itatoka imejiandika Ukraine.

Hii ni thread yetu sisi Pro Ukraine. Watu watuache tujadili jambo letu.

Urusi ana uwezo wa kuipiga Ukraine, lakini hii Vita Urusi hatashinda. Quote me. 💪
 
Nimekuelewa mkuu. Kweli -"Urusi ana uwezo wa kuipiga Ukraine, lakini hii Vita Urusi hatashinda. Quote me. 💪" Yani ni kama kusema ni vigumu sana kumpiga mtu aliye nyumbani kwake. Ni tofauti kabisa na ile ya kupigana na mtu njiani, barabarani au kilabuni. 💪
 
HII THREAD SI YA KUSHINDANISHA URUSI NA UKRAINE BALI PICHA NA VIDEO ZA MAFANIKIO YA UKRAINE WALIO FRONTLINE VITANI.
Naamini sasa imeeleweka na hatutegemei tena kusoma comments zenye mwelekeo wa mashindano, propaganda au maswali ya kwa nini hazioneshwi picha na video za mafanikio ya Urussi.🔨
 
Msemaji wa Ukraine upande wa Mashariki Colonel Serhiy Cherevaty, amekanusha habari zinazosambazwa na Uruai kwamba Soledar ipo chini ya Urusi. Alikuwa akiongea na Wanahabari

Naliamini jeshi la Ukraine. Hawatoi habari za Uongo. Wakiretreat wamasema.
 
Huyu yupo Frontline mjini Soledar. Anasema anashangaa habari za Urusi kusema Soledar imechukuliwa na Urusi. Amekiri kwamba mapambano ni makali ila Ukraine bado inalinda frontline yake na hawajaretreat. Hapo alipo ni Soledar. Angefikaje kama ingekuwa chini ya Urusi?
Your browser is not able to display this video.
 
1. Makanali Generali wa Urusi wanatekeleza agizo la Putin kuwa anataka Bakhmut ikombolewe.

2. Wagner kupoteza Bakhmut ni fedheha sana kwao, maana wao wanaipigiania DONBAS kufa na kupona ili kumfurahisha mwajiri (Putin) wao kwa kuwa ndo ajira yao ilipo. Kuondoshwa kwa Urusi DONBAS ni kushindwa kwa Wagner. Wagner wanajiona kuwa wao ndo wapiganaji imara na wenye uzoefu kwenye vita kuliko jeshi la Urusi.

3. Bakhmut ni strategic logistic area au military Hub, wakiichukua Bakhmut ni rahisi kusonga mbele na kukamata miji mingine. Kwa lugha rahisi Bakhmut ni makutano ya njia za kwenda miji mingine.

4. Bakhmut na DONBAS kwa ujumla ndo eneo lenye utajiri wa rasilimali. Wagner wanavuna rasilimali hizo na zinawasaidia kupata pesa nyingi na kununulia silaha pamoja na kulipa wanajeshi wao.

Hata kama Ukraine troops watalazimika ku retreat Bakhmut lazima wataikomboa tu Bakhmut siku siyo nyingi. Wagner wame deploy very professional and experienced soldiers eneo la Bakhmut na Soledar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…