Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Special Thread: Video na picha kutoka Vikosi vya Jeshi la Ukraine walio Frontline dhidi ya Urusi

Watakuwa wanajiandaa kwa mission ya kuchukua mji mwingine.
Ila Bakhmut imeharibiwa. Sio mji tena wala Kijiji bali Magofu. Yaani Urusi wanachokifanya ni kubomoa kila kitu kuanzia nguvo za Umeme, Mabomba ya Maji Majumba sehemu za Makumbusho Shule ma kila kitu. Kwamba hata akishindwa upate na wewe hasara. Angekuwa anawatetea watu wa Bakhmut au angekuwa anawapenda Waukraine qa Donetsk asingewabomomolea nyumba zao. Wanabomoa Nyumba Moja baada ya nyingi. Na ikiwa nzuri umepaka rangi ndo hawaiachi
 
Wanaenda kuongeza Nguvu Avdiivka. Wanaamini wataichukua Avdiivka.
Prigozhin anajua Bakhmut itarudi muda si mrefu. Kuondoka kwao wanataka Legacy yao iendelee kuwepo na baadae waje waseme kuwa Wagner wasingeondoka Ukraine wasingeweza kuichukua.
Walijua Bakhmut watateka zana za Kivita na Miundombinu ya Jeshi la Ukraine angalau warudishe gharama lakini wapi. Wameambulia Patupu. Uzuri hii si Mara ya kwanza Bakhmut inatekwa na Mrusi. 2014 Warusi wakitumia Mgongo wa DRP waliiteka Bakhmut lakini si muda mrefu wakaondolewa.
 
Hata Prigozhin amelisifu jeshi la Ukraine kuwa si jeshi la mchezo huku akiliponsa jeshi la nchi yake ya urusi kuwa hamna kitu.
Na kama kweli Wagners wataondoka Bakhmut, Jeshi la Mrusi linaachwa hapo ili limalizwe kama sehemu ya Wagners kujilipizia kisasi kwani Warusi waliwategea sana na kuwatanguliza mbele wakati wa mapambano makali hadi Prigozhin akaanza kulia-lia hapati ushirikiano wa kutosha kutoka kwa Jeshi la Urusi ikiwa ni pamoja na kubaniwa kupata silaha alizaohitaji.
 
Huko Mkoani Krasnodar Nchini Urusi, Drone imevamia Bohari ya Mafuta
20230528_213807.jpg
 
Back
Top Bottom