Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Babushka(Bibi) aliwaibia risasi Warusi, Wanajeshi wa Ukriane walipofika amewapa wakazitumie kuwafukuza wavamizi hawa. Ukraine wana umoja sana na wanapendana, kuwashinda si rahisi
 
Nchini Ukrain ni sherehe nchi nzima yaani mrusi kashindwa vita rasmi

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
Hatuwezi sema Kashindwa nchi nzima wakati kuna maeneo kayakalia kimabavu. Wanafurahia kurudi kwa Mji wa bandari Kherson.

Bado hatujashinda hadi tushinde. So wanajeshi wa Ukraine waendelee kukaza, wasiwasikilize orcs wanaodai Ukraine kashinda Nchi nzima
 
Wananchi wa Kherson wamepewa tahadhari wasikusanye Mines, Waachie jeshi ifanye kazi hiyo. Mengine yameachwa kimtego. Hata kama unaona halijategwa, toa taarifa tu
20221112_221721.jpg
 
Sasa Urusi waje Kherson waendeshe zoezi la kura tuone wanapata ngapi
View attachment 2414649
Kha! Kwanza siku yenyewe ya kupiga kura Mahudhurio kwenye vituo vya kupiga kura ni sifuri (0). Watakuwepo Msimamizi wa Uchaguzi, Msaidizi wake na Mgambo wa kulinda Amani (lakini ni analinda masanduku ya kura) basi.
Hatuwezi sema Kashindwa nchi nzima wakati kuna maeneo kayakalia kimabavu. Wanafurahia kurudi kwa Mji wa bandari Kherson.

Bado hatujashinda hadi tushinde. So wanajeshi wa Ukraine waendelee kukaza, wasiwasikilize orcs wanaodai Ukraine kashinda Nchi nzima
Very Nice. Sema ukweli hata kama ukweli huo unauma kuliko kujidanganya au kujifariji.
Asante sana - ngoma bado. Kaza buti.
 
Kwanini Wanajeshi wa Urusi hawana Uchungu na Vifaa vyao vya Jeshi? Wameviacha Kherson vimetapakaa tu. Asante Urusi inaitwa... Tunaenda kuwatwanga navyo Luhansk
 
Hapa ni Urusi huko Belgorod, wanajiandaa kwa kuweka Frontline nchini mwao. Eti wamenusa LEGION wanataka kuvamia Mkoa huo🤣🤣
Kumbuka LEGION ni Warusi, so hii ni Vita yao, wasijesema Ukraine tunawasaidia. Wanataka Putin atoke madarakani. Wanadai kaingiza Nchi Vitani bila sababu
 
Rais wa Ukraine Mheshimiwa Zelensky amesema, ameomba majadiliano miaka miwili kabla ya Vita lakini walikuwa wanamkatia simu. Wanamdharau. Urusi wamekuwa wakiua Wananchi wetu. Sasa hivi jeshi lao limezidiwa na kukosa mwelekeo, eti ndo wanaomba majadiliano.

Putin anataka majadiliano huku ameshika Mtutu wa Bunduki, huku anashambulia Kyiv kwa Missiles. Aweke Silaha chini, aondoke kwenye Ardhi yetu ndipo aombe Majadiliano.
 
Ukraine hataki mambo mengi. Bali anataka mipaka ya Nchi iliyowekwa mwaka 1991 iheshimiwe.

Pili alipwe fidia kwa hasara iliyosababishwa na hii Vita ikiwemo kutengeneza miundombinu waliyo haribu. Na wote waliosababisha uharibifu huu wachukuliwe hatua. Basi.
 
Back
Top Bottom