Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Naona Waukraine wamtandaoni mmefungua uzi wenu ili mjifariji. Mnavyotiana moyo sasa utafikiri mnauhalisia wa kinachoendelea field..

Mnaongea utafikiri watoto yatima yaani....Vita sio movies za Hollywood....Vita havibadirishwi na mapichapicha ya mtandaoni.Anyway poleni sana kwa kinachompata Ukraine..hakuna mtu anapenda vita..hii vita ni zao la watu wa West kujiona wao wanahaki na thamani kuliko watu wengine..kulazimisha values zao na usalama wao mbele...

UKRAINE acha wavune walichopanda kwa miaka mingi.....

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Huyo Figa Ni MTU wa temper Sana ukienda tofauti Na mawazo yake huwa anapanic ovyo.
Huwezi kuja hapa na habari za uongo na uzushi halafu nikae kimya ili nionekane sina Temper.

Post unachojua kuhusu Frontline ya Ukriane sio utuletee habari za Frontline ya Urusi. Huna kinachohusu Ukraine kaa kimya, una habari za Irusi kapost kwenye thread ya Urusi.

Urusi ni Magaidi, Wavamizi, waonevu na mashetani. Siwezi kula nao au kuwavumilia na ushetani wao wa kuleta vita kwenye nchi iliyokuwa inaishi kwa amani.
 
Michezo ya watoto wa Ukraine
FlamDEsXwAEHiOM

FlamDSvXwAM6A7a
Sehemu ya neno ukraine weka nato
Ni Russia vs nato
 
1. Nikiri kuona malumbano yasiyo na mashiko baina ya Pro Ukraine wenzangu. Mtu yeyote anayesimama katika ukweli bila kujali mrengo wake huitwa muungwana.

2. Kwenye vita kuna kushindwa na kushinda, kama ulivyo mpira. Lakini huwezi kupingana na ukweli hata ungekuwa shabiki wa kuvua nguo.

3. Uzi (thread) bila watu wa ku follow hauna maana. Nakubaliana na member mmoja kuwa kuanzisha thread (uzi) siyo kuwa mmiliki wa thread au kuwa na hati miliki ya uzi huo. Kwa vyovyote vile hakuna umiliki halali wa kuanzisha uzi au mada. Ukishaanzisha mada basi haki na uhuru wako unaishia hapo. Mtu yoyote anaruhusiwa kuchangia chochote hata kama ni cha kijinga au kina mauzi au kukerekwa. Haki hiyo hakuna mweñye mamlaka ya kumnyang'anya ili mradi hatumii matusi. Kikubwa ana hoja au hana.

4. Ukweli ni kwamba mji wa Soledar, Bakhmuts'ke, Yakovlvika, Pidhorodne na Optyne iko under full control ya Russia. Pia eneo la Salt mine liko karibu kuzungukwa na majeshi ya Russia. Hata kama tutatumia neno kuwa nì uwanja wa mapambano lakini ukweli utabaki kama ulivyo kuwa tumelemewa eneo hilo. Mimi huwa nachukia propaganda maana ni muumini wa kusema ukweli

5. Ni ukweli usiopingika kuwa direction ya Klishchiivka, Russia ime advance, Lengo lao wanapambana kuizunguka Bakhmut kutokea kusini magharibi mwa Bakhmut.

6. Ni ukweli kuwa kuna mitaa ya mjini Bakhmut Russia wana control, hata kama tutasema ni battle field. Lakini ndo ukweli wenyewe. Kwa kifupi tukubali tu kuwa mapigano ni makali direction ya Bakhmut. Wagner group na kikosi vya Russia wame strengthen military forces.

7. Mimi bado naamini kuwa Ukraine haina vifaa vya kutosha direction hiyo lakini wana uwezo wa kuwapiga warusi. Mzigo mpya ukifika Ukraine, lazima Russia ateme bungo apende usipende.
 
3. Uzi (thread) bila watu wa ku follow hauna maana. Nakubaliana na member mmoja kuwa kuanzisha thread (uzi) siyo kuwa mmiliki wa thread au kuwa na hati miliki ya uzi huo. Kwa vyovyote vile hakuna umiliki halali wa kuanzisha uzi au mada. Ukishaanzisha mada basi haki naa uhuru wako unaishia hapo. Mtu yoyote anaruhusiwa kuchangia chochote hata kama ni cha kijinga au kina mauzi au kukerekwa. Haki hiyo hakuna mweñye mamlaka ya kumnyang'anya ili mradi hatumii matusi. Kikubwa ana hoja au hana.

4. Ukweli ni kwamba mji wa Soledar, Bakhmuts'ke, Yakovlvika, Pidhorodne na Optyne yako under full control ya Russia. Pia eneo la Salt mine liko karibu kuzungukwa na majeshi ya Russia. Hata kama tutatumia neno kuwa nì uwanja wa mapambano lakini ukweli utabaki kama ulivyo kuwa tumelemewa eneo hilo.

5. Ni ukweli usiopingika kuwa direction ya Klishchiivka Russia ime advance, Lengo lao wanapambana kuizunguka Bakhmut kutokea kusini magharibi mwa Bakhmut.

6. Ni ukweli kuwa kuna mitaa ya mjini Bakhmut Russia wana control, hata kama tutasema ni battle field. Lakini ndo ukweli wenyewe. Kwa kifupi tukubali tu kuwa mapigano ni makali direction ya Bakhmut. Wagner group na kikosi vya Russia wame strengthen military forces.

7. Mimi bado naamini kuwa Ukraine haina vifaa vya kutosha direction hiyo lakini wana uwezo wa kuwapiga warusi. Mzigo mpya ukifika Ukraine, lazima Russia ateme bungo apende usipende.

Sababu kubwa ya mafanikio ya adui huko Bakhmut na Soledar ni wale askari waliokimbia kule Kherson, wengi wamepelekwa kule.

Pia nadhani adui ameamua kufanya uamuzi kuwa hakuna kuretreat tena hata kama wanakufa mobilized milioni.

Ila naamini, Vikija vile vifaru vya Leopard kutoka Ujerumani na nchi washirika, Tutakuwa katika position nzuri ya kuwapelekea moto Warusi.

Hofu niliyonayo ni kwamba, inasemekana adui anataka kujaribu tena operation nyingine kutokea Kaskazini, Kule Belarus kipindi cha Spring. I hope Makamanda wa Ukraine wameshajipanga vizuri kuthibiti hiyo situation.

Kwa sasa Tukipata ATCMS za kutosha, Leopard tanks , Patriots na zile Bradley amored vehicles, Tutakuwa pazuri zaidi.
 
1. Nikiri kuona malumbano yasiyo na mashiko baina ya Pro Ukraine wenzangu. Mtu yeyote anayesimama katika ukweli bila kujali mrengo wake huitwa muungwana.

2. Kwenye vita kuna kushindwa na kushinda, kama ulivyo mpira. Lakini huwezi kupingana na ukweli hata ungekuwa shabiki wa kuvua nguo.

3. Uzi (thread) bila watu wa ku follow hauna maana. Nakubaliana na member mmoja kuwa kuanzisha thread (uzi) siyo kuwa mmiliki wa thread au kuwa na hati miliki ya uzi huo. Kwa vyovyote vile hakuna umiliki halali wa kuanzisha uzi au mada. Ukishaanzisha mada basi haki na uhuru wako unaishia hapo. Mtu yoyote anaruhusiwa kuchangia chochote hata kama ni cha kijinga au kina mauzi au kukerekwa. Haki hiyo hakuna mweñye mamlaka ya kumnyang'anya ili mradi hatumii matusi. Kikubwa ana hoja au hana.

4. Ukweli ni kwamba mji wa Soledar, Bakhmuts'ke, Yakovlvika, Pidhorodne na Optyne iko under full control ya Russia. Pia eneo la Salt mine liko karibu kuzungukwa na majeshi ya Russia. Hata kama tutatumia neno kuwa nì uwanja wa mapambano lakini ukweli utabaki kama ulivyo kuwa tumelemewa eneo hilo. Mimi huwa nachukia propaganda maana ni muumini wa kusema ukweli

5. Ni ukweli usiopingika kuwa direction ya Klishchiivka, Russia ime advance, Lengo lao wanapambana kuizunguka Bakhmut kutokea kusini magharibi mwa Bakhmut.

6. Ni ukweli kuwa kuna mitaa ya mjini Bakhmut Russia wana control, hata kama tutasema ni battle field. Lakini ndo ukweli wenyewe. Kwa kifupi tukubali tu kuwa mapigano ni makali direction ya Bakhmut. Wagner group na kikosi vya Russia wame strengthen military forces.

7. Mimi bado naamini kuwa Ukraine haina vifaa vya kutosha direction hiyo lakini wana uwezo wa kuwapiga warusi. Mzigo mpya ukifika Ukraine, lazima Russia ateme bungo apende usipende.
Tatizo ni mtahimili vishindo iwapo tutapost pale tulikung'utwa? Mimi napost mafanikio, sikutaka kujikita tuliposhindwa. Lakini yote yanawezekana. Mkitaka nipost wanajeshi wa Ukraine wakichinjwa kukatwa korodani au kupigwa risasi za kichwa inawezekana.

Mfano hapa chini hii ni video ya Wanajeshi wa Ukraine wawili wakilimwa risasi huko Svatovo Mkoani Luhansk. Je, twende hivi? Haikuwa Malengo ya thread
 
Sababu kubwa ya mafanikio ya adui huko Bakhmut na Soledar ni wale askari waliokimbia kule Kherson, wengi wamepelekwa kule.

Pia nadhani adui ameamua kufanya uamuzi kuwa hakuna kuretreat tena hata kama wanakufa mobilized milioni.

Ila naamini, Vikija vile vifaru vya Leopard kutoka Ujerumani na nchi washirika, Tutakuwa katika position nzuri ya kuwapelekea moto Warusi.

Hofu niliyonayo ni kwamba, inasemekana adui anataka kujaribu tena operation nyingine kutokea Kaskazini, Kule Belarus kipindi cha Spring. I hope Makamanda wa Ukraine wameshajipanga vizuri kuthibiti hiyo situation.

Kwa sasa Tukipata ATCMS za kutosha, Leopard tanks , Patriots na zile Bradley amored vehicles, Tutakuwa pazuri zaidi.
1. Kwa mujibu wa intelligence ya UK, tishio la kuvamia kutokea Belarus halipo, wametumia Neno "unlikely"

2. Inawezekana Wagner waliokuwepo Kherson wakawa wamepelekwa Kreminna na Bakhmut. Lakini they are professional and experienced soldiers. Pamoja na kwamba mobilized wamekuwa deployed wengi.

3. Pamoja na wanajeshi wengi wa Russia kuuawa Bakhmut lakini nashangaa wanashambulia massively. Wanasema mizoga ni mingi kwenye trenches huko Soledar na Bakhmut lakini bado wanakuja kwa kasi. Sijui wamelishwa nini.
 
Tatizo ni mtahimili vishindo iwapo tutapost pale tulikung'utwa? Mimi napost mafanikio, sikutaka kujikita tuliposhindwa. Lakini yote yanawezekana. Mkitaka nipost wanajeshi wa Ukraine wakichinjwa kukatwa korodani au kupigwa risasi za kichwa inawezekana.

Mfano hapa chini hii ni video ya Wanajeshi wa Ukraine wawili wakilimwa risasi huko Svatovo Mkoani Luhansk. Je, twende hivi? Haikuwa Malengo ya thread
View attachment 2478247
1. Hatuna maana kuwa tunataka picha za wanajeshi wetu wakipigwa. Lakini kama mtu ataamua kuweka video ya kututambia kuwa wanatupiga hatuwezi kumfanya lolote maana ni haki yake, sisi tuna ushahidi mwingi sana wa mizoga ya warusi .

2. Mafanikio makubwa waliyoyapata Ukraine kwa jasho na damu ni makubwa mno. Askari wa Ukraine akifa vitani ni shujaa maana kapigania nchi na watu wake kwa uzalendo mkubwa. Mwanjeshi wa Russia kufa kwenye vita hii siyo shujaa maana amekufa bila sababu ya msingi. Ndiyo maana tunasema ukimuua jambazi wewe ni shujaa. Jambazi akikuua unapambania haki yako bado utakuwa shujaa.
 
Mimi ni pro Ukraine. Mkuu wa majeshi hajatangaza kwamba sehemu fulani tumepoteza, kwanini niseme? Sababu taarifa zipo wazi na Jeshi likipoteza linasema. Mfano pale Soledar, rais Zelensky kasema mapambano yanaendelea. Mimi nawasikiliza Viongozi wangu. Siwezi kucheza ngoma ya Pro Urusi. Tuongee vitu tukiwa na chanzo cha habari.

Je, chanzo cha kusema Ukraine imeretreat Soledar ni kipi? Hadi sasa sijaona. Ninachojua Urusi wameadvance kwa mara ya kwanza ndani ya miezi miwili. Hivyo mimi ninachopinga ni watu kuleta habari za upotoshaji ambazo hazijafanyiwa uhakiki. Bora mtu apost kama swali kuliko kuhitimisha kwamba tayari Soledar imechukuliwa wakati sio kweli. Tunawavunja moyo wanajeshi wetu.
 
Chechen wana Vikundi Vinne vinasaidia Ukraine kuoambana na Urusi. Ukiachilia mbali hawa Dzhokhar Dudayev Battalion, Vikundi vingine ni Sheikh Mansur Battalion, Separate Special Purpose Battalion na Ruslan Gelayev Battalion. Wote hawa ni wamoja, wanajiita Peacekeeping.
View attachment 2478103
Slava Ukraine [emoji1255]
 
Back
Top Bottom