Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Inadaiwa Putin kampigia Magoti rais wa China. Bado sijafuatilia kama picha imetengenezwa
20230320_213226.jpg
 
Waukraine walipiga counter offensive ndogo huko Bakhmut kuwarudisha nyuma warusi. Warusi wafa kama kuku

View attachment 2558901
Tarehe 19/03/2023 Wagner walifanya offensive tatu (3) na walifanikiwa kusonga mbele (advance) kama ifuatavyo;

1. Kaskazini magharibi mwa Bakhmut kuelekea Pryvillya barabara kuu ya kwenda Slovyansk, walifanikiwa kua advance sehemu kubwa.

2. Magharibi mwa Bakhmut kuelekea Hryhorivka, Wagner walifanikiwa ku advance wakakaribia mji wa Hryhorivka.

Lengo la Wagner kufanya offensive hizo mbili (2) lilikuwa ni kuhamisha concentration ya Ukrainian troops kulinda katikati ya mji wa Bakhmut ambapo wanajaribu kuuzingira ili wenzao wafanye offensive kubwa kusonga katikati ya mji kutokea kusini mwa Bakhmut.

3. Offensive nyingine waliyoifanya Wagner 19/03/2023 na kufanikiwa kuchukua mji wote wa Krasnohorivka na kusonga mbele zaidi kuelekea mji wa Berdychi ambao uko kaskazini magharibi mwa Avdiivka. Wanajaribu kuizunguka (encircle) Avdiivka. Ukraine wakiendelea kufanya uzembe huo wanahatarisha Avdiivka kuzungukwa na kuchukuliwa na Russia. Ukraine ilifanya uzembe Bakhmut, kosa lile lile wanataka kulirudia Avdiivka.

Narudia kusema tena USA, NATO na EU waharakishe kuipa ukraine silaha nzito mapema. Wanawakatisha tamaa wanajeshi wa Ukraine. Wawape silaha wawafurushe hawa Wagner/Russia.
 
Inadaiwa Putin kampigia Magoti rais wa China. Bado sijafuatilia kama picha imetengenezwa
View attachment 2559692
Kwa hali mbaya aliyo nayo Putin, mimi sitashangaa kuipigia magoti china. China ndo taifa pekee lenye uchumi mkubwa kuweza kumsaidia kijeshi na kumpa raw materials ya kutengenezea silaha. Hii vita ikifika December Russia itakuwa na hali mbaya. Vita hii ali undermine, alifikiri atachukua Ukraine kama ilivyochukua Crimea.
 
Teh teh 😂😂 sio rahisi hivyo...
Kweli sio rahisi hivyo lakini inawezekana ikiwa atakuwa amebanwa mbavu kama chatu anavyombana mbwa. Hebu fikiria: Putin, Mamluki aliowakodi (Wagner) pamoja na mbwembwe zao lakini bado hawajafanya la maana bali wanateketea mno wengi; Putin anayo RB ya ICC- kwa maana hiyo hawezi kutoka kwenda mbali zaidi ya nyumbani au kwa majirani marafiki au makoloni yake; Miundombinu ya umeme imeanza kushambuliwa na maadui walio ndani ya Urusi; Putin anajua kwamba siku Ukraine akipata silaha alizohitaji itakuwa ndo mwisho wake; lakini zaidi Putin anajua kwa uhakika hiyo vita haitakaa iishe kama hataondoka katika maeneo ya ardhi ya Ukraine. Mwisho Putin analiona DENI kubwa litakalomkabili la kulipa fidia kwa Uharibifu alioufanya huko Ukraine ilhali uwezo alokuwa nao ameshautumia vibaya kwenye vita ya kipuuzi.
 
Ukraine isipokuwa Makini Avdiivka itaanguka mapema zaidi ya Bakhmut. Kitendo cha kuhamisha mifumo ya Ulinzi na baadhi ya Wanajeshi kwenda Bakhmut, naona si sawa. Tayari Bakhmut ina kila kitu internet imekaa Vizuri. Avdiivka wataanza kuishi kwenye mahandaki. Japo Urusi inapelekewa moto kama kawa
20230321_040045.jpg
 
Uzuri ni kwamba, Urusi imetanguliza Mobilized kushambulia Avdiivka. Hapa wanalalamika kwamba 70% wamepungua kwa kuuawa, kutekwa na kujeruhiwa. Wanasema hawana mafunzo ya kitumia Silaha kubwa. Hawa Warusi Wanaomba msaada Avdiivka.
 
Back
Top Bottom